CHADEMA mtatatua vipi tatizo la umeme? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA mtatatua vipi tatizo la umeme?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BondJamesBond, Jul 27, 2011.

 1. B

  BondJamesBond Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba mtupatie clear strategy ya namna mtakavyotatua tatizo la umeme.

  we need to see your strategic plan na solution

  ONYO: Enough with blame games hivyo naomba we leave CCM na akina EL na Rotam out of this. Naombeni Clear plan yenu ambayo ni workable and not some soundbite ambazo tumezizowea humu ya kutaka ku score political points
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwani Magamba wamekili kushidwa??

  Kama wameshidwa basi wao waombe msaada from CDM maana siku zote wanaega
   
 3. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Soma bajeti mbadala ya nishati na madini iliyosomwa bungeni na John mnyika imeeleza kila kitu.
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Serikali iliyoshindwa kazi yake ipishe wanaoweza kazi.CDM haipo kuifundisha kazi CCM.
  Ila kama CCM imeshindwa ni heri ijitokeze yenyewe kuomba msaada sio itume watu JF kupima upepo.
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  BongJames, soma Ilani ya uchaguzi ya CDM 2010, vilevile fanya homework vizuri kwa kupitia pia bajeti ya wizara kivuli husika.
   
 6. A

  Alakara Armamasitai Verified User

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mimi nashangaa jamaa kuomc strategy wakati kikwete anahoji na mtangazaji wa bbc aliibeza strategy za mnyika baada ya kuwambiya kwanini wasitumie ushauri wa waziri kivuli wa upinzani akaibeza na kusema naomba unisikilize mimi achana na hao mimi nakuwambiya shida ni ukame alibaki kuliya ukame hata pale alipoambiwa ushauri wa john unafaa alipimga vikali sasa kama ccm wataka chadema walete umeme wa uhakika waachie serikali sio kulialia ukame kama mr.president
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Na kule jangwani wangekaa wanalia lia ukame sidhani kama Dubai kungekuwa na bustani nzuri za kupendeza kiasi kile.
  Akili ya JK na chama chake imeishia hapo, wao kwao ikikosekana mvua ndo mwisho wa maisha. poor JK
   
 8. A

  Awo JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Wapi naweza kupata hiyo hotuba ya bajeti mbadala ya CDM?
   
 9. Nditu

  Nditu Member

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ovyo! Maswali mengine Bwana utafikiri yanaulizwa na mgonjwa anaye recover toka kwenye kale kadawa ka usingizi kanakoitwa Ketamine! Kwa kawaida mgonjwa aliyefanyiwa mapasuaji kwa kupewa usingizi wa dawa hii anaporudia fahamu huweweseka nakusemasema maneno ya namna hii. Hebu tuambieni wana magamba (Makuwadi wa Nape) mnataka viongozi wa CHADEMA wajibu ili muwapige fix watz kwamba ulikuwa nimpango wenu kama mlivyofanya katika kila mliloliiga toka CHADEMA? Mimi siwakilishi uongozi wa CHADEMA lakini ni rahisi tu, kwa kuanzia chama makini cha
  CHADEMA kitakomesha ulipwaji wa fedha za rushwa kwa makampuni mnayoyasingizia kumbe fedha zenyewe mnagawana hapahapa. Bilioni 6 wanazolipwa IPPTL kila mwezi tu zinatosha kununua Jenereta za nguvu kuzalisha umeme kwa ajili ya gridi ya taifa. Vibaka walowekeza kwa mkataba mliokula rushwa wa kuchimba gesi watalipishwa kodi na kuelekezwa kuiuza gesi kwa fedha za hapahapa nyumbani na si kama sasa hata serikali hii ya vibaka inanunua kwa fedha za kigeni wanapoitaka gesi hiyo! Mipango endelevu ya kuzalisha umeme iliyosimamishwa kwa ushawishi wa vibaka wenzenu wa IPPTL, Aggrecco, Songas n.k. itafufuliwa na utakuwa ndiyo mwisho wa shida hii ya kutengenezwa ya umeme.
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Huyu mleta thread katumwa, na ushauri wangu hapa ni kumfumbua macho hapahapa ili akigeuka nyuma ageuke jiwe la chumvi! Ni bora tumwelimishe ili ujinga umtoke na asirudie tena. Atambue kuwa atakuwa mpumbavu sana kama ataipigia kura sisiem alafu aje aulizie mipango ya maendeleo cdm. Huo ni upuuzi kabisa!
   
 11. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,402
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  kwani hao uliowataja wamesema wameshindwa..?? na kwa nini unakimbilia kuita ..BALME GAMES... wakati ni ukweli..?? Wao ndo wametufikisha hapa. TATIZO LA MAGAMBA KUUKUBALI UKWELI KWAO NI ISHU KUBWA................ WAKO TAYARI WANYONGWE LAKINI HAWATAKI KUAMBIWA UKWELI................ NA NDIYO MAANA HATA HAO WANAOWAHITA MAGAMBA NAO WANAKANA KWAMBA WAO NI MAGAMBA................. kuna mmoja alisema yeye hajui kama naye ni gamba.......
   
 12. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,402
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Na akigeuka jiwe la chumvi sisi TUNAMLAMBA au TUTAMTIA kwenye mboga au wali TUMLE huko
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Mpaka saa hizi hakuna hata mmoja aliyekuja na njia kivuli?
   
 14. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,153
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Usilete hoja za kijinga! Mnahongwa kofia na tisheti mkitegemea chadema kushika dola! kwanza mpeni dola ndio muulize swali kama hili na sio kukurupuka kama umefumaniwa
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kule kuanza kuomba MBINU leo hii wakati awamu hii ya nne inakaribia kumaliza safari yake hakika ni ajabu na vichekesho kwa watu wenye akili. Yaani ni sawa na kusema umefunga safari kutoka stendi Ubungo hadi mtu unafika mjini Tanga kisha ndio unaanza kuuliza watu barabarani wkuelekeze jinsi gani ya kufika Nyalugusu - CCM guys you are NOT serious; stop taking us for a ride!!!!!!!!!!!

  Kwa nini mmanze kuomba blanketi alfajiri yote hii wakati hata nyinyi mnajua kwamba tayari kumekucha na hata sauti ya VINDEGE (WaTanzania Walalahoi) tayari vinatawala kila mahali??

  Mambo ya kupewa nyinyi ulichokiita STRATEGY ya kutatua tatizo la umeme ni sharti kwanza mkubali kwamba mmeshindwa kuongoza nchi, pili mkapishe katika hizo ofisi mbalimbali mlizojikimbilia kunyakua hat bila kujua mnaenda kufanya mfikapo mle, hapo ndipo mtakapojua kwamba wapo Watanzania wengine pia huku nje ambao wanao uwezo mkubwa sana kutatua tatizo la umeme nchini.

  Kimantiki zaidi, siku zote kabla mtu haujaanza kutatua tatizo lolote kwanza ni sharti ukalichunguze tatizo lenyewe na kutafuta kujua kwamba ni kivipi Watanzania tulifika hapa tulipo kama nchi kwenye umeme wa kubahatisha ambalo hivi sasa limekua sugu. Hakika jibu la swali hili kamwe haliwezi kupatikana bila kupembua nini walichokifanyia taifa CCM, Rostam Aziz na Edward Lowassa mpaka tukafika hapo.

  Maswali ya kinadharia (Hypothetical questions) bila shaka yatakua pamoja na haya:

  (1) je tatizo la umeme nchini ulianzaje? Pengine lilisababishwa na mtu, pengine na kikundi, pengine na hali tu ya hewa.
  (2) Je, ni hatua zipi zilizowahi kuchukuliwa kutafuta ufumbuzi?

  (3) Je, hatua hizo zilizochukuliwa kweli ndizo zilizokua bora zaidi kuwahi kufikiriwa katika hali kama hiyo inayotukumba?
  (4) Je, wataalam wenye taaluma zao nchini walihushishwa kwa kiasi gani katika swala zima tangu mwanzo (na wataalam hao walipatikanaje)?

  (5) Je, kuna uwezekano wowote kwamba 'Executive Intervention' katika tatizo hili liliweza kuleta ushawishi wowote na kuumba sura mpya ya tatizo tulio nayo (hilo lilitokeaje na huo mguso ulikua ni wa manufaa au adha ndani mwake)?
  (6) Je, kuna uwezekano wowote kwamba fedha za Watanzania huenda zilitumika nje ya sheria na taratibu zozote zinazotambulika na kukubalika?
  .... etc

  Mara baada ya kujiuliza MASWALI MAGUMU yote juu ya changamoto la umeme hapo ndipo tunapoweza sasa kuanza kujiuliza kwamba katika yote hayo sisi kama Taifa tuliangukia wapi na sasa kitu gani kifanyike, lini, wapi na kwa mtindo upi, kwa kutumia rasilmali zipi zitakazopatikana kutoka wapi na kwa TAHADHARI zipi ili tuweze kuwa na hali njema ki-Umeme kuliko tulivyokua hapo jana LAKINI KWA GHARAMA STAHIKI, VYOMBO STAHIKI, na kwa kutumia watu stahiki, mbinu stahiki, kwa wakati stahiki ili taifa letu tuweze kupata TIJA STAHIKI kwa kila Mtanzania.

  Hivyo nasema, STOP JUMPING THE GUNS if at all you would still be interested to be lined up as one of the Great Thinkers on board, a hoard of homework MUST be done and NOT just giving such a casual treatment to a matter of GRAVE NATIONAL CONCERN like this of Umeme. If you agree with me on a number of propositions above then let me know.
  (3) Je hali kama hii iliwahi kutokea huko nyuma katika kipindi cha awamu nyinginezo? fedha kw

   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Shukran umejibu vizuri... Kumbe kuna watu hawafuatilii vitu kabisa...
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Watatuaje wakati wako nje ya serikali na wewe??

  hebu tumia hicho kidogo ulichonacho kichwani kusalimiana na watu, haya mengine huyawezi
   
 18. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jinsi ulivyolitoa swali lako inaonesha wazi kuwa magamba wamekiri kuwa tatizo halina solution na hawaamini kama kuna watakaoweza kulitatua. Kazi ipo!
   
 19. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Wakati wa kupiga kura ulipigia magamba ukaingia nao mkataba wa kukuongoza wala haukuwakumbuka CDM sasa mambo yamekufika pabaya ndo unawakumbuka CDM,kwani uliowachagua wako wapi,nenda magogoni uwaulize jamani vipi tena?mkiambiwa wala hamsikii,mkioneshwa hamuoni,mara hii mtakoma na mtajuta,njaa ufundisha kula naamini 2015 utajua nini maana ya CDM,...bullshit!!
   
 20. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimejaribu sana lkn nimeshindwa kukuelewa, unatoa onyo hapa wakati umejitapikia, umejiharishia na unahitaji msaada!! Sijawahi kuona...
   
Loading...