CHADEMA na unafiki uliotukuka

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,856
7,003
Kupitia hili suala la Mbunge wa Nkasi pamoja na wabunge wa viti maalumu, CHADEMA wamejitanabaisha ni kiasi gani wamekua wanafiki kwa watanzania na wapenda Haki na amani wote.

Uchaguzi wa mwaka 2015 CHADEMA walikiri wazi kuwa ni uchaguzi ambao haukua huru na Haki hadi kupelekea kususia hotuba ya Rais Bungeni lakini ajabu walikubali kuapa na majina ya viti maalumu yakapelekwa bila hata kuchelewa.

Ajabu na unafiki ni mwaka huu, hoja ileile ya uchaguzi kutokua huru na Haki lakini ajabu ni kwamba kwa sababu viongozi wakuu wamekosa basi safari hii hawataki hata yule aliyepata au nafasi za viti maalumu walivyopata kuzitumia, wanataka wakose wote, wakati uchaguzi uliopita viongozi walipata na wagombea wengine wa CHADEMA walidhurumiwa ushindi wao, hakuna aliyewajali zaidi ya kuacha machozi yao yaende na maji.

CHADEMA waache kuwa wanafiki.
 
....Uchaguzi wa mwaka 2015 CHADEMA walikili wazi kuwa ni uchaguzi ambao haukua huru na Haki hadi kupelekea kususia hotuba ya rais bungeni lakini ajabu walikubali kuapa na majina ya viti maalumu yakapelekwa bila hata kuchelewa.
Kwa hiyo Kama mwizi alikamatwa mwaka juzi akapigwa mawe, miaka yote wakamataji watumie adhabu ile ile?!

Mwaka huu adhabu kwa mwizi yule yule ni tofauti. Tulia tulii
 
Wewe nini kinakuuma yeye akiongelea hiyo issue? ni lini wana JF tumeanza kupangiana vitu vyakuandika? Kwahiyo mtu akiongelea issue za team ya Barcelona naye ataambiwa nini kinakuuma kuongelea mabaya ya Barcelona? kama ni hivyo basi JF itabidi wote tuwe Mabubu!
Umeelewa kweli alichoandika? Ni wapi amempangia cha kuandika?
 
Hivyo na yule aliyesema Maendeleo hayana vyama, halafu baadae akasema nichagulie “fulani” kuwa mbunge ili niwaletee maendeleo nae ni mnafiki?
Pangu pakavu tia mchuzi kwenye siasa ni jambo la lazima. Lakini tunapinga tabia ya nguruwe kulia wakati anakula miwa wakati anafurahia hiyo miwa. Kwanini asicheke tu?
 
Wewe nini kinakuuma yeye akiongelea hiyo issue? ni lini wana JF tumeanza kupangiana vitu vyakuandika? Kwahiyo mtu akiongelea issue za team ya Barcelona naye ataambiwa nini kinakuuma kuongelea mabaya ya Barcelona? kama ni hivyo basi JF itabidi wote tuwe Mabubu!

hahaha kuna watu unawatafuta ubaya
 
Kupitia hili suala la Mbunge wa Nkasi pamoja na wabunge wa viti maalumu, CHADEMA wamejitanabaisha ni kiasi gani wamekua wanafiki kwa watanzania na wapenda Haki na amani wote.
....
CHADEMA waache kuwa wanafiki.
Maoni yangu kuhusu hili ni kwamba; Nafikiri haujafanya utafiti juu ya mlolongo wa matukio kuelekea maamuzi yaliyofanywa na CHADEMA 2015 na 2020.

Naamini ukifanya utafiti utafikia suluhisho tofauti na hili la kua ni wanafiki. Bila utafiti utaishia kufanya generalization (ujumla) ambao mara nyingi hutoa picha tofauti na hali halisi.
 
Vibaraka wa mhutu wa kijani kibichi mnawashwawashwa kweli na CHADEMA , hebu nendeni Bungeni mkawawapelekee wananchi maendeleo , tekelezeni ilani uchwara nyie mapimbi muigeuze nchi kuwa ulaya kama Dar mvua ya siku moja tu , hata pa kupita hamna .
 
Back
Top Bottom