bwana wenger, ni kwamba tunaposema Chenge , Lowasa, RA, Karamagi, nk kua ni mafisadi tunakua na malengo mawili.kwahio na wale wanao toa tuhuma kwa mafisadi hawana haja ya kuwachukulia hatua kwa vile siasa haiko kiivyo sana? mie naona tuhuma za mbowe kufuja mil 35 ni nzito sana ukiangalia wananchi wengi wana moyo na chadema sasa kupatikana tuhuma kama hizi inatufanya tuone mambo ni yale yale kote kote.
Nawaonea huruma vijana wenzangu. Kuanza Siasa bila tabia njema ni aibu kubwa. Sasa ikigundulika hakuna Ufisadi hao vijana waliko kimbilia wataaibika na hawataaminika hata kidogo. Hata huko walikokwenda watakutana na hayo hayo.
Pili kuwa signatory haina maana ya kuwa Mwizi. Basi tuombe wakurugenzi wote wasiwe masignatory. mbona maofisini masignatory ni hao watoa majukumu mbona hatuogopi kama ni wezi.
Yuko tayari kuingia jela kwa kosa gani? Hebu nielimishe hapa.Unapoona umedhalilishwa huwa wanaenda mahakamani na huko ukishinda ,unaweza mwachia mtuhumiwa na wananchi kukuelewa, ama kuamulu mahakama itende unavyotaka.
Sasa Juju kwa kutambua hilo kawaambieni wzi ya kuwa, kama tuhuma ni za uongo basi mwende mahakamani kwa kuruhusu kwanza NGAG ikague mahesabu ,na mkishinda basi jamaa yuko radhi kuingia jela. simple and clear
kama tuhuma za uongo wapelekeni mahakamani basi kwani wanawachafulia sana.kila siku hapa tunasema mafisadi wanaotajwa kama tuhuma ni za uongo waende mahakamani sasa leo swala liko kwenu chadema onyesheni mfano kwa kumpeleka huyu kijana mahakamani kwa kutoa tuhuma za uongo kuhusu ufujaji wa pesa ndani ya chama chenu,
tumechoka watukutupiana maneno kila siku kama swala uongo mnaweza kumshitaki na hapo mwenye nguvu ya ushaidi ndio atapona.lakini hayo mambo yakutupiana maandishi na maneno kila siku hayatupeleki popote.
Yuko tayari kuingia jela kwa kosa gani? Hebu nielimishe hapa.
Tangu lini kusema uwongo limekuwa kosa la jinai? Mnawadanganya akina nani?kusema uongo kama upo, udhalilishaji kama kweli aliyosema si sahihi.
Mfano anapokusia wabunge wanawake wanavyofanywa.
Wanabodi,
Madai haya ni mazito sana kiasi kwamba yanaweza kukichafua chama vibaya sana. Ni tuhuma ambazo hazina tofauti na zile za kesi nyingi hapa nchini zinazohusu Ufisadi ikiwa ni pamoja na Matumizi mabaya ya madaraka - Ufisadi una tafsiri kubwa zaidi ya wizi wa fedha za EPA.
Mimi sioni tatizo hapa kufikia kuanza kumshambulia mtu wakati hatuna majibu ya tuhuma zilizotolewa....Kwa wanachama wa Chadema, Ukaguzi ufanyike tutakuwa tumemaliza ubishi!..Na kama kuna mtu mwenye taarifa nzuri kuhusiana na mahesabu ya chama ayaweke wazi kinyume cha madai ya Danda, Siku zote ukweli utajitenga!
Kwa mujibu wa taarifa hii inaonyesha wazi kwamba danda kafukuzwa kazi kutokana na madai yake ambayo yananipa wasiwasi kubwa zaidi kutokana na kauli za Zitto hapa JF kwamba kuna matumizi mabaya ya fedha za ruzuku. Na picha nzima inaonyesha wazi kwamba yapo makundi mawili ndani ya chama Chadema na yametokana na matumizi ya hizi ruzuku.
Haiwezekani kuwa kila anayeondoka Chadema swala liwe hili hili la matumizi mabaya ya ruzuku, hata kama Mbowe hutoa fedha zake mfukoni na kukikopesha chama..Bado haipotoshi madai ya matumizi mabaya ya fedha...Swala sii fedha ngapi zimechangishwa ama zimeibiwa isipokuwa ni matdai yote yanahusu matumizi mabaya ya RUZUKU.. Hizi ni fedha za walipa kodi wala sii za CCM ama Chadema ni fedha za wananchi ambazo zinatakiwa vyombo hivi kuwakilisha matumizi yake ktk vyombo husika kama Wizara, mashirika na Taasisi nyinginezo..Tunabishana ktk jambo ambalo lipo wazi kabisa...
Mimi sina wasiwasi na Mbowe najua fika kwamba amekisaidia sana chama Chadema kwa fedha yake mwenyewe lakini ikiwa kuna madai yasiyokuwa na msingi kama haya ni bora kuondoa nuksi hii kwani Chama kilipoamua kuwaondoka wahusika ktk madaraka walikuwa wakijua wazi ni kitu gani kinachofuatia. Na kuwatukana wahusika kwa maneno mazito na machafu haiwezi kusaidia kitu kabisa kwani hata mimi nimeanza kuwa namashaka makubwa na Uongozi ndani ya Chama hasa pale wanaposhindwa kutoa majibu yanayohusiana na madai isipokuwa wanakwenda Personal.. Swali linabakia palepale - Je, ni kweli, fedha za ruzuku na michango inatumiwa vibaya na huyu msaini aitwaye KOMU ambaye inadaiwa yuko karibu na Mbowe hivyo hupewa kinga inapofikia kuwakilisha mahesabu?..
Nitashangaa sana kuona viongozi wa Chadema na wanachama wake wataendelea kuyabeba madai kama haya kwa majibizano..Hawa wote walikuwa ama ni wanachama wa Chadema, na inasemekana wote wamefukuzwa uongozi kutokana na madaia yao kuhusiana na Matumizxi mabaya ya ruzuku..Chadema onyesheni mfano wa kuigwa na vyama vingine vyote iwe CCM, TLP, NCCR - Mageuzi.. Vyama hivi vyote vinatakiwa kukaguliwa mahesabu yao kwani ndio utaratibu unaoheshimika ktk ngazi zote za Uchumi..
Tangu lini kusema uwongo limekuwa kosa la jinai? Mnawadanganya akina nani?
Nani kasema kosa jinai, kwanza ndo nalisikia kwako.Acha upotoshaji kubali chalenges
Panapofuka moshi ni dalili kwamba kuna moto
Afichaye uginjwa/maradhi kifo kitam-umbua
Kelele zote hizi bado hamjui tatizo lenu....ama kweli sikio la kufa halisikii dawa...