CHADEMA na kichaka cha "vikao halali vya chama"

CHADEMA na kichaka cha "vikao halali vya chama"

Wewe hupiganii taifa lako kwa namna yoyote ile bali upo humu kulinda mkate wako hasa baada ya kuchukua nafasi ya Ludovick. Pia hupiganii chama chako bali unapigania kakikundi kadogo ka viongozi wa juu ambao kwa namna moja au nyingine una nasaba nao au unanufaika kutokana na wao kuwa viongozi

Suit yourself.

Ndiyo hivyo tena hamna la kufanya.
 
Kama hatuheshimu katiba tuliyojitungia wenyewe hatuwezi kuheshimu kafiba ya nchi au sheria na mikataba ya kimataifa.

Chama kina taratibu zake na demokrasia in essence hutekelezwa kwa utaratibu

Kutumia Fake ID kuchafua watu au taasisi ni kielelezo cha unafiki na ukosefu wa maadili

Mimi kama mwanachama ninso ujasiri wa kukosoa kwenye vikao bila kutafuna maneno na inajulikana hivyo,sasa iweje kiongozi ashindwe kukosoa kwenye vikao?

Ukiweza kutumia ID fake kuchafua au kuhujumu taasisi basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuingia kwenye secret mission ya kukihujumu chama

Ningekua kiongozi kwenye taasisi yoyote halafu nikakosa uhuru wa kutoa maoni kwenye vikao basi nitajiuzulu mara moja.
Honestly speaking,
Your comment sounds good; as good as matumizi ya VIKAO HALALI VYA CHAMA; as good as GOOD GOVERNANCE! Yote hayo, yanaashiria jambo lile lile, kuminya uhuru wa maoni! Waandishi wa Habari huwa wanakumbana na mambo kama hayo pale wanapotaka habari ama serikalini au kwenye taasisi kubwa kubwa! Huko wanakutana na maneno "MIMI SIO MSEMAJI WA WIZARA/IDARA/KAMPUNI!"

So, frankly speaking, nakubaliana na maoni yako kwa 100% lakini kwa kiasi kikubwa mawazo kama hayo huwa yanatumika kama DEFENSIVE MECHANISM! Wote tupo tayari kukaa kimya kuona Katiba inavunjwa ikiwa kuvunjwa huko hakuathiri maslahi ya uongozi lakini tunakuwa wepesi wa kukimbilia suala la kuheshimu katiba pale inapoonekana kwamba uvunjwaji huo unahatarisha maslahi ya watu wenye nguvu! To make it in a single sentence, double standard zimekuwa zikitumika linapokuja suala la kuheshimu katiba!

Hapo kwenye RED, nakuunga mkono mia kwa mia lakini kwa bahati mbaya viongozi wetu wa kisiasa kama sio wote Siasa ni biashara, ni ajira! Ni bahati mbaya sana Watanzania wengi ni wabinafsi; mtu mbinafsi kamwe hawezi kuwa na ujasiri wa kujiuzulu! Hata hivyo, I don't justify!
 
Kama umeongea kwa akili wakati ni siasa zilezile za kutoona mbali,nani kasema Dr.Slaa na Mbowe ni malaika? Tunajua hawa hawa ni binadamu kwa uhalisia kabisa na wanaweza kufanya makosa kama binadamu yeyote yule,lakini kwa namna siasa inavyochezwa Tanzania mimi binafsi napenda kuamini hawa ndio mwarobaini wa ccm kuliko wewe ambaye unataka tuendelee kuwa kwenye kongwa la utumwa ccm kwa sababu tu umelambishwa.

Vikao halali vya chama ulitaka wewe uwepo nd'o viwe halali,mbona jk akikutana na watu wake wawili watatu wa ccm pale ikulu wanatoa tamko hatujasikia ukisema lolote hapa?

Kama wewe unavyojmjua MSOMAJI WA RAIA hata mimi nimekung'amua hapa kuwa wewe ni nani,ila sasa wewe umetia aibu kwa sababu unaisaliti course ya ukombozi iliyokufikisha ulipo,ila kwasababu wewe ni failure wa kawaida umepofushwa na vipande thelasini vya ccm nakuuza utu wako na heshima kubwa ambayo kwa uvumilivu kidogo tu ungekuwa nayo shame on you hukohuko ulikojijaladia na hili li id fake.
 
Umejuaje kama mtu anashindwa kunena ya moyoni.Leta ushahidi hapa.Acha umbeya maana JF ni facts tu zinazohitajika
Ushahidi wa wazi ni pale Zitto Kabwe ambaye ni Naibu Katibu Mkuu alipomwandikia Dr Slaa ambaye ni Katibu Mkuu barua binafsi ya kuomba chama kimsimamishe uongozi Lwakatare kutokana na kupatikana video akijihusisha kupanga njama za kumdhuru Denis Msacky. Hawa kama ni viongozi wa karibu, ilishindikana hayo aliyokuwa nayo Zitto kueleza ndani ya hivyo unavyoita vikao halali? Mbaya zaidi, ile barua baada ya kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu, barua hiyo ilitundikwa mtandaoni na Mtu ambaye anadhaniwa kuwa ni Katibu Mkuu kupitia Id fake. Kwangu nilitafakari sana tukio lile na nimebaini yafuatayo
  1. Viongozi wa ngazi za chini wa CHADEMA hawana uhuru wa kueleza jambo mbele ya viongozi wa juu
  2. hakuna mawasiliano ya ana kwa ana baina ya Dr Slaa na Zitto
  3. homa ya uchaguzi mkuu inafanya viongozi wa juu wajenge hofu kwa viongozi wa chini
 
Ni kifungu Kipi nilichokiuka kikatiba?Mbona tangu nimekua JF hujawahi kuuliza kama mimi ni msemaji wa CHADEMA?Acheni woga.I'm here to stay.Siendi popote na nitaendeleza mapambano hata kama hamtaki
Hakuna aliyekuambia kuwa uondoke bali unashangaza kwa jinsi unavyokuwa msemaji wa CHADEMA au viongozi wake bila ya kutumwa. Waache watu waseme ya kweli na wewe huna mamlaka ya kuwakata ngebe
 
Na ndivyo inavyostahili kipindi hiki kuliko wakati wowote.Marafiki wa maadui zetu na mifumo yao hawatapata nafasi.

Majenerali wakuu hawabadilishwi katikati ya vita

Kama CCM mna uchungu sana wachukueni mnaowataka wakagombee huko kwenu.Msitupangie aina ya silaha za kuwapiga nazo ninyi.

Mtaishia kulalama tu na kupoteza muda.Hampati kitu.So, go home
well done kamanda
 
Walimu wako walipata shida sana

Hoja ninazojibu hapa ninajibu kwa uelewa wangu na tangu nimejiunga JF mwaka 2007 nimekua nikifanya hivyo.Unataka wanikemee kwa lipi?Kuipigania nchi yangu kwa hoja?Kukitetea na kukilinda chama changu ambao ni wajibu wa msingi kwa mwanachama kikatiba?

Unaongelea kubadili katiba?Hili limekujaje hapa?Huwezi hata kujieleza

Unaelewa vizuri sana tu,unajua kwa kusoma michango na uandishi tunajuana uwezo pia?????!!!!

Wewe sio mjinga kiasi cha.kushindwa kuelewa haya!!!! Na mimi sio mjinga kiasi cha kushindwa kuandika kitu kikasomeka na kueleweka!!!! Ila shida ni attitude uliyonayo na unaijua na umeamua kuichagua,kuilea na.kuifanyia kazi kila uchao,sio bahati mbaya ni delibarate na ndio inakufanya uwe hapa jukwaani!!!!!

Ila chama huanzishwa na wachache, hujengwa na wengi na kubomolewa kwa makosa ya wachache kwa makusudi au kwa bahati mbaya!!!!!!

Chaguo ni lenu kubadilika na kuchukua maoni au kubaki mnabisha kwa kila kitu wakati hali inaendelea kubadilika!!!!!!
 
Kama hatuheshimu katiba tuliyojitungia wenyewe hatuwezi kuheshimu kafiba ya nchi au sheria na mikataba ya kimataifa.

Chama kina taratibu zake na demokrasia in essence hutekelezwa kwa utaratibu

Kutumia Fake ID kuchafua watu au taasisi ni kielelezo cha unafiki na ukosefu wa maadili

Mimi kama mwanachama ninso ujasiri wa kukosoa kwenye vikao bila kutafuna maneno na inajulikana hivyo,sasa iweje kiongozi ashindwe kukosoa kwenye vikao?

Ukiweza kutumia ID fake kuchafua au kuhujumu taasisi basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuingia kwenye secret mission ya kukihujumu chama

Ningekua kiongozi kwenye taasisi yoyote halafu nikakosa uhuru wa kutoa maoni kwenye vikao basi nitajiuzulu mara moja.
Punguza unafiki kidogo, kwa issue ya Zitto kipindi kile ulifanya hivyo? Kesi ya Mwigamba na ya kwako kuhusu Zitto mbona haina tofauti kabisa ( Wote mmetangaza mabo yenu humu JF) cha ajabu hadi leo hii bado wamekuacha tu kwenye hicho chama.
 
Hakuna aliyekuambia kuwa uondoke bali unashangaza kwa jinsi unavyokuwa msemaji wa CHADEMA au viongozi wake bila ya kutumwa. Waache watu waseme ya kweli na wewe huna mamlaka ya kuwakata ngebe
jibu hoja, yeye c mwanachadema kwa nini asiseme ukweli, au unaona malengo yenu ya kuua chadema yanafifia maana dead line ya kuua chama inakaribia na hakuna mafanikio yoyote kuhusu project yenu hiyo chafu ya kutoka kuzim
 
CHADEMA wanapambana na dola nas si chama dola kama ambavyo mara nyingine imekuwa ikifahamika,hivyo wanafanya siasa kwenye mazingira magumu sana,na katika hayo mazingira magumu usitarajie kila mkakati wao utakuwa unajulikana navyombo vya habari,vikiwemo hivyo VIKAO HALALI VYA CHAMA.Japo siijui vizuri sana hiyo katba yao ya chama.
 
Nimesoma thread yako kwa umakini sana. Nimepata tafakari ya mambo ma-nne;

1. Vyama vyetu vya siasa vimejaa ubabaishaji, wachache walio na nyadhifa za juu wanaamua kwa makusudi kuhodhi madaraka na kufanya wapendavyo. Hii si tofauti kwa CCM,CDM,CUF au Vyama vingine.

2. Kutokana na taratibu za vyama kuvunjwa na viongozi hawa ambao jambo pekee wanalolijua kwenye katiba zao ni ''Vikao halali'' na ''adhabu kwa wasema ovyo'' wasiotumia vikao halali vya chama, vyama vingi vya kisiasa vimejaa manung'uniko na malumbano ya chini kwa chini

3. Kwa mfumo wa vyama vya siasa vya Tanzania inaonekana wazi kuwa kuna waanzilishi wa vyama ambao pia ni kama wamiliki hawa wana sauti na maamuzi ya mwisho hata kama hiyo itamaanisha kuvunja katiba ya Chama.

4. Wanasiasa wengi kama si wote wamejaa ubinafsi na wakandamizaji wakubwa wa DEMOKRASIANA NI WATU kujitazama wenyewe huku wakijivika tafswira ya kutetea wanyonge. Kwa mfano, kwa nini mtu mmoja abaki kuwa Mwenyekiti wa Chama kadiri apendavyo? Angalia pale CUF - Prof.Lipumba yeye yupo tu siku zote na mwenzake Maalim Seif. Hivi ni kweli kuwa hizi nafasi zinawatosha wao tu?!
Hii ndio sababu itakayochelewesha mabadiliko ya kisiasa kwenye hii nchi yetu.
Nakubalina nawe moja kwa kiasi kikubwa kabisa lakini ningependa sana kuzungumzia hapo namba 2, RED! Hakika, hicho ndicho kilichopo ama ndicho kinaendelea; NIDHAMU YA WOGA! Jambo hilo si jema hata kidogo. Hii nidhamu ya woga ndiyo ilikuwapo Awamu ya Kwanza ya Utawala wa nchi hii hadi watu wakadhani kwamba viongozi wote walikuwa na maadili; kumbe walikuwa na nidhamu ya woga dhidi ya Rais wa nchi na mwenyekiti wa chama, Hayati Mwalimu Nyerere! Matokeo yake, Mwalimu alipong'atuka tu, viongozi wale wale ambao walidhaniwa kwamba ni waadilifu wakubwa wakageuka na kuwa mafisadi na walafi wakubwa! Wakakomaba kila kitu, wakaokota hadi punje za ubwabwa zilizodondokea kwenye mikeka ili mradi tu akina siye hata zile chambe za zilizomwagika tusiambulie!

Kwa uhai wa chama, huwezi kujenga base ya waoga! Nakubali kabisa kwamba ni lazima kuwe na nidhamu katika chama lakini matakwa hayo yanaonekana kutumika vibaya.
 
Kama umeongea kwa akili wakati ni siasa zilezile za kutoona mbali,nani kasema Dr.Slaa na Mbowe ni malaika? Tunajua hawa hawa ni binadamu kwa uhalisia kabisa na wanaweza kufanya makosa kama binadamu yeyote yule,lakini kwa namna siasa inavyochezwa Tanzania mimi binafsi napenda kuamini hawa ndio mwarobaini wa ccm kuliko wewe ambaye unataka tuendelee kuwa kwenye kongwa la utumwa ccm kwa sababu tu umelambishwa.

Vikao halali vya chama ulitaka wewe uwepo nd'o viwe halali,mbona jk akikutana na watu wake wawili watatu wa ccm pale ikulu wanatoa tamko hatujasikia ukisema lolote hapa?

Kama wewe unavyojmjua MSOMAJI WA RAIA hata mimi nimekung'amua hapa kuwa wewe ni nani,ila sasa wewe umetia aibu kwa sababu unaisaliti course ya ukombozi iliyokufikisha ulipo,ila kwasababu wewe ni failure wa kawaida umepofushwa na vipande thelasini vya ccm nakuuza utu wako na heshima kubwa ambayo kwa uvumilivu kidogo tu ungekuwa nayo shame on you hukohuko ulikojijaladia na hili li id fake.
Haidhuru kwamba uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo; TUENDELEE!
 
CHADEMA wanapambana na dola nas si chama dola kama ambavyo mara nyingine imekuwa ikifahamika,hivyo wanafanya siasa kwenye mazingira magumu sana,na katika hayo mazingira magumu usitarajie kila mkakati wao utakuwa unajulikana navyombo vya habari,vikiwemo hivyo VIKAO HALALI VYA CHAMA.Japo siijui vizuri sana hiyo katba yao ya chama.
Halafu bado unatoa povu! Maajabu sana haya.....
 
Kama hatuheshimu katiba tuliyojitungia wenyewe hatuwezi kuheshimu kafiba ya nchi au sheria na mikataba ya kimataifa.

Chama kina taratibu zake na demokrasia in essence hutekelezwa kwa utaratibu

Kutumia Fake ID kuchafua watu au taasisi ni kielelezo cha unafiki na ukosefu wa maadili

Mimi kama mwanachama ninso ujasiri wa kukosoa kwenye vikao bila kutafuna maneno na inajulikana hivyo,sasa iweje kiongozi ashindwe kukosoa kwenye vikao?

Ukiweza kutumia ID fake kuchafua au kuhujumu taasisi basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuingia kwenye secret mission ya kukihujumu chama

Ningekua kiongozi kwenye taasisi yoyote halafu nikakosa uhuru wa kutoa maoni kwenye vikao basi nitajiuzulu mara moja.

Pole na kazi kaka, najua mko katika jukumu zito sana la kuhakikisha Taifa linakombolewa kutoka kwa dhalimu CCM, inshort tunaweza kuwa na watu wa mioyo ya ki-CCM ndani ya CDM na tunaweza kudhani tumewafahamu lakini kumbe hatujawafahamu.

Kuna kitu kwenye private Companies kinaitwa "Whistle-blowing", hiki kinahusu kuripoti mis-conduct internally bila unayemripoti kufahamu chochote, na hii inakuwa effective kama tu watu wanaokuwa roported wako chini ya governance (Board of Decision Makers) na pia Board yenyewe iko independent, inafata confidentiality, inasikiliza, inafanyia kazi hizo whistle-blows!

Changamoto inakuwa kubwa pale anayetakiwa kuwa reported ni member wa hiyo Board ya Maamuzi, itakuwaje? Na kama ilishawahi kutokea katika mfumo wa kawaida watu wakaripoti issues ambazo ni genuine halafu hazikufanyiwa kazi, grievances zitakuwa nyingi na mwisho wa siku inakuwa ni kutoka nje ya chama kama hivi.

Chama kama chama lazima kifanye assessment ya jinsi ya kureport issues ndani ya chama, baadhi ambazo ni kazi kumwambia mtu makavu, kuwe na huo utaratibu wa Whistleblowing, malalamiko yafanyiwe kazi, kusiwe na kuanza kutafuta walio-report badala yake tujadiri kilicholetwa.

Ni hayo tu kwangu!
 
tatizo la chadema ni kuwa hawataki kuambiwa ukweli. Ukweli kwao ni usaliti

kweli kabisa, mmejujua hivyo achana nasi. Tu kilimani bondeni jerusalem imezingirwa na wafirisi hali sio mbaya punde tutaikomboa. Lolote au yeyote anayejaribu kutuondoa kwenye umakini ulio tutoa mbali atachukuliwa kuwa mfirisi tutampitia juu bila kumusikiliza hadi tutakapokuwa tumeingia jerusarem. Tunawashauri hao wasema ukweli wawe wamesubiri isije ukweli wao ukawafanya wakasahaulika wakati shamura shamura zinaendelea ktk nchi ya maziwa na asali tanzania.
 
Ushahidi wa wazi ni pale Zitto Kabwe ambaye ni Naibu Katibu Mkuu alipomwandikia Dr Slaa ambaye ni Katibu Mkuu barua binafsi ya kuomba chama kimsimamishe uongozi Lwakatare kutokana na kupatikana video akijihusisha kupanga njama za kumdhuru Denis Msacky. Hawa kama ni viongozi wa karibu, ilishindikana hayo aliyokuwa nayo Zitto kueleza ndani ya hivyo unavyoita vikao halali? Mbaya zaidi, ile barua baada ya kuiwasilisha kwa Katibu Mkuu, barua hiyo ilitundikwa mtandaoni na Mtu ambaye anadhaniwa kuwa ni Katibu Mkuu kupitia Id fake. Kwangu nilitafakari sana tukio lile na nimebaini yafuatayo
  1. Viongozi wa ngazi za chini wa CHADEMA hawana uhuru wa kueleza jambo mbele ya viongozi wa juu
  2. hakuna mawasiliano ya ana kwa ana baina ya Dr Slaa na Zitto
  3. homa ya uchaguzi mkuu inafanya viongozi wa juu wajenge hofu kwa viongozi wa chini

Haya mambo ya kudhani yanatufanya tunaopenda data na logic tusikuchukulie serious.Ni umbea

Ni lini ID ya Dr.Slaa iliweka barua humu?Leta uthibitisho
 
Unaelewa vizuri sana tu,unajua kwa kusoma michango na uandishi tunajuana uwezo pia?????!!!!

Wewe sio mjinga kiasi cha.kushindwa kuelewa haya!!!! Na mimi sio mjinga kiasi cha kushindwa kuandika kitu kikasomeka na kueleweka!!!! Ila shida ni attitude uliyonayo na unaijua na umeamua kuichagua,kuilea na.kuifanyia kazi kila uchao,sio bahati mbaya ni delibarate na ndio inakufanya uwe hapa jukwaani!!!!!

Ila chama huanzishwa na wachache, hujengwa na wengi na kubomolewa kwa makosa ya wachache kwa makusudi au kwa bahati mbaya!!!!!!

Chaguo ni lenu kubadilika na kuchukua maoni au kubaki mnabisha kwa kila kitu wakati hali inaendelea kubadilika!!!!!!

Ni lini ulishawahi kuwa na nia njema na CHADEMA hadi maoni yako yachukuliwe serious kiasi hicho wakati siku zote umeonyesha chuki ya hali ya juu dhidi ya CHADEMA?Acha hila
 
Punguza unafiki kidogo, kwa issue ya Zitto kipindi kile ulifanya hivyo? Kesi ya Mwigamba na ya kwako kuhusu Zitto mbona haina tofauti kabisa ( Wote mmetangaza mabo yenu humu JF) cha ajabu hadi leo hii bado wamekuacha tu kwenye hicho chama.

Mnafiki ni wewe.Sasa kama haina tofauti mnatoa mapovu ya nini kuhusu hatua zilizochukuliwa?Mimi niliadhibiwa na kusimamishwa kugombea uongozi kwa muda wa mwaka 1.Ni dhahiri kama ningekua kiongozi ningevuliwa madaraka.

Mimi nilikua nakitetea na kukilinda chama changu na kujibu tuhuma zilizotolewa juu yangu in the process nikajikuta nimevunja kanuni bila kutarajia.Nilikata rufaa kupinga adhabu ile kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama chetu

Acheni kulialia kinafiki.Mimi sikutumia ID fake na nilikua na ujasiri wa kukabiliana na yoyote bila kutafuna maneno.Usilinganishe oranges na apples.Unafiki tu
 
Back
Top Bottom