Chadema nayo itapewa label ya 'chama vurugu' na serikali ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema nayo itapewa label ya 'chama vurugu' na serikali ya CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Aug 5, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wadau,
  Kama tunavyoona, moto waliouwasha Chadema baada ya kumteua Dr Slaa kugombea urais umeanza kuwa mkali kila kukicha. Inaonekana kama vile Watanzania wengi wanataka mabadiliko, lakini hiari yaho hii inapigwa vita na chama tawala ambacho kiko tayari kutumia mbinu, na nguvu zote, pamoja na zile za dola kuondoa uwezekano wa matakwa haya.

  Kama vile walivyokifanyia CUF huko nyuma, sasa hivi inaletwa hoja ya udini -- kwamba Chadema ni chama cha Wakristo na kwamba Dr Slaa ni pendekezo la Kanisa (Katoliki). Hii inashangaza kwani hapo nyuma Kanisa hilo liliposema JK ni chaguo la Mungu, hakukuwa na rabsha yoyote -- hasa kutoka kwa Waisilamu.

  Lakini yote hayo hayanipi tabu. Wasiwasi wangu mkubwa ni pale serikali ya CCM itakapoanza kukipaka Chadema label ya "Chama vurugu" -- kama vile walivyokuwa wanafanya kwa NCCR -Mageuzi mwaka 1995 under Mzee Ruksa, na CUF mwaka 2000 under Mkapa.

  Tatizo kubwa la CCM ni kwamba wakikiona chama chochote cha upinzani kinaanza kuwa tishio kwake, basi hutumia jeshi la polisi kukisaidia, na hii ndiyo huwa silaha yao kubwa. Mwaka 2000 mara kadha jeshi la polisi under IGP Mahita lilikuwa linaingilia mikutano ya CUF na kuanza tu kulipua mabomu ya machozi, bila ya sababu yoyote, eti tu kuonyesha tu CUF ni chama cha vurugu tu.

  Chadema waliangalie hilo na wajue namna ya kukabili nalo -- ingawa naamini JK siyo Mkapa, na Saidi Mwema siyo Omar Mahita. Lakini kama tujuavyo, paka ukimkabili sana hadi ukutani atakuparua tu. hana namna nyingine ya kujihami kwani siyo binadamu. Wasiwasi wangu ni huo tu.
   
 2. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Very true bro inabidi Chedema wawe makini na waangalifu kwa sana maana hawa jamaa wa ccm wanapenda sana mchezo mchafu.
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena nimekugongea thanas
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  haijalishi hata wakiwaita chama kinachonuka mwaka huu ni Dr.Slaa tuu hatuambiwi kitu hapa
   
 5. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani kakwambia CUF Hawakufanya Vurugu? kwani watu hawakuona kwa macho yao? je n aZanziba utasemaje?
  kilicho waangusha CUF ni Slogan zao,, " mara Jino kwa Jino" what do they mean?
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Sasa ulitakaje? Ulitaka slogan ya CUF iwe 'polisi kwa polisi' kwani wao wana polisi?
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Well answered Mkuu. Huyu hawezi kuwa na wimbo tena.
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Upo sahihi kabisa mkuu, ila sema watanzania wenyewe tumeshachoshwa sana na huu mfumo uliopo madarakani hivi sasa. Wasiwasi wangu ni kwamba tunaweza kuishia kwenye vurugu kama za Kenya mwaka 2007.

  Mimi na watanzania wengine ambao naamini ni wengi, mwaka huu hatutakubali kuibiwa wala kuonewa katika kile tunachoamini ni haki yetu. Tutapambana! Binafsi nipo tayari kupoteza uhai kwa maslahi ya nchi. Sitaona shida kukabiliana na polisi hata kama ni kwa mawe, ilimradi nijue kwamba wanatufanyia fujo kwa kutuonea.
  Hatuna silaha, lakini umoja wetu itakuwa ni silaha kubwa.

  Mkwawa aliwashinda wajerumani pamoja na bunduki zao walizokuwa nazo. Tukiungana na kukubali kwamba tunataka mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, kiafya, kielimu na maisha kwa ujumla, tutawakabili polisi na hata jeshi. Tunajua waatatupiga risasi lakini hawatatumaliza sisi wote. Wengine wataishi na watafaidi matunda ya damu zetu zitakazomwagika.

  Hata biblia inasema ni sharti punje ya ngano ife ndipo iweze kuzaa. Kifo changu na cha watanzania wengine wapenda nchi kitakuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya wananchi wengine watakaobahatika kuishi. Nitasimama imara kulinda na kutetea uhuru na ustawi wangu na wa nchi yangu.
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hii inaitwa risks identification. Lets identify more risks and advice how thy should be dealt with to avoid unforeseen impacts.
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mimi sisemi mengi kwa kuwa nitasimamia kura za Dr. Slaa, litakalotokea na litakuwa provided kura haziibwi kwa gharama yeyote ile ila zitalindwa kwa gharama yeyote ile.

  Kaeni chonjo safari ya nyie walafi na wezi wa hii nchi.
   
 11. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wao kwa Wao wanachezea rafu ( Rejea Taarifa/Habari Kura za Maoni) ila hawachukuliani hatua koz ni kawaida yao kulindana, so nina uhakika hawatakubali kushindwa at any cost, wanamiliki vyombo vyote vya dola ila hawamiliki haki ya raia na ustawi wake, hawamiliki maamuzi ya umma ila wanayasimamia.

  Kinachotakiwa ni kuipa CHADEMA haki hii ya kusimamia maamuzi ya Uma, kulinda na kuheshimu utawala bora. SLAA kesha onyesha katika level ya ubunge kuwa anaweza na good enough anawajua mafisadi wote, thus why aliwahi kuwataja kwa majina na hakuna hata mmoja aliyekwenda mshitaki mahakamani. Anajua maisha ya watu wa Chini na ninauhakika atasweep mabepari wote serikalini na kuweka watu clean ambao hawatakua na uroho wa kujilimbikizia mali au ktoa maamuzi ambayo yatakua yanaegemea katika maslahi yao na familia zao. Kwa sababu anao uwezo wa KUTHUBUTU then nina uhakika hata akitokea mwenye kuboronga basi kibarua kitaota nyasi fasta.

  Kama uchaguzi utakuwa wa huru na Haki then its SLAA 2010
   
 12. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tupige kura kwa siri na mshindi aibuke kwa minongono na tetesi tuu.
  Mkizomea mtapigwa virungu pende msipende.
  Kashika rungu tafuta njia ya kulikwepa lisikupate.
  Jeshini tunatumia staili ya kupigana vita kwa kujificha na kuvizia unahakikisha adui yako hakuoni mpaka umemmaliza unaweza kubofya hapa http://Camouflage maelezo kwa ya kina.Hata Dr Slaa anajua wako wana ccm wengi watakao mpa suport.
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Chadema take this as an advance information to you.
  We need all of you running a modern and professional campaign. CCM ni balaa.:nod:
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aibu! Sasa ndo watu wanaanza kuona kuwa eti CUF walifanyiwa fujo ila kipindi hicho walikuwa wakwanza kusema kuwa CUF ni watu wa fujo. Kweli siasa bwana! utatetea tu pale utakapokuwa na maslahi binafsi na si kwa taifa kama wengi wanavyojinasbisha humu jf. Yale ya CUF yameshahamia kwa chadema. Mpaka sasa hivi ni chama cha wakatoliki (ila wamejificha yuma ya watu), muda si mrefu kitakuwa ndo chama kinachoongoza kwa fujo. Lakini ni yale yale tu, mkuki kwa nguruwe.... ila mkuki kwa mtu hapo ndo panapokuwa hapatoshi.
   
 15. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NCCR Mageuzi ilibambikwa na CCM mwaka 1995 kuwa ni chama cha Kidini na kuomba Waislam wakikatae kwa kuwa Mrema aliruhusu bucha za Nguruwe na atendeleza udini.
  Mwaka 2000, CCM wakahamisha udini kutoka NCCR kwenda CUF kwa sababu kilikuwa na mvuto mkubwa. wakaeneza siasa za chuki kuwa CUF ni chama cha waislam na kuomba wakristo wakikatae. Ilifika mahala hata waislam wakaanza kuamini kuwa ni chama chao na kujiunga nacho kwa wingi hata CCM wakashtuka tena na kumtuma mzee ruksa kuzungukia sehemu zenye waislam wengi kuwaambia kuwa sheria ya msajili wa vyama inakataza chama chenye muelekeo wa kidini na kukisafisha CUF ili sehemu kama huzo wagawane kura!
  Sasa mwaka huu wanahamishia siasa hiyo chafu ya kuiangamiza nchi kwa CHADEMA wakiomba waislamu wasikipigie kura zao. siku za CCM zitaisha siku Vyama kama CHADEMA na CUF vitakapo unganisha nguvu na kutafuta ridhaa ya kutawala kwa pamoja. Hapo SISIEM watakosa la kusema
   
 16. upele

  upele JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIJUI KAMA WAPINZANI HILI WANATAMBUA KUWA HAWA JAMAA WA CCM HAWANA MPANGO WA KUJUA NANI ATAWASUMBUA WAO WANAWAANDAA VIJANA FULANI KTK MAENEO MAALUUM HIVI SASA WAPO CHIMBONI WANAKULA COURSE YA KUFANYA AMBUSH ILI KUWEZA KUFANIKISHA MALENGO YAO
  WANA JF HILI MWALIJUA BASI HABARI NDIYO HII
  cONQUEST-CCM DAIMA HATA KWA WIZI.SINCE 1961
   
 17. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Usikute hao vijana wakavishwa sare za vyama vya upinzani ili kuleta picha kwamba upinzani ni waleta vurugu.
  Mkuu lete data kamili tujue wapo wapi tuwamulike na kurunzi letu
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  CCm wana utamaduni wa kuwawekea kambi vijana wao ambako wanawafundisha mbinu za kuhujumu uchaguzi mara pale inapoonekana wanazidiwa!!
   
 19. upele

  upele JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI KWELI KUBWA HIYO NI NJIA YAO MOJA WAPO ILA KWA SASA HAO WATU WAPO KANDO YA MJI MAARUFU ETI NDIO KITOVU CHA MARAHA ITAKUWA NGUMU KUBAINI HILO ILA WE TEMBELEA KTK HOTEL ZILIZOKO MAENEO YA BAMBA,BAGAMOYO,BUNJU, WAMEJITENGA NA HAYA KAMA UNAWEZA KAZI KWAKO WEYE NA ROHO YAKO,
  cONQUEST-PESA NI MZURI ILA UACHANISHA MWILI NA ROHO
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mkuu nimekusoma tayari.
  hapo kwenye bold umetuma ujumbe mzito sana wenye kila aina ya ujumbe ndani yake...
  Wadadisi wapo kazini kufukunyua hii ishu
   
Loading...