CHADEMA na Zitto watafuta suluhu

CHADEMA na Zitto watafuta suluhu

habar zenu wana jamvi... Ni mda mrefu sana mwana siasa machachali zitto kabwe zuberi amekuwa na mgogoro na chama chake cha chadema ambacho kilifikia na kumvua nyadhifa zake zote ndani ya chama. Pamoja na hayo mambo mengi alihusishwa nayo kama vile usaliti, na huku akishukiwa kuwa ni kibaraka mkubwa wa ccm. Yote yalipita na hatimaye kauli ya mwisho ya zitto ikawa kwamba "mimi ntakuwa mtu wa mwisho kutoka chadema..." lakin jana nimeweza kushitushwa pale zitto kabwe alipo uelezea umma kuwa alikaribishwa kwenye mkutano wa (ukawa). Kijana huyu kaweza kukalibishwa na walio mwita msaliti? Hakika chadema wamegundua kitu kwa kijana huyu.... Chadema wamefyata mkia kwa zitto kabwe tusipepese macho kwa kuongea uongo. Huo ndio ukweli na hakika ukweli unauma. Tafakari. Nawasilisha.

Acha kuongea pumba. Swala linalojadiliwa ni la kitaifa kwa manufaa ya Wananchi wote wa Tanzania. Sasa mambo ya vyama yanaingiaje hapo? Maana wote vyama vya upinzani na CCM wamejadili swala hilo kwa pamoja kwa sbb ni la kitaifa. It means na CCM nawo wameufyata? Shame on you
 
Huyu jamaa analeta ushabiki ambao hauna maana.. Kama alimsikiza Zitto jana alikiri kwa mara ya kwanza kukubaliwa kuingia kwenye kikao cha ukawa.. Huku akisema ni watu aliokua wamic na anawashukuru sana.. Haya yako yanatoka wap..!

kama wameweza kukaa meza moja kama ukawa wakaongea watashindwaje kuongea nae ili waongee kama chadema?? Kwann ishindikane?? Chadema imefyata mkia kwa uwezo wa zitto kabwe.
 
imeripotiwa katika magazeti ya leo kwamba chadema imemwangukia mbunge wa kigoma kaskazini zitto kabwe na kutaka kusuluhishana na kumaliza tofauti zao na hatimaye kurudi kukijenga chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa dola 2015.

Nini tafsiri na mantiki ya hatua hiyo muhimu ya chadema baada ya kukamisha uchaguzi wa ndani ya chama bila Zitto kisha kumwangukia?? Je, ni dhamira ya dhati au ni kumhadaa na kumkejeli kumpima kama yuko imara??
DSC03488.jpg

hahahaaaaaaaaa wambie maana watu ni wagumu kuelewa sana. Asante sana kwa mwono wako. Mungu akubaliki
 
mimi nitumie fursa ihi kumwomba,mbowe na zito wakae chini waondoe tofauti zao,umoja ni nguvu,na kauli 1 ni bora 2015
 
Hakuna uongozi au kiongozi wa chadema amemtaka Zitto arudi au kumaliza tofauti zao. Acheni propaganda. Cha msingi Zitto bado ana act kichadema na magwanda ya chadema bado anavaa na hakuna aliyemnyima asivae. Cha msingi kama anataka kurudi mwenyewe afuate taratibu na apinwe upya lengo la kurudi.
 
kama wameweza kukaa meza moja kama ukawa wakaongea watashindwaje kuongea nae ili waongee kama chadema?? Kwann ishindikane?? Chadema imefyata mkia kwa uwezo wa zitto kabwe.

Hakuna hoja hapa mkuu. Hizi porojo zisizo na tija kwa taifa. Ulitaka aachiwe Zitto na kafulila hili swala kwa sababu zito na chadema wanamgogoro.. Watu makini huweka maslahi ya taifa kwanza mengine baada..
 
Zitto anajiuzulu tarehe 05.12.2014 na anahamia ACT take it from me.
 
Siamini. Zitto huyuhuyu aliyeshirikiana na Bukoba boy katika kupanga njama za kumteka Kibanda ili tu ionekane CDM ni chama cha magaidi? Aliyerekodiwa akiongea na Jack Zoka usiku wa manane na mazungumzo yao yakiwa ya kuihujumu CDM? CDM wala wasilifikirie hilo.
 
imeripotiwa katika magazeti ya leo kwamba chadema imemwangukia mbunge wa kigoma kaskazini zitto kabwe na kutaka kusuluhishana na kumaliza tofauti zao na hatimaye kurudi kukijenga chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa dola 2015.

Nini tafsiri na mantiki ya hatua hiyo muhimu ya chadema baada ya kukamisha uchaguzi wa ndani ya chama bila Zitto kisha kumwangukia?? Je, ni dhamira ya dhati au ni kumhadaa na kumkejeli kumpima kama yuko imara??
DSC03488.jpg

Wanambembeleza ili akagombee urais chadema kwa sasa hawana president candidate material anayeweza kuwa na sifa zinazomzidi Zitto.
 
Back
Top Bottom