CHADEMA na mikakati ya kujiimarisha kanda ya Pwani na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA na mikakati ya kujiimarisha kanda ya Pwani na Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALI KIBERENGO, Dec 5, 2010.

 1. A

  ALI KIBERENGO Member

  #1
  Dec 5, 2010
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa Mujibu Wa Sheria ya Vyama Vingi, vyama vyote vya siasa vilivyopata Usajili wa Kudumu ni lazima viwe ni vya Kitaifa, sasa CHADEMA Zanzibar hamuitaki?

  Mbona hamuimarishi Chama maeneo haya?
   
 2. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  muungano bomu ukirekebishwe utaona vitu cdm huko visiwani...
   
 3. M

  M TZ 1 Member

  #3
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  CHADEMA,Wamesha sema chama kinaweka maslahi ya taifa kwana,ndiyo maana kwa upande wa zanzibar,wanawaunga mkono cuf ngazi ya urais na kwenye ubunge wanawaunga pia sehemu ambazo cuf wananguvu,na wamefanya hivyo kwa vitendo,walisimamisha wagombea wa ubunge zanzibar lAKINI HAWAKUTILIA MKAZO,WHAT ELSE NDUGU
   
 4. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar kura zake ni chache sana, so hakuna haja ya kupoteza muda huko.
   
 5. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #5
  Dec 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkubwa, kwa elewa kwamba kwa mujibu wa kanuni za usajili wa vyama vya siasa hakuna chama kinachosahiliwa bila kudhibitisha kuwa na wanachama mikoa yote pamoja na ile ya znz. Hivyo weka akilin mwako kwamba TZ hakuna chama chenye usajili wa kudumu kisichokuwa na wanachama znz, ndo ulete hoja ya msingi kwa great thinkers.

  Pia mgombea mwenza wa chadema amekuwa kiongoz wa chadema upande wa znz kwa miaka zaid ya 10 sasa,unadhani alikuwa anaongoza mawe tu huko! Vyama vya upinzan bado vinakinakua huwez kulinganisha na ccm amboa wapo miaka mingi madarakani na wana vitega uchumi vingi ndo maana hakuna chama cha upinzani chenye matawi kila wilaya nchini kama ccm.

  Ndo maana chadema hawana ktk baadhi ya maeneo ya znz na bar vile vile, pia cuf na vingine hawana matawi sehemu kibao tz?kwa nini kuulizia chadema tu? ina maana mpinzani ni chadema tu?

  Naamini wanajipanga zaid mda si mrefu utaona bendera nyingi tu huko znz na mikoa mikoa mingine ya bara. mingine ya bara a.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  ALI KIBERENGO,


  CCM ,wajanja sana, wao waliunganisha TANU na ASP na hivyo wakawa wamepata "dezo". Hawakuhitaji kutafuta wanachama au kujenga mtandao. Halafu wakapitisha sheria hiyo uliyoisema. wanajua kuwa ni kazi nzito kwa chama kipya kujijenga, kikaimarika katika sehemu mbili za Jamhuri ya Muungano.


  Ujanja mwengine ambao CCM wameutumia ni kutokuweka sheria ya kuruhusu vyama vinapoamua kuungana viweze kuungana.


  Pia, wanahakikisha kila chama ambacho kinaonekana ni tishio kwa CCM basi wanatumia jembe na nyundo (panga!!??) yao kukishughulikia.


  Kwa kifupi ni kuwa CHADEMA, CUF, NCCR, TLP, TADEA, UDP vimezidiwa "usungura" na CCM.


  Kama hilo halitoshi basi wameweka sheria kuwa , hata ikitokea miujiza na Mpinzani akashinda, ni Tume ya uchafuzi yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi na ikishamtangaza mshindi, watu waondoke, wanune, watukane, walaani, waseme mpaka vipovu vya mdomoni viwatoke, wasikitike au walie, ndiyo huwa imetoka hiyo. Mkutano kwenye ukumbi wa kutangazia matokeo baada ya miaka mitano mengine.


  Kwa matokeo ambayo yanaweza kupingwa mahakamani, kesi zitapigwa date, hukumu itatolewa ikiwa imebakia miezi 3 kabla ya uchaguzi mkuu mwengine.


  Hapo, hujazungumzia migogoro ndani ya vyama vya upinzani ,wala hujazungumzia wapinzani wanavyohujumiana na kurushiana madongo.


  Kwa hili, CCM ni kiboko yao, Tuwape sifa yao. CCM wanacheza karata zao kwa kuficha, wapinzani, domo jingi kwenye viriri na vyombo vya habari.


  Haya Changamoto hiyo, wapinzani! Tukutane baada ya miaka mitano ijayo. In the mean time, kaeni kwa tahadhari, marungu na nyundo nje nje!

  Hebu na ninyi jaribuni kucheza Chess! Tumieni "Bongo" zaidi ya "Domo".


  Ukifuatilia siasa za Tanzania, utacheka mpaka mbavu zikatike/ zichanike.

  Ukizichukulia serious sana unaweza kupata heart attack! au vidonda vya tumbo!


  Tufanyeje? Tufanye nini, wadau?
   
 7. D

  DENYO JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haina tija -kwa sasa tunataka katiba mpya na tume huru ndio mzizi wa fitina uliopo, majaji wamesema -bomani, manento, kisanga sijui masultani wanasubiri nini.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  No room for perceived christianity in zenj. It is a historical accident that ccm is there
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Raia Fulani,

  That is a dream, fantacy to say it was a historical accident. Trace the sequence of events!

  Moreover, for Christianity to reach you, to find you, you may well thank Zenj and their rulers back then. Zanzibar was the launching pad for Missionaries to spread Christianity into continental Africa, of course they did not want to upset their hosts by trying to Christianize the locals there.

  However, the real reason, as you may not be aware it seems, was to help their governments, companies easily plunder our resources!
  That is why coastal areal is more Islamic than upland. Interior is more Christianized than coastal areas.


  "Have you heard of the story? That they asked us to close our eyes to pray and when we opened them our land was gone!"

  Islam reached the coast first, thenfollowed by Christianity. Open your history books!

  Our dear Mwalimu was received by Muslims and given the opportunity to rise to the highest rank of the leadership in Tanganyika and Tanzania, is the testimony that Muslims did not have the mentality you portray now.

  So what when wrong?

  You may listen to the bidding farewell speech Mwalimu gave to the wazee of Dar es salaam alipong'atuka to satisfy yourself, if you think I lie to you.

  Hatred will destroy you, preach love and follow what you preach with actions!

  Do some observation! You will notice in almost every political party in Tanzania there are Christians, muslims, traditionalists, pagans you name it.

  If we had religion specification in national census, you might have been surprised to know how many Christians live in Zanzibar now.

  If it is a propaganda machine,then

  Good luck, Raia Fulani.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  jkNI KWELI MWAFAKA VISIWANI ULIKUA NI WA VIONGOZI CUF NA CCM KUGAWANA MADARAKA; CHADEMA WAPELEKEE WANANCHI 'MABADILIKO SHIRIKISHI' ZANZIBAR

  Madai ya ndugu Ali Kiberengo ni ya kweli na yenye umuhimu kabisa. CHADEMA, jitahidini kuwafikia wapenzi wa chama hiki walioko Tanzania Visiwani. Wapo wengi ambao wamekerwa sana tena sana na hii NDOA YA MKEKA kati ya CCM na CUF, hivyo wameachwa yatima bila kupata pa kusemewa.

  Tukumbuke, maridhiano Zanzibar ni kati ya viongozi wa juu CCM na wenzao wa juu CUF ndio maana kunaonekana maridhiano ya KIVYEO katika serikali ya Visiwani. Lakini wananchi wa kawaida wao hawamo kwenye picha ya maridhiano hayo hivyo wanaendelea kuteseka na kuonewa kama sisi huku.

  Hivyo CHADEMA hawana budi kukumbuka kufikisha SALAAM ZA KHERI NA MABADILIKO YA KWELI, na wala si viongozi wachache kujineemesha kwa kugawana vyeo VISIWANI kwa jina la MWAFAKA, badala yake CHADEMA kiwashirikishe zaidi Watanzania wenzetu wale wa hali ya chini huko kwenye kuandika KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru za Uchaguzi Bara na visiwani.
   
 11. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  thanks, nonda. I know about the historical evolvement in zenj when it comes to political struggle and religion. Christianity in zbar is there for political reasons. And for political reasons, christianity is being oppressed there. In Tanganyika we see cuf as islam oriented. So they see cdm as christian party. Before 1977 zbar had no ccm. It was mwalimu's idea and calculated strategies and karume's political ignorance that ccm is in zbar though ccm haina dini. Ccm ni tanu. Wangekuwepo kina babu madarakani enzi hizo unadhani ccm ingezaliwa? Unadhani ni kwa nini hadi leo wazenj hawaamini katika muungano? Kama ccm iliingia zbar kwa gia ya ujanja, ulaghai na ushawishi na hadi inapingwa (ccm ni muungano) itakuwaje kwa chama ambacho kinadhaniwa ni cha kidini?
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wakuu nimesoma kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu sakata linaloendelea katika kuunda kambi ya upinzanu kwenye bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania


  Chadema wanasema wao hawawezi kuungana na CUF kwenye kambi ya upinzani kwa sababu wao ni sehemu ya serikali ya Zanzibar, kwa sifa hio wamaekosa uhalali wa kuwa wapinzani


  ukiangalia juu ya suala hilo, sidhani kama Chadema wanajua kuwa Tanzania kuna Serikali Mbili na hata tume za uchaguzi ni mbili, moja kwa ajili ya serikali ya Muungano, na ya pili kwa serikali ya zanzibar. na hata mabaraza ya kutunga sheria na katiba zenye kuiongoza jamhuri ni mbili


  sasa serikali ya zanzibar kwa mujibu wa sheria kuna uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, na kutokana na katiba si lazima vyama hivyo viwe ccm na cuf, bali vuama vyovyote vitavyotimiza masharti ya kisheria vitashirikishwa kwenye serikali.


  suali langu jee ingetokea chadema wamepata namba ya wakilishi zanzibar wa kuingizwa kwenye serikali kama mawaziri wangrvunja kambi yao ya upinzani? au hii imekuja kwa choyo na chuki binafsi zisizoegemea sheria bali utashi tu ?
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wishiful thinking.
  Kama ni Soka Umeotea au umefunga goli kwa mkono.
   
 14. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Utaundaje upinzani wakati nawe unashiriki kwenye serikali!!! It is none sense na meaningless. Chadema wana 'vichwa'. Before acting, they start by thinking in all dimensions. Hawakurupuki na hii ndiyo tabia inayowajengea heshima mbele ya jamii ya wasomi.
   
 15. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jee kuulisha watu arusha bila ya kuangalia sheria vizuri si kukurupuka?
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mtu wa Pwani , hivi unashindwa kuangalia siasa za Tanzania zikoje?
  Hivi unawezekanaje CUF na CCM kuwa wamoja Zanzibar na kisha kuwa Wapinzani Bara, Mapalala alianzisha Chama vizuri sana Hamadi akaja kukiua Kile Chama na kuanzisha chama kingine chenye Malengo ya Kuitenga Zanzibar na kuifanya ni nchi nje ya Muungano sawasawa, Hilo kalifanya kiasi kwamba hata Maprofessor (Safari, Lipumba) hawakuliona, Hamadi keshapata alichokuwa anakitaka sawasawa,
  Chadema hawawezi kuunda kambi hiyo yenye mkono wa CCM, Hapo hakuna chama cha upinzani zaidi ya Chadema vyote vilivyobakia (TLP, UDP, NCCR nk) ni vibaraka wa CCM, sawasawa
   
 17. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo unataka kusema CUF ni chama cha Zenj?
   
 18. n

  niweze JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijui jibu huna kweli au unataka tukuchangie. Tangu lini au unafikiri Chadema wana haja ya kwenda Zanzibar? Uamuzi wa Hamad na CUF-Zanzibar kujiunga na CCM kuongoza Serikali ya Zanzibar unafikiri ni malengo ya ukweli au mipango ya Hamad kurudi CCM. Kitu gani Hamad kilimfanya akimbilie kukubali matokeo ya tofauti asilimia moja? Au CCM na Hamad wanaona watanzania ni vichaa kama wao...Hamad alishapanga matokeo na CCM na alijua kitu gani kita tangazwa na hata kataa chochote. Shida ya CUF ni Visiwani na tunaona wazi sera zao zinalenga Visiwani. Chadema hawatakubwali kushirikiana na chama-Traitors. CUF wanatumiwa na CCM na kutaka kuchafua Bunge la Muungano na Hii Haitatokea kamwe. Chadema wana haki ya kukataa na viongozi wowote wale wasioitakia Tanzania mema. Ndoa ya Hamad na CCM tutaiona itafika wapi? Wanaoumia ni hao hao wananchi wa visiwani na sisi bara we don't want nothing to do with them and they should do the same for us... Visiwani ni Visiwani na Bara ni Bara (Tannganyika)
   
 19. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa hio chadema ni chama cha Tanganyika pekee? haina mpango wa kuwakilisha matatizo ya upande wa zenji?
   
 20. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Ndugu yangu nani amevuruga kambi ya upinzani au ni wivu tu ndo umewajaa watu?
   
Loading...