CHADEMA mtatoka na ajenda gani baada ya kurudi kwa mikutano ya hadhara ya siasa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,638
46,279
Kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara ya siasa ni fursa nyingine inayofungua milango ya kisiasa kujenga na kumarisha demokrasia ya Tanzania wapinzani wanapaswa kuchanga karata zao vizuri katika agenda watakazotoka nazo.

Japo mlikuwa wahanga wakubwa wa utawala wake mnatakiwa kuachana na kumzungumzia au kulitaja jina la Magufuli kabisa katika majukwaa ya hadhara ya kisiasa. Magufuli haipaswi kuwa mojawapo ya ajenda kwa sababu hayagusi maisha ya raia tena kwa namna yoyote kwa sasa, hata hivyo mnaweza kuwazungumzia watu wake aina ya kina Mnyeti, Gelasius Byakanwa, Makonda, Sabaya, Muro n.k

Ajenda kuu za upinzani zinatakiwa kuwa

1. Hali ya maisha kiuchumi
2. Upatikanaji wa huduma za kijamii
3. Miondombinu
4. Hali ya kidemokrasia
5. Tume huru ya uchaguzi
6. Katiba mpya
7. Mikopo ya nchi
8. Mazingira ya kufanya biashara
9. Matumizi ya serikali
10. Uvunaji na uhifadhi wa maliasili zetu.
 
Agenda mbona zipo tu mfano kiswahili kiwe lugha ya kufundishia kama siyo basi mfumo wa elimu ubadilike haraka sana maana hatuwezi kulazimisha walimunwa sekondari wawafundishe watoto kingereza wakati elimu ya msingi janja janja ilikua nyingi
 
Mimi kama mjasiliamali wa kuprinti tisheti nimeanza kupokea order za kuprint tisheti zenye picha ya hayati Magufuli zitazovaliwa siku ya mkutano mkubwa wa Chadema pale jijini Mwanza.

Mtu mmoja aliyenipa order aliuliza.

Tisheti za JPM zinauzwa wapi, ndio za kuvaa nyakati hizi za mikutano sasa, bila kujali upo mkutano gani, no matter what kuna ujumbe utapenya, tena wenye nguvu, usiobezeka..

Njooni Mwanza tuwalie hela zenu na mtueleze kwa nini mlishangilia kifo cha Magufuli, na mtueleze pia kwa nini watoto wa Mbowe ,Lisu na Lema ni raia wa Marekani.

Niko hapa naprint za kutosha
 
Pengine ndani ya CHADEMA hakuna mwenye kuona hili lakini acha nitoe ushauri kuisaidia.

Mnaenda kwenye marathon ambayo kikawaida ni mbio ndefu na mbio ndefu ina kanuni yake muhimu kwamba mchezaji hatakiwi kuanza kwa spidi kali kumsaidia kuvuta hewa mapafuni na kubalance pumzi.

Naona CHADEMA wamesahau kanuni hii na nawakumbusha THIS IS MARATHON, mtachoka haraka kabla ya mbio kufika nusu

Msije kusema kuna tuvituvitu CCM imefanya mshindwe mbio hizo.
 
Mimi kama mjasiliamali wa kuprinti tisheti nimeanza kupokea order za kuprint tisheti zenye picha ya hayati Magufuli zitazovaliwa siku ya mkutano mkubwa wa Chadema pale jijini Mwanza.

Mtu mmoja aliyenipa order aliuliza.....
Tisheti za JPM zinauzwa wapi, ndio za kuvaa nyakati hizi za mikutano sasa, bila kujali upo mkutano gani, no matter what kuna ujumbe utapenya... tena wenye nguvu... usiobezeka..

Njooni Mwanza tuwalie hela zenu na mtueleze kwa nini mlishangilia kifo cha Magufuli, na mtueleze pia kwa nini watoto wa Mbowe ,Lisu na Lema ni raia wa Marekani.

Niko hapa naprint za kutosh
 
Back
Top Bottom