Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,187
- 670
sijaona salam za rambi rambi za chama makini juu ya huu msiba kama chama, jee ndio hauwahusu? ndio mafisadi hawastahiki kupewa mkono wa pole?
...Lipumba, Makamba wamlilia
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amemtumia Rais Jakaya Kikwete, salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bibi Salome Mbatia.
Katika salamu hizo alizozituma jana, Profesa Lipumba alisema amepokea
kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Bibi Mbatia, kilichotokea juzi kwa ajali ya gari lake kugongana na lori aina ya Mitsubishi Fuso katika wilaya ya Njombe, mkoani Iringa.
"Nilimfahamu marehemu Mbatia tangu tukiwa wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1973/76. Tangu akiwa mwanafunzi, alikuwa mchapa kazi, mwenye bidii na nia ya kijiendeleza na kushirikiana na wenzake.
"Kama kiongozi mwanamke, alikuwa mfano mzuri kwa wanawake wengine katika nchi yetu. Na kwa kweli Watanzania tulikuwa bado hatujautumia kikamilifu uwezo wa marehemu Salome Mbatia," alisema Profesa Lipumba.
Alisema Watanzania ni waumini wa dini mbali mbali na wao CUF wanaamini kifo ni jambo la lazima kwa kila binadamu.
"Lakini pia Mwenyezi Mungu ametupa uwezo wa kujiendeleza na kuepukana na ajali. Mheshimiwa Rais tumepoteza Watanzania wengi kwa ajali za magari barabarani. Pamoja na kauli za Serikali na jitihada mbali mbali ikiwa ni pamoja na kampeni maalumu, bado ajali ni nyingi mno," alisema.
Alisema ajali nyingi zinasababishwa na kutofuata sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani na kwamba kifo cha Bibi Mbatia na wenzake, hakina budi kutoa changamoto mpya ya mjadala wa kitaifa, kuhusu kuzuia ajali za magari barabarani na kuchukua hatua madhubuti ya kufanya hivyo.
"Tunawapa pole familia ya marehemu Mbatia. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu wakati huu mgumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amin," alisema Profesa Mbatia.
Naye Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, katika salamu zake za rambirambi kwa Rais Kikwete, alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwa Serikali, CCM na jamii kwa ujumla.
"Marehemu atakumbukwa kwa ucheshi, uhodari wa kazi na upendo wake kwa watu...alikuwa amana ya Mwenyezi Mungu, kwa chama na Serikali na sasa Mungu amechukua amana yake," alisema.
Bw. Makamba aliwataka wana CCM, ndugu, jamaa na marafiki na wananchi kwa ujumla, kulitaza tukio hio kuwa ni mapenzi ya Mungu na kutambua kuwa ingawa wengi walimpenda na walikuwa bado wanamhitaji, lakini Mungu alimpenda zaidi.
Marehemu Mbatia pamoja na kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, na Naibu Waziri, aliwahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wa Uchumi na Fedha na mjumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) tangu mwaka 2002 hadi mwaka jana.
Hadi anafariki dunia, alikuwa mjumbe wa NEC na akiwa mgombea wa NEC kundi la wanawake.
Aliwahi pia kuwa Meneja Mkuu wa kampuni ya Biashara Consumers Services Ltd kwa miaka 10, Mwenyekiti wa Bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam na mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Pia aliwahi kuwa mjumbe wa bodi za TBS, Uhuru na Mzalendo, Bahati Nasibu ya Taifa na Privatization Trust.
Wakati huo huo, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM inatarajiwa kukutana leo Dar es Salaam, kwa ajili ya kikao cha siku moja chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete.
Kikao hicho kitajadili taarifa ya hali ya siasa nchini na mapendekezo ya wana CCM wanaoomba uongozi wa CCM mkoa wa Arusha na maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM na ushiriki wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani.
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4313