Elections 2010 Chadema nayo itapewa label ya 'chama vurugu' na serikali ya CCM?

Habari nilizozipata toka huko kilimanjaro zinasema. Katika jimbo la hai anakogombea mh freeman mbowe mwenyekiti wa chadema, kabla ya vurugu zilizotokea masama kulikuwa tena kumetokea vurugu nyingine katika kijiji cha kimashuku, wilayani hai.
Inadaiwa katibu wa ccm wa wilaya alimkamata mwanacham mmoja wa chadema na kumpiga na kumpulizia sumu machoni. Mwanachama huyo wa chadema alitapika na kuzirai. Kisha walimchukua na kumpekeleka kituo cha polisi kwa kutengeneza madai. Hadi viongozi wa chadema walipopata taarifa na kwenda kumtoa mwanachama huyo.

Inashangaza kuwa tanzania yetu imeingiliwa na pepo wabaya. Amani ihubiriwe na tusubiri maamuzi ya haki ya wananchi na tuyaheshimu.
Nadhani wale mnaokemea kwa jina la yesu basi kemeeni pepo wa vurugu tanzania na ikiwezekana fungeni na kuomba.
 
Wacha GREEN GUARDS waendelee kumwaga damu bila vyombo vya usalama kuchukua hatua! The day is coming and i see it coming soon when the first shall be the last and the last first! Haki na kweli vitadhihirika siku hiyo.
 
Matukio ya kuvunjika kwa amani baada ya baadhi ya vijana wa ccm kuvamia na kusababisha umwagaji damu hasa tukikumbuka tukio la mkoani Mara lililotokea juzi yameanza kutoa mwanga zaidi baada ya tukio la kuvamiwa kwa mkutano wa Mbowe huko Hai.

Katika tukio la huko hai ambapo kundi la vijana wa ccm walikuwa na mapanga, na majembe na silaha nyingine walivamia vijana wa chadema ilI kuvuruga mkutano. Kuna kijana mmoja wa ccm aliyekamatwa na akatoa mwanga wa kile ambacho ccm walikuwa wamejiandaa. Inadaiwa kwamba, CCM iliwafanyia mafunzo ya kijeshi vijana wapatao 5000 huko Iringa mwezi March mwaka huu na baadaye kule Moshi Vijijini ambako walitoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana 350.

Tunatoa taadhari kwa umma waangalie kwa makini vikundi vya vijana wanaojiita ni ccm ambao wamekuwa wanatumia silaha za jadi kuharibu mikutano ya wapinzani na hata kusababisha umwagaji damu.

Tusipoangalia kwa makini chama hiki kikongwe kinaweza kuvuruga amani maana inaonekana wamejiandaa kukaa madarakani kwa njia yeyote ile,

Taarifa hii inakuja huku kukiwa na dokezo za mbinu za mafunzo ya uchakachuaji kura ambapo pia vijana kadhaa wamefundishwa jinsi ya kuchakachua huko Mkoani Pwani.
 
Zimbabwe, Malawi under Kamuzu and Muluzi walikuwa na hawa vijana wao watata watupu. We don't want that in Tanzania. Tufike sehemu ya kuogopa kujaribu kuichakuwa amani maana ikiondoka haitarudi.
 
Matukio ya kuvunjika kwa amani baada ya baadhi ya vijana wa ccm kuvamia na kusababisha umwagaji damu hasa tukikumbuka tukio la mkoani Mara lililotokea juzi yameanza kutoa mwanga zaidi baada ya tukio la kuvamiwa kwa mkutano wa Mbowe huko Hai.

Katika tukio la huko hai ambapo kundi la vijana wa ccm walikuwa na mapanga, na majembe na silaha nyingine walivamia vijana wa chadema ilI kuvuruga mkutano. Kuna kijana mmoja wa ccm aliyekamatwa na akatoa mwanga wa kile ambacho ccm walikuwa wamejiandaa. Inadaiwa kwamba, CCM iliwafanyia mafunzo ya kijeshi vijana wapatao 5000 huko Iringa mwezi March mwaka huu na baadaye kule Moshi Vijijini ambako walitoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana 350.

Tunatoa taadhari kwa umma waangalie kwa makini vikundi vya vijana wanaojiita ni ccm ambao wamekuwa wanatumia silaha za jadi kuharibu mikutano ya wapinzani na hata kusababisha umwagaji damu.

Tusipoangalia kwa makini chama hiki kikongwe kinaweza kuvuruga amani maana inaonekana wamejiandaa kukaa madarakani kwa njia yeyote ile,

Taarifa hii inakuja huku kukiwa na dokezo za mbinu za mafunzo ya uchakachuaji kura ambapo pia vijana kadhaa wamefundishwa jinsi ya kuchakachua huko Mkoani Pwani.

Mafunzo ya kijeshi??????
Fujo za kihuni tu hizo ambazo police wanatakiwa wadhibiti mara moja! Tusikuze mambo.
 
siniulize source, lakini nalazimika kusema ukweli kwani nafsi inanishitaki

Vurugu nyingi zinazotokea kwa sasa ni mbinu za ku-destruct wanaCHADEMA na mikutano na kuvuruga amani

Lengo sio tu kuwafanyizia wagombea wa chadema, bali lengo baya zaidi ni kuharibu muendeleo mzima wa kampeni

KIBAYA SANA KWA SASA NI ILE VIONGOZI WA CCM KUWATUMIA RAIA MASIKINI, WASIO NA KITU KUUMIA NA KUPOTEZA MAISHA HUKU VIONGOZI WAKIWA HAWANA HATA LEPE LA MAJONZI.. makatibu wa ccm wanajua

  • je mmesikia any condemnation from higer authorities za ccm?
  • je mmeshanoti hizi coincidence za wanaccm kuwa kwenye misafara isiyoeleweka wakikatiza karibu na mikutano ya chadema?
  • wakizidi yatatoka mengi

mods mnaweza kuondoa kama mnaona haina tija, ila sitatoa source...
 
ACID uko sahihi bana...why mod aondoe? mambo hayo ya CCM na upunguwani wao ndo unapelekea fujo...Nimefurahishwa sna sana na watu wa MASWA kumtwanga yule dereva na kumuuwa.maana wamezidi CCM
 
ACID uko sahihi bana...why mod aondoe? mambo hayo ya CCM na upunguwani wao ndo unapelekea fujo...Nimefurahishwa sna sana na watu wa MASWA kumtwanga yule dereva na kumuuwa.maana wamezidi CCM
thanks mkuu, ila napinga kuuaana wakati tunawapigania wamekaa kwenye viota vya mabilioni

why am i in this??? nahisi presha aisee
 
siniulize source, lakini nalazimika kusema ukweli kwani nafsi inanishitaki

Vurugu nyingi zinazotokea kwa sasa ni mbinu za ku-destruct wanaCHADEMA na mikutano na kuvuruga amani

Lengo sio tu kuwafanyizia wagombea wa chadema, bali lengo baya zaidi ni kuharibu muendeleo mzima wa kampeni

KIBAYA SANA KWA SASA NI ILE VIONGOZI WA CCM KUWATUMIA RAIA MASIKINI, WASIO NA KITU KUUMIA NA KUPOTEZA MAISHA HUKU VIONGOZI WAKIWA HAWANA HATA LEPE LA MAJONZI.. makatibu wa ccm wanajua

  • je mmesikia any condemnation from higer authorities za ccm?
  • je mmeshanoti hizi coincidence za wanaccm kuwa kwenye misafara isiyoeleweka wakikatiza karibu na mikutano ya chadema?
  • wakizidi yatatoka mengi

mods mnaweza kuondoa kama mnaona haina tija, ila sitatoa source...

Mkuu Acid, Big up !!! uko sahihi sana kuhusiana na hilo hauhitaji kuweka source kwa kuwa ndivyo ilivyo. Kwa kweli yaliyotokea Maswa ni yakulaaniwa na wote kwa kuwa sio vyema kwani nnaowapigania wako mbali na hayo matatizo na familia zao. Cha muhimu ni watanzania walielewe hilo na kufanya kampeni bila kumwaga damu. Kwa hilo lilitokea Maswa ni kuwa dicredit Chadema na lazima Chadema wajihadhari hizi dakika za mwisho.
 
kuna kundi limekwenda mwanza leo baada ya kuona mambo yameondoa umaarufu wa ccm badala ya kuujenga, sasa tutaona vurgu zinapungua kuanzia jumanne
 
Mwenzenu pamoja na majiranizangu tumekuwa tukipokea meseji za kumchafua Dr. Slaa au Kuisifia CCM kuwa ichaguliwe. Hii ni tokea siku nyingi sana, mimi, jirani yangu, au hata moja ya family members lakini paia watu wengine wamekuwa wakipokea meseji hizi zenye pande mbili tu. (Yaani CCM nzuri au Chadema/Dr. Slaa kuchafuliwa)
Japo ni suala la kampeni, lakini mbona si chama kingine chochote kikitajwa, na zaidi ni pale inapoonesha kuwa, eti Chadema ni wachochezi, wanamwaga damu na mambo kama haya.

lakini mimi ninachokerwa zaidi ni pale tu, ambapo katika vurugu nyingi za Chadema, unakuta CCM ndio wanaoanzisha VAGI hilo kwa kupita sehemu ya mkutano wa Chadema au sehemu wanapolala,

Juzi Dr. alisema kabisa kuwa CCM na vijijeshi vyake ndo wanaleta fujo, lakini mbona hata polisi, na baadhi ya viongozi wanataka kuikandamiza chadema makusudi?
Jana/juzi naona Magu ati chadema kisitishe kampain kisa ile vurugu, kwanini siyo CCM pia?

Niende katika maada yangu kuwa, hawa TCRa wasitufanye mabwege, naona kama wanadhalilisha taaluma zao, maana kama wangekuwa Chadema tayari wangeshakamtwa, kwa hizi meseji za uwongo na uchochezi,
Sasa je na chadema pia waanze kuzisambaza meseji za aina hiyo, si watu watakamatwa haraka sana!

JAMANI TUWE MAKINI KURA ZETU NI SIRI WALA MWAKA HUU TUSIDANGANYIKE
KILA MTU AWE CHANZO CHA MABADILIKO
 
Kwa njia halali kabisa ni wazi ccm haiwezi kushinda, labda kwa njia haramu; what a coincidence with Makamba? akiwa Tarime na Musoma watu wamekatwa mapanga, akiwa kilimanjaro vurugu kubwa imetokea iliyopelekea mkutano wa kampeni wa Chadema jimboni Hai kuvunjika, alipopita Arusha mjini yale yale, kaenda Busanda raia wamekatwa mapanga, sasa ndani ya Maswa mtu kauwawa, hii dhambi Makamba anatakiwa atueleze kulikoni?
 
Hawa jamaa wa CCM wanazani wao ndio wana ati miliki ya kutawala taifa ili!!wewe miaka 50 ya utawala kila kitu kiko hovyo wanatupita ata Rwanda!!!
CCM akina wazo jipya kwaiyo bora wakapumzike tu kama wastafu wengine.
 
Kwa njia halali kabisa ni wazi ccm haiwezi kushinda, labda kwa njia haramu; what a coincidence with Makamba? akiwa Tarime na Musoma watu wamekatwa mapanga, akiwa kilimanjaro vurugu kubwa imetokea iliyopelekea mkutano wa kampeni wa Chadema jimboni Hai kuvunjika, alipopita Arusha mjini yale yale, kaenda Busanda raia wamekatwa mapanga, sasa ndani ya Maswa mtu kauwawa, hii dhambi Makamba anatakiwa atueleze kulikoni?

Ila sasa inakera pale ninapoona eti watu wanasema kuwa Chadema ndo wameshakamilisha azma ya kumwaga damu!! wakati ni mbinu za ccm.
Ila wanatenda dhambi sana kwa sababu dereva kasakiziwa aendeshe gari hadi chadema walipo na hilo likamkuta ili tu wao wapate kupaka matope chadema.
Cheki Tanga juzi wamesakizia mwingine tena alete fujo bahati mbaya rais mwenyewe alikuwepo akakemea watu wasi react.
Iringa vile vile watu wanatolewa na ccm wajitoe mhanga,
Ni kweli mkuu CCM kihalali hawawezi kushinda kamwe, labda waibe sana
 
Mjukuu
CCm hawana hati miliki, maana kama ni wanachama wa ukweli wameshaondoka, yaliyobaki ni majizi tu yanayoendelea kujificha ilimradi tu wajilimbikizie mali
Huku wakisahau kuwa kufa ni lazima, maana kuna watanzania wanapata taabu wao wapo kama vile paradise ni kubaya zaidi ya hapo walipo.
sasa wamefikia ukingoni bado kidogo wanaondoka, siku zinahesabika
 
Back
Top Bottom