Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,904
- 7,746
Mkuu CV ya mtu sio kurahisishia wananchi bali kuwahadaa zaidi kwa sababu sasa hivi kila mtu anataka phd ili kuwarusha wananchi. Tunamtaka kiongozi bora ambaye anaweza kuwawakilisha wananchi na sio hawa wanaojifanya kujua sana kuliko kila mtu kwa sababu kaishi Marekani na ana Phd. Tumewaona wengi sana wengine marafiki zetu wakisema hawawezi kuishi maisha ya Kimaskini na majigambo kibao.
Ni lazima apimwe kwanza kwa ujasiri na uzalendo wake kwa wananchi bila kujali elimu yake hatumtafuti waziri hapa wala mkurugenzi. Hii habari ya kuendelea kuchafuana mkiendelea nayo itawakwaza zaidi na nitaendelea kuwaasa. habari ya Zitto iacheni haiwajengi bali inazidi kuwabomoa mitaani amini maneno yangu, maana hata mimi nimeshakosa imani na mawazo ya watu wengi sana humu, Huyo Msacky na MM inahusu nini kuyaweka humu ili MM naye awekwe kundi moja?.
Zitto kisha fukuzwa kama hakuna mazungumzo inatosha kuyakana kuliko kuendelea kutubebesha fikra za kumchukia mtu kwa mambo yalokwisha hukumiwa. Zitto yupo kifunguni, habari mjini bado zinaendelea - mnamtakia kifo kabisa? mnachosha jamani hata kama watu hawampendi basi mwacheni afanye kazi alotumwa na walomkubali.
Mkandara, kwa sisi wazoefu hapa jukwaani tunaelewa ni jinsi gani usivyopendezwa na treatment anayopewa Zitto na wana jukwaa. Ni bahati mbaya kwake lakin hiyo ndio hali halisi. Wana chadema, at least wa hapa mitandaoni ndivyo wanavyomchulia Zitto. Mimi mmoja wao. Simpendi! Na siku chadema waki reconcile na huyu mhuni mimi na siasa itakuwa basi. Naamini wengi wanafanana kimisimamo na mimi as far as Zitto is concerned. Lakini haina maana tunapinga uwezo na akili binafsi alizo nazo. Ila kwa maono na mahitaji ya chama na wanachama, zitto hatumtaki.
Kuhusu CV, mimi nadhani sio ya kupuuza. Kujua wasifu wa mtu ni njia mojawapo ya kuelewa ufanye nini wakati wa uchaguzi. Zitto aliingizwa bungeni akiwa hana uzoefu hata wa kuwa katibu kata. Elimu yake, ushirika wake na Fredrick Nouman Stifftung na harakati zake zilijenga imani kwa wapigakura wake. Lakini watu hawakupiga ramli kujua elimu yake na uzoefu wake kiduchu aliokuwa nao. Alii-publish cv yake. Wapambe wake wa kipindi kile walimsaidia kuipublish CV yake. Wewe hukuja hapa kupinga. Ila leo CV ya yareda imekukurupusha umekuja kupinga!
Last edited by a moderator: