Chadema na SIRI nzito juu ya Usala ma wa nchi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema na SIRI nzito juu ya Usala ma wa nchi yetu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by engmtolera, Mar 24, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  haya wanachadema mnataka kutupeleka wapi sasa kwani Mbunge wa wawi Mh Hamad Rashid amesema kuwa nanukuu “Napenda kuthibitisha kauli yangu kuwa wenzetu CHADEMA wana siri nzito na usalama wa Taifa hili na si vinginevyo. Ni vyema Watanzania sasa kutumia akili za kuwakwepa CHADEMA ambao wanataka kuleta agenda yao ya siri isiyo na lengo la kulinda amani ya Taifa.”

  sasa wana chadema umefika wakati wa kutueleza wanajamii tukatambuwa mna agenda gani ya siri juu ya usalama wa nchi yetu?

  Tambueni kuwa hii nchi inahitaji kulinda AMANI iliyonayo sasa ni vyema tukatambuwa kama hayo aliyo yasema Mh mbunge yana ukweli ndani yake,ili kila mmoja wetu aweze kuanza kujiandaa na hiyo agenda yenu juu ya amani ya nchi hii.
  [​IMG]
   
 2. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa wawi Mh Hamad Rashid nina katika nchii?
  Nini mchango wake katika nchiii ??
  Je anafanya kazi gani sasa.????
   
 3. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Huyu Rashid anatofauti gani na maneno wanayotoa ccm, kila siku tumeona matamko kama chama chenye udin, ukabila, uhaini na sasa wanakuja na siri nzito ya usalama wa taifa. Sasa simngemuuliza atoe siri gani hiyo? Tumeona nchi nyingi vyama tawala ndo chanzo cha vurugu, ona ivory coast, nchi za kiarabu n.k. Hivyo hizi ni propaganda za kisiasa. Tuwaombe ccm waachie madaraka kwa hiari yao wakati ukifika. Peoples power.
   
 4. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,974
  Likes Received: 20,336
  Trophy Points: 280
  usijadili amani kwa kuwa tu unaona watu hawawezi kuhoji, amani bila HAKI ni kujidanganya, cdm endelea kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao ndani ya nchi hii adhimu
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jamaa mbona ana hasira sana tangu aliponyang'anywa tonge?
   
 6. n

  nndondo JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hivi Hamad Rashid ameanza lini tena kuwa kiongozi wa maana, tangu tujua kuwa anasumbuliwa na ruzuku ya uongozi wa upinzani tumemuacha kama alivyo, hana moral authority ya kuongea na watanzania wa leo, afurahie ndoa yake na CCM na kutafutiwa nafasi katika serikali ya umoja ambayo tayari imeshazua utata wa kutosha pasipo kuongeza mziki mzito wa CHADEMA, wameshindwa wameshajulikana ni CCM B waendelee tu kufurahia hilo wakati seif wao akiwa na cheo chenye jukumu la kushughulika na ukimwi, madawa ya kulevya sijui na nini, can you imagine? how low kisa ni kupanda benz? CCM OYEEEEEEEEEE, tunangoja mapinduzi ya kweli eti huyo mcheza disco, hivi yeye na prof lipumba nani amefanya vitu vikubwa, mwambieni prof si amesoma? hebu atuambie yeye na lula de salva wa brazll nani kasoma zaidi na nani kafanya makubwa? kati ya yeye na master sugu nani kafanya makubwa? heri ya kumsikia Mr II akipigania studio iliyotolewa kuliko hotuba za prof zilizojaa upupu mtupu,
   
 7. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwenye siri nzito yeye Rashid na wana CUF wenzake kutoka Zanzibar wanao wahadaha wa kina Lipumba kuwa wako wote huku wakihujumu muungano wa Tanzania kwa kuimarisha utaifa wa wazanzibari
   
 8. D

  Derimto JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ngoja nikweleze wewe mvivu wa kufikiri hivi hapa unayozongumza ni amani ya aina gani maana wewe na huyo Hamadi wako wala hamwelewi dhana nzima ya amani na usalama wa wananchi.

  Hivi kuwa na nchi unayoishi kama mtumwa huku ukiwa na njaa na unapata mlo mmoja na wengine wanakula na kusaza wakisomesha watoto wao ulaya na wenyewe kutibiwa huko hata wakiugua mafua tena kwa fedha ya bajeti ya afya na elimu iliyopitishwa na bunge kuhudumia watoto wetu na fedha hizo hizo zinaliwa kwa fujo wagonjwa wakilala mzungu wa nne na wengine kulala chini na watoto wetu kusomea chini ya miti na wakiwa madarasani wanafundishwa na mwl.mmoja ambaye hana pa kukaa amepangisha huku anafundisha madara zaidi ya matano!

  Hakuna amani ila kwa ncha ya upanga! Sijajua unamzungumzia amani gani wakati tunaishi kama watumwa huku tukidai tuna uhuru ambao ni wa bendera wala hautusaidii naona ni afadhali tungechelewa kupata uhuru kama Africa ya kusini angalau tuambulie miundo mbinu ya miji na maendeleo ya lazima kama wao wamejengewa na wazungu kila kitu kuanzia barabara mpaka mashule na hospitali ambazo wanawatibu watu wote!

  Kuna haja ya nchi hii watu kujitoa kwa hali na mali kwa kuipigania ili irudishe hadhi ya nchi na hata iukibidi zaidi ya rwanda ambapo leo wanaheshimiana na kujenga nchi yao kwa nidhamu na umakini wa hali ya juu, maana hakuna faida na sihitaji amani ambayo itanifanya watoto wangu na vizazi vijavyo vije kutemea mate na kukojolea makaburi yetu na matusi kibao kwa kushindwa kuitawala na kuindesha nchi vizuri badala ya kutuwekea maua na kutumbuka kwa mazuri tuliyowafanyia tulipokuwa hai.

  Kwa kifupi ni kwamba wewe na huyo Hamadi wako na mafisadi na wavivu wenzako wa kufikiri hamjui maana ya amani halisi na tena muwe na adabu msitutishe na mafuvu ya vichwa vya wanyarwanda niko tayari hata zaidi ya hapo na CHADEMA ndiyo angalau kimeonyesha njia ya kuifikia demokrasia ya kweli kwa njia sahihi bila kumwaga damu bali kutumia nguvu ya uma maana wangeweza kuchufua hali kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita lakini walitumia busara zao ambazo zimewafanya waonekane wajinga na bado ccm hawataki hata kushituka na kusoma alama za nyakati na kujipanga upya wamelewa na madaraka wanaendeleza ubabe na kuacha kila kitu kinapanda bei bila utaratibu!

  Nadhani uliyeanzisha hii mada umenichefua roho kabisa na kuharibu siku yangu ya leo HAPA SI IHITAJI HIYO HADITHI YAKO YA AMANI NINACHOHITAJI HAPA NI TANGAZO LA MAANDAMANO NA HATA KUBEBA SILAHA YOYOTE YA KUPAMBANA VIBARAKA WAO KAMA POLISI WALIOJICHUKULIA RUSHWA NA HATA KUIBA KWA KUTUMIA SILAHA ZETU WENYEWE NA KUJAZA MADALADALA BARABARANI HUKU WAKIWA NA MSHAHARA WA 120000.
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Haya mafuvu mliyatumia uchaguzi wa 1995 kutisha watanzania.
  Kuyaleta tena hapa ni kuifanya CCM na washirika wake wachukiwe zaidi maana kama tungekausha mafuvu ya watanzania wenzetu wanaokufa kila siku kwa madhira yatokanayo na uongozi mbovu basi maghala yangejaa.

  BTW, kwa nini mnatumia Rwanda kama mfano wa machafuko wakati leo hii Rwanda wana amani na maendeleo kuliko amani tunahubiri hapa kwetu. Na endapo mauaji ya haraiki ilibidi yatokee ili Rwanda ipige hatua ya kijamii na kimaendeleo kama ilivyo sasa basi tunachagua njia hiyo kwani hata tusipoichagua we are dying anyway chini ya mkono wa CCM na kina Hamad.
   
 10. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Weye acha uchochezi!!! kwa nini uwaulize chadema badala ya mtoa shutuma?
  Weye nenda kamuulize HAMADA aeleze hiyo Siri nzito ni ipi!!!!!
  Usilete ushabiki wa majungu humu!!!!!!!!!
   
 11. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Asilaumiwe mtoa mada, bali ameweka hadharani tudadavue nini viongozi wetu walivyo na mitazamo tofauti juu ya muendelezo wa siasa za Tanganyika. Mtoa mada pia ametoa angalizo lake la kueleweshwa vema na tusimu-attack as if ame-conclude kwa thread yake hii, tuchangie kwa vina ili tujue kisemwacho kipo ama ni uzushi, bali hoja za msingi zitawale nasi tuelewe, Kwani hajazungumzia kama yeye ni mwanachama wa chama gani. Cha msingi kwake ni kutuletea chanzo (source) ili ituwie rahisi sote wadau wa siasa hapa JF.
  Ni maoni yangu kwa nilivyomuelewa
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Si umuulize huyo babako alosema wana ajenda ya siri akueleze ni ajenda gani badala ya kuwauliza chadema?
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HAMAD RASHID NA CCM MJUE USALAMA WA NCHI UNAYUMBISHWA NA 'MUAFAKA WA MASLAHI BINAFSI' YA VYEO NA KUJIUNGA KULE NA NGURUWE KULA
  MABUA NA UFISADI ULIOKITHIRI NCHINI


  Jamani kuna uwezekano Wa-Tanzania tukawa na tofauti nyingi tu nchini zikiwemo zile za kitamaduni, kiimani, kijinsia na kadhalika lakini matatizo yanayotuhatarishia amani nchini, Wakristo kwa Waislmu na kote Bara na Visiwani ni zile zile!!

  Nasema matatizo ya kusisitizwa tu AMANI na kufichwa kule kwa HAKI kwa raia ni chanzo cha matatizo kibao yanayotukaba kila siku nchini kama vile: (1) UFISADI uliokithiri ndani ya serikali ya CCM yatuathiri sote, (2) Muafaka wa CUF kujiunga na CCM kula mabua kwa pamoja na kuwaacha wananchi solemba kwenye umasikini wa kutupwa ni letu sote, (3) Utaratibu wa Serikali ya Muungano usiona tija, na fursa sawa wa moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida, (4) ukosefu wa ajira, (5) elimu duni, (6) Maisha kupanda gharama kila kukicha ni letu sote hivyo kwa hali ya kawaida kabisa Mtanzania hahitaji KAMPENI ZA KUTIANA HOFU pale tunapojiunga kama taifa kujikomboa kwa kudai haki zaidi na Katiba Mpya nchini!!!

  ... hatuwe kujua vizuri; wenzetu wa CCM na CUF waulizwe vizuri juu ya hilo jambo wanaloliona peke yao tu hapa nchini kuhusu usalama kutetereshwa ambalo sisi wengine hatulion.

  Lakini kama kudai HAKI SAWA NA MASLAHI KWA UMMA wa Tanzania ndicho hasa kile kinachowakosesha amani wale MAFISADI walioko serikalini na kuitwa KUHATARISHA USALAMA WA NCHI na basi CHADEMA kazeni mwendo mdundo kwa sana tu.

  Wa-Tanzania tunaakili sana kote Bara na Visiwani na pia tunafahamu fika kwamba wale wanaoingia muafakaka na serikali ya CCM gizani kwa maslahi binafsi ya kupata vyeo, mijumba, na mashamba ndio hasa wanaoHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU.

  Ndugu zetu akina Hamad Rashid, CUF-Maslahi na CCM-Ufisadi, acheni mara moja kuchezea akili za Mtanzania wa leo kote Bara na Visiwani tunasema kwamba Hatudanganyiki wala Hatugawanyiki kwenye Kutafuta Maslahi yetu kama Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 14. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa nini usimuulize huyo Hamad Rashidi, si kasema anaoushahidi, inakuwaje unawauliza CDM.
   
 15. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,079
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  safari kazi ipo. hapa kwenye usalama wa taifa ndipo walipokuwa wanapatafuta sana wanaccm. walivyo wajinga wamemtuma kibaraka wao aliongelee hilo kwa kujua kwamba watz hawatashtukii mchezo. udini,ukabila,uhaini na sasa ni usalama wa taifa. kwisha habari yao ccm.
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyo hamad rashid kwanza siyo mtanganyika yeye ni mzanzibar ataongeleaje mambo ya nchi isiyomhusu?
   
 17. C

  Chamkoroma Senior Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mada hii inanifanya kushindwa kukaa kimya hapa nilipo, nakunifanya kusema kidogo, This man, Rashid na mtoa mada wana agenda ya siri na sivinginevyo, hivi kugugumia ubaya unaofanywa na watu wachache kwa hasara ya watu wengu na kwa faida ya wachache, CDM kuongea nikuleta machafuko nchini? nakumbuka 1995 au 2000 ccm walisema cuf wameleta mapanga nawanafundisha vijana wao kuleta vurugu siku yakupiga kura, je nikweli cuf walifanya hivyo? nikasikia kuwa misikitini kulikuwa kunaandaliwa mjahidina kwa ajili ya kuhujumu kura ni kweli miaka hiyo cuf waliwashawishi waumini wa dini yao kufanya hivyo? naamini ilikuwa uvumi tu wakuonyesha kuwa cuf walikuwa na SIRI NZITO NA AMANI YA NCHI HII, kitenda cha huyu jamaa kusema hadharani uongo usio nautafiti unaonyesha wazi kuwa sasa cuf bara imepoteza wanachama wengi hasa wawakati ule wa miaka ya 1995/2000, hata mtoa mada nifisadi mkubwa wa ccm ili tu aonyeshe kuwa CDM PP inamipango yakuyumbisha amani ya nchi kumbe wanamipango yakuficha ufissadi unaofanywa nawafadhili wakuu wa ccm wanaokwepa kulipa kodi kwafaida ya mafisadi wenyewe.
   
 18. m

  matambo JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada sijafurahishwa na hayo mafuvu uliyoyaweka hapo, sidhani kama ni sahihi kwani yanaweza kuwa misleading
   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hamad naona bado hajakubali kuwa Mbowe ndiye Kiongozi wa Upinzani nchini. Bado hilo linamsumbua sana na hakulitrajia. Thats all.
   
 20. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka kauli ya mwanaharakati mmoja wa Ufaransa.
  "PEACE SHOULD MEAN MORE THAN THE ABSENCE OF WAR"
   
Loading...