Chadema msiba wa Salome hawahusu??

Mushobozi

JF-Expert Member
Aug 20, 2007
543
225
ilikuwa kali!!!!!!!!!!!!!

kura za maoni zinajieleza zenyewe........kwi! kwi! kwi!!!!!!!!
 

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
0
tatizo mtu wa pwani, mgumu kuelewa,mwepesi kusahau. Kijana kabla ujaongea jaribu kufanya utafiti, katika source mbalimbali za habari,siyo unakurupuka tu kama Karamaghi. Unataka wanaotoa rambirambi wabandikwe kwenye mabango? Mbona raia masikini wakifa hatusikii unasema? au mzee ni wa kizazi cha karamaghi?
 

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,172
2,000
tatizo mtu wa pwani, mgumu kuelewa,mwepesi kusahau. Kijana kabla ujaongea jaribu kufanya utafiti, katika source mbalimbali za habari,siyo unakurupuka tu kama Karamaghi. Unataka wanaotoa rambirambi wabandikwe kwenye mabango? Mbona raia masikini wakifa hatusikii unasema? au mzee ni wa kizazi cha karamaghi?

tuonyeshe wapi chadema imetuma salam za rambi rambi kama chama?

acha mapenzi ya kibubusa
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,876
2,000
Haha mliosema juu ya Mbowe sasa leteni habari mpya. Mbowe alipanda ndege na kuwahi mazishi . Mbowe kaacha shule yake na kuja kuhudhuria mazishi kama Kiongozi na Mtanzania .Ila nimeshangaa sana mazishi yalitawaliwa na U CCM . Kumbe nilidhani Marehemu alikuwa ni kiongozi wa Tanzania na Watanzania kumbe CCM ilikuwa ya kwanza kwa wana CCM ?

Ushahidi wa Mbowe kuwepo kwenye mazishi ni huu hapa .

Mamia wamzika Salome Mbatia kijijini Mioshi
*Kikwete afananisha msiba na wa baba yake
*Makinda asema Taifa limepoteza mwanaharakati


Na Daniel Mjema na Ally Sonda, Moshi


SAFARI ya mwisho duniani ya Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia ilihitimishwa jana katika makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mbokomu na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji.


Rais Jakaya Kikwete aliongoza waombolezaji na akaueleza umma kuwa, taarifa za kifo cha Mbatia zilimkumbusha siku alipopata taarifa za kifo cha baba yake mzazi, wakati alipotua tu katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Saaam.


“Niliporejea kutoka katika safari yangu ya Roma na Italia ndipo Makamu wa Rais ananiambia; unajua mheshimiwa Rais...lakini anababaika hivi na baadaye ndio akaniambia kuwa Salome amepata ajali na amefariki dunia,” alisema.


Kwa mujibu wa Rais Kikwete, taarifa hiyo ilimkumbusha Septemba 08, 1998 alipokuwa akirejea nchini akitokea nje ya nchi na alipotua katika uwanja wa ndege akataarifiwa kuwa baba yake mzazi amefariki dunia.


“Haya si mapokezi mazuri sana unaporejea nyumbani," alisema Rais Kikwete na kumuelezea marehemu Mbatia kama kiongozi aliyeweka mbele maslahi ya nchi na ndio maana hata hakusita kumteua kuwa Naibu Waziri.


Rais alisema marehemu alikuwa ni mmoja kati ya watu ambao akiwa na jambo analoliamini au akipewa kazi yoyote aliifanya kwa moyo safi na kwamba alikuwa ni mtu mwenye adabu mithili ya mtoto aliyelelewa vizuri.


“Taifa limepoteza mwananchi wake mzalendo lakini familia imepoteza zaidi na imepata pigo ambalo halitazibika,” alisema Rais Kikwete ambaye alifuatana pia na mkewe, Mama Salma Kikwete katika mazishi hayo.


Akizungumza kwa niaba ya Bunge la Tanzania, Naibu Spika, Anna Makinda alimwelezea marehemu kama mmoja wa wanaharakati wa usawa na haki za kijinsia na mchapakazi hodari ambaye taifa limewahi kupata.


“Alikuwa anajitoa kwa hali na mali katika kusimamia maslahi ya nchi, alikuwa mtu mwenye msaada mkubwa kwa kila mtu aliyehitaji msaada wake na alisimamia sana suala la uwakilishi wa wabunge uwe nusu kwa nusu,” alisema.


Kwa mujibu wa Makinda, wabunge wote wametoa rambirambi ya Sh 7,337,000 kwa familia ya marehemu Mbatia ambaye alifariki kwa ajali ya gari mkoani Iringa.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Kapteni Jacka Mwambi alisema CCM imetoa rambirambi ya Sh2.4 milioni wakati Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) taifa umetoa Sh150,000.


Mbali na rambirambi hizo UWT wilaya ya Mvomero ambako marehemu alikuwa ni mlezi ilitoa Sh150,000, UWT mkoa wa Iringa Sh150,000 na UWT katika wilaya zake zote na mikoa imetoa Sh620,000.


Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta, alisema kwa kutambua mchango wa Mbatia, serikali imetoa ubani wa Sh1 milioni wakati mawaziri na manaibu waziri kwa ujumla wao wametoa Sh3 milioni.


Mazishi ya marehemu Mbatia yalifanyika saa 7:45 mchana ambapo Rais Kikwete pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo mawaziri walipata fursa ya kuweka mchanga katika kaburi la Marehemu.


Kaburi lake lilipambwa kwa mashada mbalimbali ya maua na kazi ya kufukia mchanga katika kaburi lake ilifanywa na chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ambao walivalia mavazi rasmi ya chama hicho.


Ibada ya mwisho katika makaburi hayo iliendeshwa na jopo la mapadre wa Katoliki wakiongozwa na Padre Paul Uria na Paroko wa Parokia ya Mbokomu yalipo makaburi hayo, Padre Nicetas Kyara.


Kabla ya kufikishwa eneo la maziko, mwili wa marehemu ulipelekwa kwanza nyumbani kwake eneo la Msaranga saa 3:15 asubuhi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kristu Mfalme.


Katika kanisa hilo, Askofu wa Jimbo la Moshi, Mhashamu Amedeus Msarakie aliendesha ibada maalumu na kumwelezea marehemu kama mmoja wa waumini wakubwa wa kanisa hilo.


Akitoa salamu kwa niaba ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk Erasto Kweka alisema Taifa limepoteza nyota iliyochomoza kwa mwanga mkali.


Dk Kweka alimwelezea marehemu kama mtu aliyewapa moyo na matumaini watu wote walioonyesha juhudi za maendeleo mema na hivyo kumvutia kila mtu kumsikiliza na kupokea ushauri wake.


“Hakutafuta umaarufu kwa maneno yasiyofaa..kama mtendaji na kama Naibu Waziri alizunguka kote nchini, alikoseshwa usingizi na maisha duni aliyokutana nayo Vijijini na mijini,” alisema Dk Kweka.


Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri Mkuu,Edward Lowassa, mawaziri, wabunge na Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhan.


Pia walikuwepo viongozi wa vyama vya upinzani akiwemo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mwenyekiti wa UDP John Cheyo.
Wakati huo huo, Burhani Yakub anaripoti kutoka mjini Tanga kuwa, Mtangazaji wa Radio ya Tanzania Dar es salaam na Televisheni ya Taifa TVT, Eshe Muhidini, aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe Magunga kutokana na kupata ajali wakati akielekea Mjini Moshi kwenye mazishi ya Mbatia amehamishiwa hospitali ya Bombo kwa matibabu zaidi.


Majeruhi huyo alifikishwa katika Hospitalini hapo usiku wa kuamkia jana baada ya hali yake kuwa mbaya na hivyo kuhitajika kufanyiwa uchunguzi wa ndani ya mwili x-Ray, ili kujua athari zilizopatikana.


Mganga Mkuu wa Bombo, Magreth Mhando aliliambia gazeti hili kuwa, Eshe alifikishwa hospitalini hapo saa 5:00 usiku na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Betty Mkwasa.


Alisema baada ya kufikishwa hospitalini hapo, Waganga walimaua kumpeleka kwenye X-Ray haraka ili kujua athari alizopata mwilini kutokana na ajali hiyo na kwamba hadi tunaripoti habari hizi majibu yalikuwa bado hajatolewa.


Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika wodi aliyolazwa ya Clief, Eshe alisema anasikia maumivu makali upande wa kushoto wa mwili wake na kwamba ana wasiwasi kuwa anaweza kuwa amevunjika mbavu.


"Nasikia maumivu kuanzia shingo, mbavu hadi mguu wa kushoto ambako gari iliangukia," alisema kwa taabu Eshe na kuwashukuru Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Suzan Lyimo kwa msaada alioutoa mara baada ajali yao kutokea.


Tuma maoni kwa Mhariri
Habari katika picha na Matangazo
Haki zote zimehifadhiwa na MCL 2006- 2007
 

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,876
2,000
Mtu wa Pwani
Are you na usemalo kwamba Zitto alileta picha za tukio la ajali ?Believe me hata wakati nasema na Zitto he was not able eaven to speak of what was happening on the scene. I think it is time you guys to grow up and stop spinning .

Nimjuavyo Zitto si mpenzi wa hata wa kutembea na camera and he was in a total shock kutokana na tukio lenyewe .
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,179
2,000
Hilo ndio tatizo, hiyo picha nililetewa mimi within few minutes za ajali, na chanzo hakikuwa Zitto. Na zipo nyingine lakini kwa ajili ya kutotukuza mauti zimebakia kwa macho yangu tu. Je, UCCM unakuja mwanzo kuliko Utaifa? jibu ni jepesi NDIYO!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom