Joss
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 765
- 191
Kwa hali ya kisiasa inavyoenda sasa ni wazi kuwa CDM wanazidi kupata umaarufu bara na wanatishia ustawi wa vyama vya CCM na CUF(achilia mbali NCCR,TLP ...). Kutokana na kuwa nguvu iliyonayo CDM ni kubwa mno na inaonesha kuwa wameshindwa kudhibitiwa huku bara, CUF wanaona kuna hatari kubwa ya CDM kuvuka bahari na kuwa na nguvu huko pia, hivyo wanacho kifanya sasa ni kuwajaza maneno ya chuki Wazanzibari kuwa CDM inawachukia, na kuwa kutokana na idadi kubwa ya Wazanzibari kuwa waislam sitoshangaa kama CUF wataanza kusema CDM kina udini. Hii yote ni kulinda maslahi ya CUF visiwanai maana huku bara wameona hawana cha kwao.
Kutokana na kuwepo kwa umoja wa CCM na CUF katika serikali ya Znz kumefanya kutokuwepo demokrasia ya kweli,hakuna mpinzani atakaye ishinikiza serikali kutimiza wajibu wake. Naamini kuwa wapo wengi tu ambao hawakubaliani na vyama hivi viwili. Hivyo basi CDM yaweza kujipanga vizuri ikafanya utafiti na kujua jinsi gani ya kujiimarisha Zanz.