CHADEMA 'mnazingua'

CHADEMA 'mnazingua'

2015 ndo ilikuwa anguko rasmi la chadema, na mageuzi makubwa ya CCM. wakabadilishana kwa chama tawala kuanza kusimamia agenda ambazo zilikuwa zikiimbwa na vyama vya upinzani, na vyama vya upinzani vikazikana agenda zilzofikisha
Ebu nikumbushe tena agenda hiyo ambayo CCM inaisimamia vile!!
 
Kama chama kikuu cha upinzani nchini, wapenda demokrasia tunawatetea na kuwategemea. Kama chama kikuu cha upinzani nchini,tunatarajia mjipange na kuwinda ushindi mwaka 2020. Lakini,mnazingua.

Kwasasa hamuainishi hoja mnazozisimamia kama ilivyokuwa wakati ule wa kupinga ufisadi. Kwasasa mmekuwa mkiibuka na hoja zinazotokana na yanayosemwa. Yaani,hoja za kudandia. Mnazingua.

Lengeni kuongeza Wabunge na Madiwani mwaka 2020 badala ya kukesha na vijembe twitter,youtube na facebook. Acheni kuyumbayumba na kudaka hoja zisizo na msingi. Mnazingua.

Jipambanueni kwa hoja. Jengeni chama chenu na kuwatumikia wananchi waliowaamini majimboni,katani,vijijini na vitongojini. Hakuna faida ya kubishana kila kukicha na vyombo vya dola na Serikali. Pigeni kimyakimya. Acheni kuzingua!
You told them brother.
 
Hoja zimekuwa nyingi ila wakujibu hizo hoja ndani ya CCM na Serikali hakuna waliondoka na Kikwete, sasa hivi kuna aina ya CCM isiyoweza kujitetea yenyewe imeamua kujificha nyuma ya Polisi. Ukijenga hoja utaishia Polisi badala ya kujibiwa kwa hoja.... Na hapo ndio pengo la CCM ya Kinana na Nape Nnauye linapoonekana wazi. Kujenga hoja kwa wanaCCM hii ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa... Ngoja waendelee kuchezeshwa ngoma tu, waendelee kuicheza tu.
 
Kama chama kikuu cha upinzani nchini, wapenda demokrasia tunawatetea na kuwategemea. Kama chama kikuu cha upinzani nchini,tunatarajia mjipange na kuwinda ushindi mwaka 2020. Lakini,mnazingua.

Kwasasa hamuainishi hoja mnazozisimamia kama ilivyokuwa wakati ule wa kupinga ufisadi. Kwasasa mmekuwa mkiibuka na hoja zinazotokana na yanayosemwa. Yaani,hoja za kudandia. Mnazingua.

Lengeni kuongeza Wabunge na Madiwani mwaka 2020 badala ya kukesha na vijembe twitter,youtube na facebook. Acheni kuyumbayumba na kudaka hoja zisizo na msingi. Mnazingua.

Jipambanueni kwa hoja. Jengeni chama chenu na kuwatumikia wananchi waliowaamini majimboni,katani,vijijini na vitongojini. Hakuna faida ya kubishana kila kukicha na vyombo vya dola na Serikali. Pigeni kimyakimya. Acheni kuzingua!
Wewe Petro kada wa CCM tangu lini ukafurahishwa na Chadema? Kazi kujipendekeza tu!
 
2015 ndo ilikuwa anguko rasmi la chadema, na mageuzi makubwa ya CCM. wakabadilishana kwa chama tawala kuanza kusimamia agenda ambazo zilikuwa zikiimbwa na vyama vya upinzani, na vyama vya upinzani vikazikana agenda zilzofikisha hapo vilipo. Watu huwa wanakataa lakini ukweli uliowazi demokrasia inayoliliwa na vyama hivi inapaswa kuanzia katika vyama vyao kwanza, laiti kama ubabe na mabavu yasingetumika ninaamini leo hii CUF ingekuwa imara, Chadema ingekuwa imara
Tatizo moja nyie watu mmekuwa kama kundi kubwa la nyumbu hakuna wa kumshauri mwenzie. Kuanzia mwenyekiti wenu mpaka nyie mizigo yake (kwa mujibu wa mwenyekiti kuwa yeye ni dereva wa roli). Ujasiri wa kusema CDM ilikufa mnautoa wapi wakati mnatishwa na CDM kiasi kwamba mnakesha hamlali hata kwenda kuchangia damu Hospital mnawakamata kisa, Kesho magazeti yataandika Chadema wachangia damu.... CCM yenye hoja ilikuwa enzi za Kina Nape na Mzee Kikwete wao walikuwa na uwezo wa kujenga hoja na kupambana jukwaani..... Leo hii hata mikutano ya hadhara mnaiogopa kwa nini wakati Chadema imekufa? Enzi za Kikwete, Chadema waliwahi kuwa na oparesheni Sangara huko kanda ya ziwa ilipita na kina Nape walijitahidi kufurukuta na kujibu hoja jukwaani. Sasa CCM hii ya Mh Sizonje hana hoja, watendaji wake kwenye chama nao hawana hoja, walitishiwa na operation UKUTA tu tukajionea maajabu, badala ya watu kujiandaa kupangua hoja tukaona Polisi mwezi mzima wanafanya mazoezi mpaka ndege za jeshi zilirushwa. Halafu kutwa eti Chadema kilikufa. Ni nini mnachohangaika nacho kila siku kama kimekufa. Msijifungie Lumumba piteni mitaani muone kama zile takwimu zenu za asilimia ngapi sijui kukubalika kama ziko mnavyojiaminisha.... Kama ni kufa kwa chama basi CCM ndio inayokufa taratiibu kwa mpangilio uliotukuka. Shida ni alie kwenye chombo kinachozama kujua kama anazama humchukua muda sana mpaka mambo yanapokuwa 'out of control' ndio hushtuka. Sasa hivi hakuna CCM inayosimama peke yake mpaka ifanye 'kolabo' na polisi kutengeneza POLICCM. Lakini bado wanachemsha, na muendelee hivyo hivyo maana mnawarahisishia CDM sana. Kila mkiwaweka mahabusu huku nje wananchi wanaona na wanakaa kimya. Sasa subirini wakati wa kupasuka. Refer to "Ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka"
 
Mkuu ukivaa Tshirt yenye picha ya Pray4Lissu unajikuta uko Central Police ukisubiria hakimu akuhukumu si tena kwa kuvaa tshirt bali kwa kuandamana bila kibali.

Ukikutwa umevaa Tshirt ya M4C uko maeneo ya MAABARA ukitoa damu napo jiandae kulala kituo kilichopo karibu na hospitali husika kama Temeke basi kituo kikuu cha Polisi Temeke,kama Muhimbili basi pale karibu na Daraja.

Unataka Chadema wafanyeje ndugu yangu??Ukiongea kama Lissu basi jiandae kwa kula mawe 38 bila huruma.Ukiwa unapigana kwa maneno wenzako wanapigana kwa SMG unataka wafanyeje Mkuu hebu tupe hint.
Akijibu mkuu naomba uni tag please maana huyu jamaa kama vile kaingizwa kwenye paylol ya lumumba str.
 
Chadema inapinga Ufisadi,hizo sera unazosema CCM imechukua kutoka Chadema sio kweli Chadema hakikuwa na sera za kuua wanasiasa na wakosoaji.
 
Back
Top Bottom