CHADEMA na kichaka cha "vikao halali vya chama"

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,152
Karibu vyama vyote vya siasa nchini hususani vile vikubwa vimekuwa vikitumia hoja ya VIKAO HALALI VYA CHAMA kama njia ya kubana wanachama wake kutoa maoni; au labda kwa usahihi, kuwazuia kueleza maovu ya chama. Katika hili, CHADEMA ndo sio wastahimilivu hata kidogo; heri ya CCM wanavumulia wanachama wao katika kile kinachoitwa kutoa habari za chama bila kupitia viako halali vya chama. Kwa bahati mbaya kabisa, wana-CHADEMA wa kawaida nao wameingia kwenye mtego huu, kwamba inapotokea mwana-CHADEMA ameeleza mambo yanayowachukiza viongozi nje ya utaratibu wa kawaida; wana-CHADEMA hawa wa kawaida watakuja juu na kumtuhumu mwenzao kwa kumuita majina mbalimbali ya hovyo hovyo!

Wapenzi, wanachama na mashabiki wa kawaida wa vyama vya kisiasa nadhani wanatakiwa kuamka na kugundua kwamba hiki kinachoitwa kwamba ni VIKAO HALALI VYA CHAMA ni ghiriba tu za viongozi wa vyama hivi ya kutaka yale mabaya ya vyama yasisemwe! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA kwa hakika kina jina la kuvutia na ndio maana hata wale wapenzi na wanachama wa kawaida nao wamekuwa wakiimba nyimbo hizi za VIKAO HALALI VYA CHAMA! Hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA ni kama kile kingine kinachoitwa UTAWALA BORA ambao Watanzania wengi tumekuwa tukiupigia upatu bila kufahamu kwamba UTAWALA BORA ni kichaka cha maovu ya viongozi na watendaji mbalimbali! Utawala Bora hauwezi kuwa na manufaaa kwa wananchi ikiwa unakuwa practiced kwenye jamii isiyo na maadili kama ya kwetu!

Sasa turudi kwenye hiki kinachoitwa kwamba VIKAO HALALI VYA CHAMA!! Hivi leo hii tuseme kuna mwanachama ana uhakika kabisa kwamba (say) Dr. Slaa au Freeman Mbowe amefanya ABC; tena jambo la fedheha kabisa! Hivi kweli mwanachama huyo anaweza kuwa na Ujasiri wa kusimama mbele ya VIKAO HALALI VYA CHAMA na kutamka waziwazi maovu hayo? Kama atakuwa na huo ujasiri, ni wanachama wangapi wanaweza kuwa na huo ujasiri wa kumchana LIVE mwenyekiti au katibu wa chama ambao tayari wamesha-prove kwamba hawana uvumilivu dhidi ya maoni hasi!

Kwa upande wangu, sina tatizo na hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini nadhani ni busara watu tukaangalia ni nani wanapaswa kuachiwa kuimba nyimbo hizo! Mwacheni Mbowe, mwacheni Dr. Slaa au watu wengine kama hao waimbe hizo nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA kwani kutofanya hivyo ni kuhatarisha nafasi zao kwenye chama! Sitaki kuamini kwamba kutahatarisha uhai wa chama unless kama tunataka kusema CHADEMA ni MBOWE au SLAA! Wakati sioni tatizo kwa akina Mbowe kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA lakini kwa mpenzi, shabiki na mwanachama wa kawaida ambae wala hajui hata viatu anavyovaa Dr. Slaa ni rangi gani au vile vya Mbowe; basi kuimba nyimbo za VIKAO HALALI VYA CHAMA ni uzuzu! Ni uzuzu kwa sababu whether you like it or not; kamwe hutaweza kufahamu ukweli mchungu unaokihusu chama chako kupitia hiki kinachoitwa VIKAO HALALI VYA CHAMA unless if you're prepared whether for bad or worse, wewe na chama chako tu kama ilivyo kwa Waislamu au Wakristo na dini zao!!

Hawa watu na wanachama wa kawaida nadhani ingekuwa ni busara zaidi kujadili contents za tuhuma kuliko kung'ang'ana na VIKAO HALALI VYA CHAMA ambavyo hata wao wenyewe hawahudhurii! Hili ambalo kwa wana-CHADEMA wanajidanganya kwamba eti ni kutowafumbia macho wasaliti ni ujinga mtupu, sana sana lina-prove ni jinsi gani UONGOZI WA CHADEMA unavyoandamwa na vivuli vya uoga! Swali la VIKAO HALALI VYA CHAMA linatumika kama njia ya kuwaziba watu midomo! Ni ajabu CCM iliyojaa ma-conservatives angalau inavumilia maoni makali ya wananchama wao yanayotolewa dhidi ya chama chao na wakati mwingine dhidi ya viongozi! Hivi ni nani asiyejua kwamba Nape na Samuel Sitta walikuwa on transit kuelekea CCJ? Hata hivyo waliwavumulia…. itakuwa ni ujinga kudhani kwamba uongozi wa juu wa chama na serikali hawakufahamu harakati hizo za akina Sitta!

Kuna Columnist mmoja kwenye gazeti la Raia Mwema anajiita MSOMAJI RAIA! Huyu jamaa huwa anaiponda wazi wazi serikali ya Kikwette! Na kwenye baadhi ya makala zake; huwa anamponda hata JK mwenyewe! Lakini what's so interesting, MSOMAJI RAIA ni wa ndani katika serikali ya Kikwete; namfahamu! Sasa ikiwa mtu wa kawaida kama mimi nafahamu who's MSOMAJI RAIA, itakuja kuwa KIkwette mwenyewe ambae amezungukwa na wana-intelejensia kadhaa kila Idara?! Hata hivyo, Kikwete anamvumilia MSOMAJI RAIA!

Huku Uswahilini kuna tabia Fulani imezoeleka kabisa! Unakuta mzazi analetewa mashitaka kwamba kijana wake amedokowa/ameiba mahali, au labda nyumba ya mtaa wa pili. Ni kawaida kukuta wazazi wanakuja juu, mithili ya moto wa kifuu kwamba mtoto wao anasingiziwa; KATU HAWEZI KUWA MWIZI. Wapo wanaofikia kusema hizo ni chuki tu utafikiri mzazi husika huwa anatembea na mwanae kila mahali! Siku wanakuja kutanabahi, anakuja kusikia kwamba Mwanao yupo Jela au kapigwa moto! Wazazi wa aina hii ndo mashabiki wengi wa CHADEMA walivyo! Wakati si Dr. Slaa wala Mbowe wana sifa za kuwa Malaika lakini wapenzi na mashabiki wa CHADEMA wanataka kufanya kama hawa watu ni MALAIKA ambao tunaambiwa huwa hawafanyi makosa!

Lililo wazi ni kwamba, mwanadamu pekee asiyefanya makosa ni MAITI! You'll never be free of mistakes unless if you're dead!
 
Kama hatuheshimu katiba tuliyojitungia wenyewe hatuwezi kuheshimu kafiba ya nchi au sheria na mikataba ya kimataifa.

Chama kina taratibu zake na demokrasia in essence hutekelezwa kwa utaratibu

Kutumia Fake ID kuchafua watu au taasisi ni kielelezo cha unafiki na ukosefu wa maadili

Mimi kama mwanachama ninso ujasiri wa kukosoa kwenye vikao bila kutafuna maneno na inajulikana hivyo,sasa iweje kiongozi ashindwe kukosoa kwenye vikao?

Ukiweza kutumia ID fake kuchafua au kuhujumu taasisi basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuingia kwenye secret mission ya kukihujumu chama

Ningekua kiongozi kwenye taasisi yoyote halafu nikakosa uhuru wa kutoa maoni kwenye vikao basi nitajiuzulu mara moja.
 
CCM wanahangaika sana na CHADEMA, nawaonya CCM mlishashindwa kuisambaratisha CHADEMA, mnachofanya ni kuzidi kuipa nguvu.
 
Dr.W.Slaa na Freeman A. Mbowe wanaiendesha Chadema kwa mkono wa chuma.

Na ndivyo inavyostahili kipindi hiki kuliko wakati wowote.Marafiki wa maadui zetu na mifumo yao hawatapata nafasi.

Majenerali wakuu hawabadilishwi katikati ya vita

Kama CCM mna uchungu sana wachukueni mnaowataka wakagombee huko kwenu.Msitupangie aina ya silaha za kuwapiga nazo ninyi.

Mtaishia kulalama tu na kupoteza muda.Hampati kitu.So, go home
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma thread yako kwa umakini sana. Nimepata tafakari ya mambo ma-nne;

1. Vyama vyetu vya siasa vimejaa ubabaishaji, wachache walio na nyadhifa za juu wanaamua kwa makusudi kuhodhi madaraka na kufanya wapendavyo. Hii si tofauti kwa CCM,CDM,CUF au Vyama vingine.

2. Kutokana na taratibu za vyama kuvunjwa na viongozi hawa ambao jambo pekee wanalolijua kwenye katiba zao ni ''Vikao halali'' na ''adhabu kwa wasema ovyo'' wasiotumia vikao halali vya chama, vyama vingi vya kisiasa vimejaa manung'uniko na malumbano ya chini kwa chini

3. Kwa mfumo wa vyama vya siasa vya Tanzania inaonekana wazi kuwa kuna waanzilishi wa vyama ambao pia ni kama wamiliki hawa wana sauti na maamuzi ya mwisho hata kama hiyo itamaanisha kuvunja katiba ya Chama.

4. Wanasiasa wengi kama si wote wamejaa ubinafsi na wakandamizaji wakubwa wa DEMOKRASIANA NI WATU kujitazama wenyewe huku wakijivika tafswira ya kutetea wanyonge. Kwa mfano, kwa nini mtu mmoja abaki kuwa Mwenyekiti wa Chama kadiri apendavyo? Angalia pale CUF - Prof.Lipumba yeye yupo tu siku zote na mwenzake Maalim Seif. Hivi ni kweli kuwa hizi nafasi zinawatosha wao tu?!
Hii ndio sababu itakayochelewesha mabadiliko ya kisiasa kwenye hii nchi yetu.
 
CHADEMA si chama cha siasa bali ni saccos ya Mbowe na DR Slaa
 
Dr.W.Slaa na Freeman A. Mbowe wanaiendesha Chadema kwa mkono wa chuma.
Bila hivyo CHADEMA itakuwa ccm C,uhuru bila nidhamu ni fujo,hamna uwanja sawa wa kufanya siasa Tanzania waliopo madarakani wapo radhi kufanya chochote kuhakikisha wanaviongoza vyama vyote kwa remote,wanashindwa kwa Chadema kwa sababu ya hicho unachotafsir kuwa ni mkono wa chuma.Kiongozi yeyote wa Chadema au mwanachama ambaye anaweza kuungana na mtazamo wako mfu huu hajui tulikotoka na wala tunakokwenda na Tanzania tunayoitaka.
 
Tatizo la chadema ni kuwa hawataki kuambiwa ukweli. Ukweli kwao ni usaliti
 
Mkuu, haya yanayoendelea yanatokea ndani ya CHADEMA. Ni makosa makubwa kwa CHADEMA kudhani kuwa kila baya linalotokea ndani ya chama chao linatokana na ushawishi au mkono wa ccm
ahahaha, sasa kwanini nyinyi CCM hamfurahii hayo masongesonge yanayotokea CHADEMA?
 
Kama hatuheshimu katiba tuliyojitungia wenyewe hatuwezi kuheshimu kafiba ya nchi au sheria na mikataba ya kimataifa.

Chama kina taratibu zake na demokrasia in essence hutekelezwa kwa utaratibu

Kutumia Fake ID kuchafua watu au taasisi ni kielelezo cha unafiki na ukosefu wa maadili

Mimi kama mwanachama ninso ujasiri wa kukosoa kwenye vikao bila kutafuna maneno na inajulikana hivyo,sasa iweje kiongozi ashindwe kukosoa kwenye vikao?

Ukiweza kutumia ID fake kuchafua au kuhujumu taasisi basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuingia kwenye secret mission ya kukihujumu chama

Ningekua kiongozi kwenye taasisi yoyote halafu nikakosa uhuru wa kutoa maoni kwenye vikao basi nitajiuzulu mara moja.

Hivi na wewe ni mwanachama wa kawaida eeenh!!!!!??????? Kawaida ipi unayoizungumzia hapa???!!!

Ujasiri huo unaouongelea ni ule wa kufundishwa au wa kuzaliwa????!!! Kuna tofauti hapo!!!!

Kama ilivyo kwa mambo mengine, wakati mwenyekiti ni KUB na.anapewa gari wakati yawezekana kuna wanaotingisha bunge zaid yake na hawajapewa gari basi ujue na personalities tunatofutiana!!!!!!!

In a way umeongeza chaka jingine linaitwa "katiba",kama ndio kila kitu why tunataka ibadilishwe na wengine wanawish ibaki???!!! Mbona mpaka watu wanatoka ukumbini kwa sababu ya uwakilishi wa makundi???!!! Umewahi kuyafikiria haya ndani ya chama chako????!!!!

Huyu kutumia ID fake litazame kwa jicho la wawakilishi wa wananchi kutoka bungeni au mbunge kupigana na askari!!!! Kuna mwananchi kamuagiza mbunge kutoka wakati wa vikao au kupigana na polisi au kulala???!!!!!!

Fanyieni kazi changamoto muda wa maneno hakuna!!!!!!

Wewe upo hapa unajibu hoja nyingi za chama na.viongozi as if umeagizwa mbona hao viongozi hawakukemei kuwasemea???!!!!! Katiba inasemaje juu ya viongozi kushutumiwa na.kukaa kimya wao instead watokee watu binafsi kuwajibia!!!!!?????? Halafu unajiita mwanachama wa kawaida...hebu tulizana ufanye mambo kwa logic kuliko kuongozwa na huo unaouita ujasiri!!!!!!!

Mambo yanabadilika mkuu hayawezi kuwa yale yale kwa kigezo cha vikao halali na katiba, m4c imekuja na.imevikuta vikao na katiba,sasa matokeo yake ni pamoja na muamko wa wanachama kuongezeka na ndio hii inayotokea,yawezekama hamkujua au mlilisahau hili jambo!!!!!!

Unaponunua kisu kipya kikali na vidole vya mkataji pia vinaingia hatarini!!!!!
 
Mkuu Ben, hivyo vikao unavyosema ni vikao gani? Kama mnadiriki kumtwanga ngumi ndani ya kikao, je kwa kusema ukweli si itakuwa balaa kwake? Kama Naibu Katibu Mkuu tu anashindwa kunena yale ya moyoni ndani ya hivyo unavyoita vikao halali kwa kuhofia Majungu ya Mbowe na Dr Slaa, je hawa wengine ambao mnawaita ni sisimizi?
 
ahahaha, sasa kwanini nyinyi CCM hamfurahii hayo masongesonge yanayotokea CHADEMA?
Kila mpenda amani na demokrasia hawezi kufurahia yanayoendelea ndani ya CHADEMA. Tunaelekea kubaya sana kwani kila anayeamua kusema ya ukweli anaishia kipigo, kifo au kufukuzwa ndani ya chama. Hawa watu hawafai kuendesha hata kitongoji
 
Walimu wako walipata shida sana

Hoja ninazojibu hapa ninajibu kwa uelewa wangu na tangu nimejiunga JF mwaka 2007 nimekua nikifanya hivyo.Unataka wanikemee kwa lipi?Kuipigania nchi yangu kwa hoja?Kukitetea na kukilinda chama changu ambao ni wajibu wa msingi kwa mwanachama kikatiba?

Unaongelea kubadili katiba?Hili limekujaje hapa?Huwezi hata kujieleza
 
Mkuu, nimetafuta kitufe cha Like sijakiona. Hakina unastahili like yangu na umeongea jambo la maana sana. Yaani siku hizi Ben Saanane ndo amekuwa msemaji wa CHADEMA! Na haya anayojibu yamepitia vikao halali vya chama? Je haya ayasemayo Ben Saanane hayapingani na katiba ya chama?
 
sasa si msubiri 2015 kwenye sanduku la kura? nawahurumia sana maana CHADEMA haitokufa, na kama mnaita ni SACCOS basi ni SACCOS yenye nguvu kuliko zote,
 
Mkuu Ben, hivyo vikao unavyosema ni vikao gani? Kama mnadiriki kumtwanga ngumi ndani ya kikao, je kwa kusema ukweli si itakuwa balaa kwake? Kama Naibu Katibu Mkuu tu anashindwa kunena yale ya moyoni ndani ya hivyo unavyoita vikao halali kwa kuhofia Majungu ya Mbowe na Dr Slaa, je hawa wengine ambao mnawaita ni sisimizi?

Umejuaje kama mtu anashindwa kunena ya moyoni.Leta ushahidi hapa.Acha umbeya maana JF ni facts tu zinazohitajika
 
Walimu wako walipata shida sana

Hoja ninazojibu hapa ninajibu kwa uelewa wangu na tangu nimejiunga JF mwaka 2007 nimekua nikifanya hivyo.Unataka wanikemee kwa lipi?Kuipigania nchi yangu kwa hoja?Kukitetea na kukilinda chama changu ambao ni wajibu wa msingi kwa mwanachama kikatiba?

Unaongelea kubadili katiba?Hili limekujaje hapa?Huwezi hata kujieleza
Wewe hupiganii taifa lako kwa namna yoyote ile bali upo humu kulinda mkate wako hasa baada ya kuchukua nafasi ya Ludovick. Pia hupiganii chama chako bali unapigania kakikundi kadogo ka viongozi wa juu ambao kwa namna moja au nyingine una nasaba nao au unanufaika kutokana na wao kuwa viongozi
 
Mkuu, nimetafuta kitufe cha Like sijakiona. Hakina unastahili like yangu na umeongea jambo la maana sana. Yaani siku hizi Ben Saanane ndo amekuwa msemaji wa CHADEMA! Na haya anayojibu yamepitia vikao halali vya chama? Je haya ayasemayo Ben Saanane hayapingani na katiba ya chama?

Ni kifungu Kipi nilichokiuka kikatiba?Mbona tangu nimekua JF hujawahi kuuliza kama mimi ni msemaji wa CHADEMA?Acheni woga.I'm here to stay.Siendi popote na nitaendeleza mapambano hata kama hamtaki
 
Back
Top Bottom