Wanabodi!!!! Kama ikitokea siku kiongozi yeyote wa CDM akija hapa jamvini na thread za kipumbavu na mipasho Kama hizi za huyu mwimba Taarabu Nnauye Jr basi nitajitoa uanachama CDM siku hiyo hiyo. Huu ni ujinga kwa kiongozi mkubwa Kama Nape kuandika mipasho akajifunze kwa wenzake wakina mnyika, mdee wapo makini sana ni Aibu kwa taifa kuwa na watu Kama wakina Nape, Malugo na Mukama. Ngoja niachie hapa nisije nikaharibu keypad zangu kwa hasira
Wanaodhani na kueneza nimekimbia si sawa, si kweli...SINA MUDA WA KUKESHA NA NYIE, MUNGU ALIUMBA USIKU TUPUMZIKE.....POLENI MLIOKESHA KUSUMBUA VICHWA MTAPOTOSHAJE UKWELI KUWA....mpira magoli si chenga......
Nawashukuru mliotambua na kukiri kuwa "nape kiongozi mkubwa" ...walau akili zimeanza kuwarudia huo ni mwanzo mzuri....! LAKINI KUBWA HAPA PIA NIMEFURAHI UKIRI WENU KUWA MAJIMBO NA KATA ZOTE NI MALI YA CCM, NDO MAANA YA HESABU YENU YA KATA MBILI KUZICHUKUA NA MKAFURAHIA KAMA MAJUHA....MPIGE HESABU HII HATA MWAKA 2014 NA 2015......MUWE NA LUGHA HII HII.....HAKIKA MTAONYESHA UKOMAVU MKUBWA SANA WA KISIASA....
Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Mara, jana uliingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa na wajumbe kurushiana ngumi, viti, mawe na silaha mbalimbali ndani ya ukumbi.
Mapigano hayo makali yaliyochukua takribani dakika 10, yalisababishwa na kilichodaiwa na wafuasi wa mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo kumvamia Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Tarime, Denis Zakaria, na kuanza kumshushia kichapo kwa madai kuwa alikuwa akiwahonga fedha wajumbe wa mkutano huo.
Kufuatia madai hayo, wafuasi hao waliendelea kumzonga Katibu huyo huku wakimueleza kuwa kama amekwenda kwenye uchaguzi huo kwa lengo la kugawa fedha nao walikuwa wakizihitaji.
Baada ya hali hiyo, wajumbe wa mkutano huo kutoka wilayani Tarime walilazimika kutoka nje ya ukumbi, kisha kuanza kupambana na wafuasi hao kwa kurushiana ngumi, mawe na viti huku katibu msaidizi huyo wa CCM wilayani Tarime akitimua mbio na kuingia kwenye ofisi ya Katibu wa CCM wa mkoa ili kunusuru maisha yake.
Kutokana na vurugu hizo, wajumbe hao walionekana kujawa na hasira huku wakimkimbiza kwa mbio katibu huyo msaidizi, ambaye baadaye alifanikiwa kuingia na kujifungia ndani ya ofisi ya CCM mkoa huo.
Baada ya Katibu huyo kujificha ndani ya ofisi akikwepa kipigo, wajumbe hao waliokuwa na hasira walimgeukia na kutaka kumnyanganya kamera mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Mara, Mabere Makubi, kwa madai kwamba amepiga picha za vurugu hizo.
Baadhi ya wajumbe hao walioonekana kumzonga kwa kutaka kumpokonya kamera mwanahabari huyo, lakini walishindwa kutimiza lengo lao hilo baada ya Makubi kuwakabidhi kamera yake ili watoe mkanda wa picha ya video waliokuwa wakiuhitaji, jambo ambalo walishindwa kisha kuondoka na hasira zao.
Mmoja wa watu walionusurika na kipigo cha vijana hao, Arafat Idd kutoka Wilaya ya Musoma Mjini, alimlalamikia mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa UVCCM Mkoa wa Mara aliyemaliza muda wake, kwa kutaka kuhodhi nafasi zote zichukuliwe na wajumbe wa wilaya ya Tarime.
Huyu (anamtaja jina) anataka nafasi zote zichukuliwe na watu wa wilaya anayotoka... Makao makuu tunaomba hili suala walione na kulishughulikia, sisi ni vijana wa mjini na tuna uwezo wa kufanya chochote, alisema kwa jaziba mmoja wa vijana hao.
Wanaodhani na kueneza nimekimbia si sawa, si kweli...SINA MUDA WA KUKESHA NA NYIE, MUNGU ALIUMBA USIKU TUPUMZIKE.....POLENI MLIOKESHA KUSUMBUA VICHWA MTAPOTOSHAJE UKWELI KUWA....mpira magoli si chenga......
Nawashukuru mliotambua na kukiri kuwa "nape kiongozi mkubwa" ...walau akili zimeanza kuwarudia huo ni mwanzo mzuri....! LAKINI KUBWA HAPA PIA NIMEFURAHI UKIRI WENU KUWA MAJIMBO NA KATA ZOTE NI MALI YA CCM, NDO MAANA YA HESABU YENU YA KATA MBILI KUZICHUKUA NA MKAFURAHIA KAMA MAJUHA....MPIGE HESABU HII HATA MWAKA 2014 NA 2015......MUWE NA LUGHA HII HII.....HAKIKA MTAONYESHA UKOMAVU MKUBWA SANA WA KISIASA....
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amezidi kuwatimulia vumbi wapinzani wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutokana na wajumbe wanaounga mkono kambi yake kuzidi kupeta katika uchaguzi.
Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha uliomalizika jana, kambi mbili zinazowaunga mkono Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe katika mbio za urais 2015, zilionekana kutifuana vikali. Msuguano huo ulianza kujitokeza tangu juzi kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa huo, ambapo juhudi za Katibu wa Mkoa, Mary Chatanda kutaka kuihujumu kambi ya Lowassa, ziligonga mwamba na kunusurika kipigo.
Chatanda ambaye alikuwa akifanya juhudi za kuhakikisha mshindi anakuwa Dk. Harold Adamson, aliambulia patupu baada ya Robinson Meitinyiku anayedaiwa kuungwa mkono na Lowassa, kushinda kwa kura 247 dhidi ya 188 za mpinzani wake.
Katika mwendelezo huo huo wa msuguano wa kambi hizo mbil, jana Katibu huyo CCM Mkoa wa Arusha, Chatanda, alijikuta akiaibishwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa chama baada ya kujifanya amesahau kumtambulisha Lowassa.
Chatanda aliufanya ukumbi mzima kupiga kelele kubwa wakisema bado! bado! Bado Eddo! Eddo! Eddo! Na ndipo kwa aibu kubwa, katibu huyo akameza mate na kumtambulisha Lowassa.
Hata hivyo, hatua hiyo ilitafsiriwa tofauti na baadhi ya wajumbe ambapo wengine walisema ni tukio la bahati mbaya, lakini wengi wao wakidai kuwa Chatanda alifanya makusudi kutokana na kundi analoliunga mkono kuanguka kwenye uchaguzi wa UVCCM.
Katika mkutano huo mkuu wa mkoa uliohudhuriwa na wajumbe 833, nafasi ya Mwenyekiti ilirudi tena kwa Onesmo ole Nangole ambaye anadaiwa kuunga mkono na Lowassa, akiwaacha kwa mbali washindani wake wawili.
Nangole alijizolea kura 604 huku akifuatiwa kwa mbali na Adam Choro wakati Dk. Salash Toure aliyedondoshwa na Lowassa kwenye uchaguzi wa ujumbe wa NEC Taifa kupitia wilayani Monduli akiambulia kura 13.
Akitangaza matokeo hayo, msaimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, alisema kura zilizopigwa ni 833 ambapo kura halali zilikuwa 830 na tatu ziliharibika.
Mapema akifungua mkutano huo kabla ya uchaguzi, Prof. Maghembe, aliwataka wajumbe kuacha kuzomea au kushangilia wagombea pindi watakapofika mbele yao kujinadi.
Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi watakaojenga chama kwa kuhakikisha wanavunja makundi na kuwaunganisha wanachama wote ili kuvirejesha viti vya udiwani na ubunge walivyovipoteza mkoani humo.
"Msichague viongozi watakaobweteka na kutugawa, hawa hawatufai, tuepuke viongozi wa aina hii, tuchague watakaokisaidia chama," alisema Maghembe.
Naye Lowassa, akizungumza baada ya kuchaguliwa na wajumbe kuwa mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, aliwashukuru wote kwa imani waliyompa huku akishangiliwa kwa kishindo. "Wajumbe nimewaelewa na sitawaangusha, nimewaelewa ndugu zangu sitawaangusha, nawashukuru kwa kunishangilia, ila sasa tusishangilie tusije kuharibu utaratibu," alisema Lowassa.
Akijinadi kwa wajumbe hao, Nangole aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia dosari zilizopo na kushughulika na watu wote wanaoleta makundi ndani ya chama kwa mgawanyiko kuanzia wilayani mpaka Mkoa.
Naye Dk. Toure, aliwaomba wajumbe hao kuwa akichaguliwa, atamaliza makundi yaliyopo ambayo yamekiathiri chama hicho kwani wanachama wamegawanyika kila ngazi na kuwasihi wawabwage wagombea waliotumia fedha kuomba kura kwenye uchaguzi huo.
Mgawanyiko ndani ya chama ulionekana kuzungumzwa na kila mtu kwani hata Chora, naye aliwaomba wajumbe wamchague ili tatizo hilo alilodai kuwa limewapotezea majimbo.
Kijana tafadhali tueleze zaidi ya kushinda uchaguzi ni nini wananchi watanufaika nacho toka CCM. Maana naona kila siku CCM mnaongelea kushinda uchaguzi, lakini hamuendi hatua moja mbele na kueleza jinsi gani wananchi watanufaika na utekelezaji wa ilani ya CCM, mipango ya maendeleo ya miaka mitano, dira ya 2025 nk. Wewe kama katibu mwenezi mbona huenezi fikra pama za CCM katika kumletea maendelea mtanzania na haswa mkulima aliye kijijini?
mchezo huu mi rahisi kuelewa nashangaa hata katibu wao mwenezi ana kichwa kigumu kuelewa.
CCM ILIKUWA INATETEA KATA JUMLA 25
CHADEMA KATA 2
CUF 1
TLP 1.
KIPENGA KIMEPIGWA BAADA YA DAKIKA TISINI.
MATOKEO.
CCM KATA IMERUDISHA KATA 23 IMEPOTEZA KATA 2
TLP 1 IMERUDISHA KATA YAKE 1 IMEONGEZA KATA 0
CHADEMA 5 IMERUDISHA KATA ZAKE 2 NA IMEONGEZA KATA 3
CUF IMEPOTEZA KATA 1 HAKUNA WALICHOONGEZA.
Kitu simple kama hicho kina ugumu gani wa kuelewa wakati kitu kinaonyesha losers na winner ni nani ndiyo maana nchi tuna matatizo
makubwa ya uongozi kama kiongozi wa chama kikubwa kama hiki haelewi hesabu rahisi namna hii unategemea anao uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi kweli.
Nape mbona huongelei yale ma land cruiser hadtop yenye nembo za kinga,ukimwi ya idara ya afya ludewa bila aibu mliyapeleka kwenye kampeni na plate number zake za stk,sm je hao madereva posho mliwalipa nyie ccm au zilitoka idala ya afya nashangaa hapa jukwaani unashabikia ushindi je ushindi niwa ccm au serikali au wa vyama vyote viwili yaani serikali na ccm halafu unasema watani zako na ukataja idadi ya viti walivyopata CDM sasa mlikuwa mnashindana na cdm peke yake bila vyama vingine?au ndio ule usemi cuf ni ccm b unaudhihilisha hapa na nccr hilo lipo wazi ni ccm c maana wengine kama Mbatia umewapa umbunge wa mezanii.
''kufungwa twafungwa lakini chenga twawala'' ndio nini sasa? mashabiki tunataka magoli sio chenga! baada ya kichapo cha magoli 22 kwa 05, chadema naona sasa mmeanza kuweweseka, hakuna haja ya kutafuta 'x' wakati hesabu ya 22 na 05 ni rahisi na aihitaji mjadala.
Wanaodhani na kueneza nimekimbia si sawa, si kweli...SINA MUDA WA KUKESHA NA NYIE, MUNGU ALIUMBA USIKU TUPUMZIKE.....POLENI MLIOKESHA KUSUMBUA VICHWA MTAPOTOSHAJE UKWELI KUWA....mpira magoli si chenga......
Nawashukuru mliotambua na kukiri kuwa "nape kiongozi mkubwa" ...walau akili zimeanza kuwarudia huo ni mwanzo mzuri....! LAKINI KUBWA HAPA PIA NIMEFURAHI UKIRI WENU KUWA MAJIMBO NA KATA ZOTE NI MALI YA CCM, NDO MAANA YA HESABU YENU YA KATA MBILI KUZICHUKUA NA MKAFURAHIA KAMA MAJUHA....MPIGE HESABU HII HATA MWAKA 2014 NA 2015......MUWE NA LUGHA HII HII.....HAKIKA MTAONYESHA UKOMAVU MKUBWA SANA WA KISIASA....
Na huu sio mpira wa miguu Nnauye Jr, ni siasa. Siasa ni sayansi, ni maisha ni kila kitu. Kufananisha siasa na mpira wa miguu...unahesabu magoli..sielewi.Labda ndio maana tupo hapa tulipo. Watu wapo Dodoma wanagawa rushwa kwenye chaguzi huu serikali wanayoiongoza haijalipa mishahara mpaka leo tarehe 2/11. Lakini serikali ipo na wenye nayo wanakenua meno kwa kupoteza kata 3 tu. Labda huo hiyo ndio kazi ya Uenezi uliyoambiwa uifanye
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.