Kule kuanza kuomba MBINU leo hii wakati awamu hii ya nne inakaribia kumaliza safari yake hakika ni ajabu na vichekesho kwa watu wenye akili. Yaani ni sawa na kusema umefunga safari kutoka stendi Ubungo hadi mtu unafika mjini Tanga kisha ndio unaanza kuuliza watu barabarani wkuelekeze jinsi gani ya kufika Nyalugusu - CCM guys you are NOT serious; stop taking us for a ride!!!!!!!!!!!
Kwa nini mmanze kuomba blanketi alfajiri yote hii wakati hata nyinyi mnajua kwamba tayari kumekucha na hata sauti ya VINDEGE (WaTanzania Walalahoi) tayari vinatawala kila mahali??
Mambo ya kupewa nyinyi ulichokiita STRATEGY ya kutatua tatizo la umeme ni sharti kwanza mkubali kwamba mmeshindwa kuongoza nchi, pili mkapishe katika hizo ofisi mbalimbali mlizojikimbilia kunyakua hat bila kujua mnaenda kufanya mfikapo mle, hapo ndipo mtakapojua kwamba wapo Watanzania wengine pia huku nje ambao wanao uwezo mkubwa sana kutatua tatizo la umeme nchini.
Kimantiki zaidi, siku zote kabla mtu haujaanza kutatua tatizo lolote kwanza ni sharti ukalichunguze tatizo lenyewe na kutafuta kujua kwamba ni kivipi Watanzania tulifika hapa tulipo kama nchi kwenye umeme wa kubahatisha ambalo hivi sasa limekua sugu. Hakika jibu la swali hili kamwe haliwezi kupatikana bila kupembua nini walichokifanyia taifa CCM, Rostam Aziz na Edward Lowassa mpaka tukafika hapo.
Maswali ya kinadharia (Hypothetical questions) bila shaka yatakua pamoja na haya:
(1) je tatizo la umeme nchini ulianzaje? Pengine lilisababishwa na mtu, pengine na kikundi, pengine na hali tu ya hewa.
(2) Je, ni hatua zipi zilizowahi kuchukuliwa kutafuta ufumbuzi?
(3) Je, hatua hizo zilizochukuliwa kweli ndizo zilizokua bora zaidi kuwahi kufikiriwa katika hali kama hiyo inayotukumba?
(4) Je, wataalam wenye taaluma zao nchini walihushishwa kwa kiasi gani katika swala zima tangu mwanzo (na wataalam hao walipatikanaje)?
(5) Je, kuna uwezekano wowote kwamba 'Executive Intervention' katika tatizo hili liliweza kuleta ushawishi wowote na kuumba sura mpya ya tatizo tulio nayo (hilo lilitokeaje na huo mguso ulikua ni wa manufaa au adha ndani mwake)?
(6) Je, kuna uwezekano wowote kwamba fedha za Watanzania huenda zilitumika nje ya sheria na taratibu zozote zinazotambulika na kukubalika?
.... etc
Mara baada ya kujiuliza MASWALI MAGUMU yote juu ya changamoto la umeme hapo ndipo tunapoweza sasa kuanza kujiuliza kwamba katika yote hayo sisi kama Taifa tuliangukia wapi na sasa kitu gani kifanyike, lini, wapi na kwa mtindo upi, kwa kutumia rasilmali zipi zitakazopatikana kutoka wapi na kwa TAHADHARI zipi ili tuweze kuwa na hali njema ki-Umeme kuliko tulivyokua hapo jana LAKINI KWA GHARAMA STAHIKI, VYOMBO STAHIKI, na kwa kutumia watu stahiki, mbinu stahiki, kwa wakati stahiki ili taifa letu tuweze kupata TIJA STAHIKI kwa kila Mtanzania.
Hivyo nasema, STOP JUMPING THE GUNS if at all you would still be interested to be lined up as one of the Great Thinkers on board, a hoard of homework MUST be done and NOT just giving such a casual treatment to a matter of GRAVE NATIONAL CONCERN like this of Umeme. If you agree with me on a number of propositions above then let me know.
(3) Je hali kama hii iliwahi kutokea huko nyuma katika kipindi cha awamu nyinginezo? fedha kw
Naomba mtupatie clear strategy ya namna mtakavyotatua tatizo la umeme.
we need to see your strategic plan na solution
ONYO: Enough with blame games hivyo naomba we leave CCM na akina EL na Rotam out of this. Naombeni Clear plan yenu ambayo ni workable and not some soundbite ambazo tumezizowea humu ya kutaka ku score political points