WanaJF,
Hoja yangu ni kwamba tangu CHADEMA ianze process ya kuchunguza kilichosababisha hawa madiwani kuingia muafaka feki tumeona hatua nyingi zikitumika.
Hatua kama upelelezi hadi jana kufukuzwa.
Lakini nimeona kwamba hatua zote zile wasemaji wamekuwa ni chama au watetezi wa kupinga muafaka.
Binafsi napinga muafaka feki. Lakini, je, inawezekanaje hawa madiwani wasiwe na hoja kabisa waliyoitumia kujitetea toka kika walipopewa nafasi hiyo.
Hivi utetezi wao ulijengwa kwa msingi upi?
Inawezekana nimezembea kufuatilia jambo hili, lakini inaniwia vigumu kuamini kuwa waliofukuzwa hawajui nini maana ya utovu wa nidhamu kwa kuingia muafaka bila ridhaa ya makao makuu. Na wakang'ang'ania utovu huo hadi kufukuzwa!
Nawaomba ili tufunuane akili kwa kujadili kauli zao walizotumia kujitetea kama mahakamani ambako mhalifu hata akitiwa hatiani tuna rekodi ya utetezi wake.