Karibu vyama vyote vya siasa nchini hususani vile vikubwa vimekuwa vikitumia hoja ya VIKAO HALALI VYA CHAMA kama njia ya kubana wanachama wake kutoa maoni; au labda kwa usahihi, kuwazuia kueleza maovu ya chama. Katika hili, CHADEMA ndo sio wastahimilivu hata kidogo; heri ya CCM wanavumulia wanachama wao katika kile kinachoitwa kutoa habari za chama bila kupitia viako halali vya chama. Kwa bahati mbaya kabisa, wana-CHADEMA wa kawaida nao wameingia kwenye mtego huu, kwamba inapotokea mwana-CHADEMA ameeleza mambo yanayowachukiza viongozi nje ya utaratibu wa kawaida; wana-CHADEMA hawa wa kawaida watakuja juu na kumtuhumu mwenzao kwa kumuita majina mbalimbali ya hovyo hovyo!
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa kawaida wa vyama vya kisiasa nadhani wanatakiwa kuamka na kugundua kwamba hiki kinachoitwa kwamba ni VIKAO HALALI VYA CHAMA ni ghiriba tu za viongozi wa vyama hivi ya kutaka yale mabaya ya vyama yasisemwe! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA kwa hakika kina jina la kuvutia na ndio maana hata wale wapenzi na wanachama wa kawaida nao wamekuwa wakiimba nyimbo hizi za VIKAO HALALI VYA CHAMA! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA ni kama kile kingine kinachoitwa UTAWALA BORA ambao Watanzania wengi tumekuwa tukiupigia upatu bila kufahamu kwamba UTAWALA BORA ni kichaka cha maovu ya viongozi na watendaji mbalimbali! Utawala Bora hauwezi kuwa na manufaaa kwa wananchi ikiwa unakuwa practiced kwenye jamii isiyo na maadili kama ya kwetu!
Sasa turudi kwenye hiki kinachoitwa kwamba VIKAO HALALI VYA CHAMA!! Hivi leo hii tuseme kuna mwanachama ana uhakika kabisa kwamba (say) Dr. Slaa au Freeman Mbowe amefanya ABC; tena jambo la fedheha kabisa! Hivi kweli mwanachama huyo anaweza kuwa na Ujasiri wa kusimama mbele ya VIKAO HALALI VYA CHAMA na kutamka waziwazi maovu hayo? Kama atakuwa na huo ujasiri, ni wanachama wangapi wanaweza kuwa na huo ujasiri wa kumchana LIVE mwenyekiti au katibu wa chama ambao tayari wamesha-prove kwamba hawana uvumilivu dhidi ya maoni hasi!
Kwa upande wangu, sina tatizo na hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini nadhani ni busara watu tukaangalia ni nani wanapaswa kuachiwa kuimba nyimbo hizo! Mwacheni Mbowe, mwacheni Dr. Slaa au watu wengine kama hao waimbe hizo nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha nafasi zao kwenye chama! Sitaki kuamini kwamba kutahatarisha uhai wa chama unless kama tunataka kusema CHADEMA ni MBOWE au SLAA! Wakati sioni tatizo kwa akina Mbowe kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini kwa mpenzi, shabiki na mwanachama wa kawaida ambae wala hajui hata viatu anavyovaa Dr. Slaa ni rangi gani au vile vya Mbowe; basi kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA ni uzuzu! Ni uzuzu kwa sababu whether you like it or not; kamwe hutaweza kufahamu ukweli mchungu unaokihusu chama chako kupitia hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA unless if youre prepared whether for bad or worse, wewe na chama chako tu kama ilivyo kwa Waislamu au Wakristo na dini zao!!
Hawa watu na wanachama wa kawaida nadhani ingekuwa ni busara zaidi kujadili contents za tuhuma kuliko kungangana na VIKAO HALALI VYA CHAMA ambavyo hata wao wenyewe hawahudhurii! Hili ambalo kwa wana-CHADEMA wanajidanganya kwamba eti ni kutowafumbia macho wasaliti ni ujinga mtupu, sana sana lina-prove ni jinsi gani UONGOZI WA CHADEMA unavyoandamwa na vivuli vya uoga! Swali la VIKAO HALALI VYA CHAMA linatumika kama njia ya kuwaziba watu midomo! Ni ajabu CCM iliyojaa ma-conservatives angalau inavumilia maoni makali ya wananchama wao yanayotolewa dhidi ya chama chao na wakati mwingine dhidi ya viongozi! Hivi ni nani asiyejua kwamba Nape na Samuel Sitta walikuwa on transit kuelekea CCJ? Hata hivyo waliwavumulia
. itakuwa ni ujinga kudhani kwamba uongozi wa juu wa chama na serikali hawakufahamu harakati hizo za akina Sitta!
Kuna Columnist mmoja kwenye gazeti la Raia Mwema anajiita MSOMAJI RAIA! Huyu jamaa huwa anaiponda wazi wazi serikali ya Kikwette! Na kwenye baadhi ya makala zake; huwa anamponda hata JK mwenyewe! Lakini whats so interesting, MSOMAJI RAIA ni wa ndani katika serikali ya Kikwete; namfahamu! Sasa ikiwa mtu wa kawaida kama mimi nafahamu whos MSOMAJI RAIA, itakuja kuwa KIkwette mwenyewe ambae amezungukwa na wana-intelejensia kadhaa kila Idara?! Hata hivyo, Kikwete anamvumilia MSOMAJI RAIA!
Huku Uswahilini kuna tabia Fulani imezoeleka kabisa! Unakuta mzazi analetewa mashitaka kwamba kijana wake amedokowa/ameiba mahali, au labda nyumba ya mtaa wa pili. Ni kawaida kukuta wazazi wanakuja juu, mithili ya moto wa kifuu kwamba mtoto wao anasingiziwa; KATU HAWEZI KUWA MWIZI. Wapo wanaofikia kusema hizo ni chuki tu utafikiri mzazi husika huwa anatembea na mwanae kila mahali! Siku wanakuja kutanabahi, anakuja kusikia kwamba Mwanao yupo Jela au kapigwa moto! Wazazi wa aina hii ndo mashabiki wengi wa CHADEMA walivyo! Wakati si Dr. Slaa wala Mbowe wana sifa za kuwa Malaika lakini wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wanataka kufanya kama hawa watu ni MALAIKA ambao tunaambiwa huwa hawafanyi makosa!
Lililo wazi ni kwamba, mwanadamu pekee asiyefanya makosa ni MAITI! Youll never be free of mistakes unless if youre dead!