Kila nyumba na utawala wake.Hebu,nieleze katika jamii yetu nani alimvumilia Mfanyakazi wa nyumbani/Housegirl ambaye anatoa siri za nyumbani kwake kwa majirani zake,wafanyakazi wenzake,wakristo wenzake,waislam wenzake,wanasimba wenzake au wanayanga wenzake???
Kwamba kila nyumba na utawala wake ni jambo lisilo na shaka hata punje, na labda kwa nyongeza tu, hata kwamba kila utawala una sheria na taratibu zake si jambo linalohitaji mjadala; kwavile hivyo ndivyo hasa ilivyo! Kwa bahati mbaya mkuu wangu, naona nawe ni kama umejikita kwenye suala la Mwigamba; anyway, wengi akili zao wameelekeza huko ingawaje nilichosema mimi ni ghiriba ya viongozi wetu kutumia kile kinachoitwa vikao halali vya chama kama njia ya kuwafunga watu midomo! Lakini kwa upande mwingine, sina shida sana na hao viongozi wanaojificha kwenye kichaka cha Vikao Halali Vya Chama pamoja na Katiba; shida niliyonayo mimi ni hawa watu wa kawaida kushabikia nyimbo hizi bila kufahamu nini hasa malengo yake! Wengine ni vijana wadogo lakini huku wakikazana kujifunika gubi gubi kwa koti la Conservative Thinking!
Leo hii Jakaya Kikwete ni Rais wangu! Akitokea mtu ndani ya system akaja JF na Fake ID akasema Mr. President amefanya hili na lile na linaleta sense! Hakika nitakuwa zuzu nikimshutumu huyo mtu na kumwambia ni kwanini hakutumia Vikao Halali! Hayo ya Vikao Halali nitwaachia wahusika! Kama tuhuma zenyewe ni dhidi ya CCM nitawaachia akina Nape au ma-conservatives wengine kama akina Kingunge. Lau kama ni tuhuma ndani ya serikali pia nitawaachia wahusika, ikiwa ni akina Salva au yeyote Yule! Hao wana wajibu wa kufanya hivyo, kwa sababu pamoja na mambo mengine, tuache unafiki, pia watakuwa wanatetea mkate wao wa kila siku! Hakika kama tuhuma zinaleta sense, nitamshukuru huyu Fake ID Users kwa kunisaidia kufahamu ambayo ima faima; nisingeyafahamu! Sasa ikiwa JK angeendelea kugombea, basi uamuzi ungekuwa wangu; kwamba pamoja na yote hayo bado anafaa au vinginevyo!
Lakini kwa upande mwingine ni kwamba, ingawaje I don't abuse the use of Vikao Halali vya Chama na kuheshimu Katiba, lakini ninachosema ni kwamba wanasiasa wamekuwa wakitumia hoja hizo kama DEFENSE MECHANISM! Kama Defense Mechanism coz' wanafahamu ni watu wachache sana au hakuna kabisa watakaokuwa na ujasiri wa kutoa tuhuma mzito mzito mbele ya vikao halali vya chama hata kama kweli tuhuma hizo zipo! Tutake tusitake; kila sekta kuna BIG FISHES; THE UNTOUCHABLE! Na kitu kibaya zaidi ni kwamba, at any possible COURAGEOUS PERSON there's at least ONE BIG FISH behind or around him/her! Kwa mfano, mtu kama
Ben Saanane, mie naamini kabisa kwamba he's so Courageous! Lakini hata hivyo; asikudanganye mtu, unaweza kuta Ben huyo huyo akikutana na baadhi ya watu/mtu mwenyewe anaufyata! Anaweza kuwa na ujasiri wa ajabu wa kueleza maovu ya Mr. X lakini asiwe na uthubutu wa kufanya hivyo against Mr. Y! That's to say, TO EVERY COURAGEOUS PERSON, THERE'S AT LEAST ONE BIG FISH AROUND/BEHIND HIM/HER!!!
Sasa yanapotokea mazingira kama hayo, kwamba tuseme mtu ana tuhuma dhidi ya BIG FISHE(S), na ana uhakika kabisa kwamba tuhuma alizonazo ni sahihi lakini hana ujasiri wa kutoa hadharani tuhuma hizo kutokana na uzito wa watuhumiwa! Sasa, ni ama mtu huyu azinyamazie tuhuma au atafute alternative means yak u-expose! Most likely, ikiwa mtu ataamua ku-expose basi wengi wao kama sio wote (pamoja na hawa ambao hapa wanaongelea Vikao Halali) wata-opt kutumia Nick Names kwenye mitandao ya kijamii kama JF! Lakini kwa vile akili yetu inaonekana kuthamini Chama Kwanza, si ajabu wengi wao wakaamua kukaa kimya unless kama tuhuma hizo zinawahusu wapinzani/wahasimu wao!!
Lakini kwa upande mwingine, kumekuwa na matumizi ya double standard linapokuja suala la umuhimu wa vikao halali na kuheshimu katiba! Kwa mfano, hata maoni ya wana-CHADEMA kwenye uzi huu; unakuta ni kama wengi wanaunga mkono suala la akina Mbowe na Dr. Slaa kuendelea kuwa madarakani! To be honest, it's none of my business! Lakini katiba si inasema hawawezi kugombea tena? Maana yake ni kwamba, wakigombea tena itakuwa katiba imebanangwa vibaya mno! Labda jibu jepesi katika hilo supportes watuzungumzia suala la kubadili katiba ili kuwapa extra time!! Watatumia maneno mazuri mazuri na tena yenye busara na hekima tele ili mradi tu kuhalalisha hilo! Wapo watakaosema it'll take a time for the new administration to take off wakati uchaguzi upo njiani; wapo watakaosema makamanda hawabadilishi in the middle of war; lakini yote hayo katu hayatafunika ukweli kwamba hatua kama hiyo itathibitisha mambo makuu mawili, ung'ang'anizi wa madaraka (a form of dictatorship) na ubanangaji wa kutisha wa katiba ile ile ambayo hapa hao hao supportes wanasema inabidi iheshimiwe!