Mkuu, tatizo si kuwa wewe ni mwana Chadema, Mwana CUF au mwana CCM au wa chama kingine chochote kile. Kiinachotakiwa ni kupingana kwa hoja, na si kutumia matusi na kejeli. Mimi naamini kuwa hakuna chama au serikali isiyopingwa duniani.
Sasa sisi wengine tusiokuwa na vyama, mnatuogopesha na siasa zenu za visasi. Mi natarajia watu washushe nondo za uhakika na waeleze mazuri ya vyama vyao, na ikiwezekana waielekeze serikali nini cha kufanya, pale linapotokea tatizo na si kuleta matusi....! Tanzania ni yetu sote, sasa msituhatarishie amani yetu.
Mtakapoanza kuwatukana kuwa wanachama wa chama fulani i.e CHADEMA/CUF/CCM kuwa ni wajinga au kuwaita wapumbavu, unaye mtukana hapa kama si nduguyo ni nani!?
Mimi binafsi nina ndugu kwenye vyama vyote hivyo, na tunaheshimiana, na wakati mwingine wananishawishi kujiunga na vyama vyao, lakini kwa bahati ghafi mimi si mpenzi wa vyama vyote hivyo, nipo neutral na ninaheshimu mapenzi ya kila mmoja.
Mkuu kwanza wengi hana hiyo neutral! hawaamini hilo!
Pili nimesema sana hata kutuma post kwa mods kusema kuwa
CREDIBILITY YA JF HIVI SASA IME-SLUMP DOWN kwa kasi ya ajabu, na si ajabu kuwa wahuni wameisabottage na wengi wanajifanya chadema, wanachojua ni matusi tu.
Chadema si chama cha matusi wala ushabiki wa usio na maana! kikubwa mchadema mmoja akitukana mwingine ana-support bila kujali kwa kufanya vile ina repel watu kujiunga na chadema!!
Mpaka viongozi wa chadema members wa humu wengi ni ziro tu, maana kwa nafasi zao wangetoa onyo chadema si chama cha matusi!!
Kibaya si hadhi ya chadema, la! wanatumia uwanja wa JF, uwanja uliotukuka wenye hadhi na historia ya kutukuka!!!
Kama ambavyo standard ya elimu imeshuka kwa shule za kata
Kama ambavyo hadhi ya elimu mlimani ilivyoshuka wa kuongeza wanafunzi bila infrastructure
Kama ambavyo uhalisia wa maziwa upotea kwa kuongeza maji
ndivyo ilivyo JF, hata kama mods na founders watajisifu kwa kuongeza watu ili kupata ufadhili wa hapa na pale , lakini ukweli unabaki palepale this is not JF we used to have here!!!
Balantanda ametoa list ndogo sana ya watu tuliowapoteza, humu yamebaki matangazo ya chadema na ccm na si uwanja wa kufikiri na kupose challenge na kuzijibu!! leo ukitoa topic kinyume na matakwa ya wengi utatukanwa mpaka uone rangi zote!!!
Personally naona bora niseme ukweli nisiondoke kwani hata nikiondoka JF itakuwepo! lakini kama nasema ukweli na we have tangible proof why not change???
majibu ya siku hizi humu ni crap, umetumwa, ......n.k this is absurd!
wengi wa waliojiunga kuanzia may 2010 mpaka February 2011 ni stubborn!!!! wachache sana wenye busara zao!
Kuna siku nilianzisha topic kama hii nikasema tulikuwa tunalazimika ukasome kitu kwanza ndio ujibu hoja......waliotukana walitukana kwa kuona kama vile nina jivuna au ninadharau wageni wa JF , but I was right.