CHADEMA mmekuwaje tena???

CHADEMA mmekuwaje tena???

VUTA-NKUVUTE Mzee Tupa Tupa wa Lumumba,

Kuna suala moja linaniumiza kichwa ambalo ni CCM watafurahi kuona CHADEMA inakufa, lakini Watanzania watafaidika nini kwenye Mfumo wa siasa wa vyama vingi ambako chama kimoja ndio kinaishi?

Siyo lazima chama cha upinzani kiitwe CHADEMA, chochote kinaweza kuwa chama cha upinzani ili mradi tu hakina viongozi wapenda madaraka, madikteta, wafuja mali za chama, wanaorusha ngumi pale wanapoambiwa ukweli.
 
Nadhani wamekusikia mzee wetu.ila ulipokosea ni uliposema "CCM yetu"mimi nadhan ungexema "CCM yangu".hatuhtj CCM ifanye vizuri.mda wbke umekwisha,it should go now!kwa ujumla wake ni vema wanaCHADEMA tukafuata ushauri huu.tusikubali kuwapopularize hawa magamba kwa Kuunga mkono thread zao nying za kuiatack CHADEMA
CCM ni yangu, yako, ya yule, yetu na ya kila mmoja wetu. Ndo maana Dr Slaa anayo kadi ya CCM hadi hii leo
 
Hakika namwaambieni, BILA YA KUWEPO KWA UKOMO WA UONGOZI KWENYE KATIBA YA CHAMA, mtawaita CCM wachawi, mtahamia kwa NCCR-MAGEUZI, na mwishoe kwa CUF na bado hamtapata suluhu.
 
Siyo lazima chama cha upinzani kiitwe CHADEMA, chochote kinaweza kuwa chama cha upinzani ili mradi tu hakina viongozi wapenda madaraka, madikteta, wafuja mali za chama, wanaorusha ngumi pale wanapoambiwa ukweli.

::::::::::::::::::::::::
Hii inanikumbusha enzi za NCCR
Mageuzi ilianza hivi hivi.
Ni wazi kabisa CCM haijazoea
kukabiliana na upinzani mkubwa /
mkali kwa mwongo mmoja(vipindi
viwili vya uchaguzi).Mwaka 1995
NCCR Mageuzi waliisumbua sana CCM
walichofanya ni kuisambaratisha
kabla ya uchaguzi wa mwaka
2000.Mwaka 2010 Dr Slaa wa CDM
aliwasumbua sana wasingependa
kuingia uchaguzi wa mwaka 2015 huku
CDM wakizidi kujitanua kila uchao
wakijua wazi watakuwa na mgombea
mpya asikuwa na nguvu za kidola
ambaye anaweza kupambana na mgombea
mwenye rekodi nzuri na mwenye mtaji
mkubwa wa kura za mwaka 2010.CCM
wanajua wazi baada ya uchaguzi mkuu
uliopita CDM haikulala bali
walianzisha programs maalum M4C
ambayo ilihakikisha inawafikia
wapiga kura wengi kabla ya uchaguzi
mkuu ujao.
CDM wakiweza kushinda mtihani ulio
mbele yao ni wazi uchaguzi mkuu
ujao itabidi CCM wajiandae kwa
kumweka mgombea mwenye rekodi nzuri
ya uadilifu.CCM isingependa
kuchagua mgombea mzuri kwasababu ya
kitisho cha CDM kuzidi kujiongezea
umaharufu.Warasimu wa CCM
wangependa kumchagua mgombea
atakayelinda uchafu (maslahi) wao
ili linaweza kuepukwa iwapo CDM
itasambaratishwa.
Kwa afya na ustawi wa taifa letu
tusikubali CDM ikasambaratishwa
itatuchukua miaka mingine 15 kujenga
upinzani mwingine wenye nguvu huku
tukiwaachia walafi/wezi wakitafuna
na kutuibia rasilimali
zetu.Tusisahau Mzee Mkapa
alivyofanya baada ya kusambaratika
kwa NCCR Mageuzi.Mabenk yaliuzwa
kwa bei ya kutupa,madini,mashirika
ya umma,EPA,Meremeta zote
zilisababishwa na ukosefu wa
upinzani wa maana ulioanza
kujengeka enzi hizo.
 
Mzee Tupatupa wa Lumumba ahsante kwa uchambuzi wako....Chadema ni chama makini sana..
 
Ushauri wangu jana niliutoa hapa na nitamwaandikia Chadema uongozi wajue .Maneno na msimamo wangu ni mmoja kwamba hakuna Uchaguzi ndani ya Chadema hadi baada ya Uchaguzi mkuu 2015.Mbowe na Slaa na timu yenu yote mtuvushe salama kwanza .
 
hii post ni mara ya tatu una paste ninauhakika kama kitendo hiki kingefanywa na mtu wa chadema angeshakula ban maana jana tu imetokea ama kweli moderator yuko mifukoni mwaccm..

Kama jana ulikula ban, leo umeingiaje humu?
 
hii post ni mara ya tatu una paste ninauhakika kama kitendo hiki kingefanywa na mtu wa chadema angeshakula ban maana jana tu imetokea ama kweli moderator yuko mifukoni mwaccm..

Mkuu, suala la Katiba ni jambo la msingi katika chama kuliko jambo jingine lile. Mkiacha katiba yenu ichakachuliwe na hawa wenye tamaa ya madaraka mwisho wa siku mtajikuta mnachakachuliwa hadi haki zenu
 
Siyo lazima chama cha upinzani kiitwe CHADEMA, chochote kinaweza kuwa chama cha upinzani ili mradi tu hakina viongozi wapenda madaraka, madikteta, wafuja mali za chama, wanaorusha ngumi pale wanapoambiwa ukweli.
Wewe pia utakua mmoja kati ya hao walionunuliwa ipads... Kazana kupost wakuone vinginevyo utanyang'anywa ubakie na kile kitochi chako
 
Wanayumbishwa na mambo madogo,kumbe mengine ni kuyaachia kama yaliyo,Zito ni mbaya sana kwa sababu ni kiongozi anayetaka kudhoofisha chama,Mungu bariki Chadema
 
Ushauri wangu jana niliutoa hapa na nitamwaandikia Chadema uongozi wajue .Maneno na msimamo wangu ni mmoja kwamba hakuna Uchaguzi ndani ya Chadema hadi baada ya Uchaguzi mkuu 2015.Mbowe na Slaa na timu yenu yote mtuvushe salama kwanza .

Nasema: CHADEMA tunadhani adui yetu ni CCM hapana ni Watendaji wetu katika chama(SLAA na MBOWE), tukawabane hao waache udikteta, waweke wazi taarifa za fedha, wakasimu shughuli zisizo wahusu kwa wenye madaraka hayo na warudishe kwenye Katiba kile kipengele cha ukomo wa uongozi wa ngazi ya juu ndani ya Chama.
 
Jana mlipotea nyie. Leo mnakuja kwa kujikongoja. Huo ndo mwanzo tu, mwisho wa siku mtakimbiana hapo Kinondoni

Chezeiya kuhongwa ipad wewe alaaah.... Ongeza bidii ya kupost labda utaongezewa nyingine ya pili!!!
 
Mzee tupatupa hapo umeeleweka, hasama hizi zilianza toka uchaguzi uliopita zimekuwa za chini chini sasa zimeanza kukua taratibu, kisa ni kundi moja dogo kuhisi linanyanyaswa!.

Sasa hebu tuweke sawa na hawa viongozi wa CDM waandamizi wanaolalamika kupitia vyomba vya habari kwamba wanaonewa badala ya kuripoti malalamiko yao kwenye vikao rasmi vya chama - je chama kiwachukulie hatua gani zinazofaa bila kuacha majeruhi?
 
Wanayumbishwa na mambo madogo,kumbe mengine ni kuyaachia kama yaliyo,Zito ni mbaya sana kwa sababu ni kiongozi anayetaka kudhoofisha chama,Mungu bariki Chadema

Haya ndiyo maneno yatakayokimaliza CHADEMA, ZITTO na wenzake wanajua uchungu walio nao juu ya matumizi mabaya ya madaraka ndani ya chama, wapambe mnawavimbisha kichwa SLAA na MBOWE kuwa ZITTO anatumiwa na CCM, hakika hili linawafanya akina ZITTO kuwa na hasira sana kwa vile wanaujua ukweli kulikoni ambavyo wanachama wa kawaida wanavyojua.
 
Nasema: CHADEMA tunadhani adui yetu ni CCM hapana ni Watendaji wetu katika chama(SLAA na MBOWE), tukawabane hao waache udikteta, waweke wazi taarifa za fedha, wakasimu shughuli zisizo wahusu kwa wenye madaraka hayo na warudishe kwenye Katiba kile kipengele cha ukomo wa uongozi wa ngazi ya juu ndani ya Chama.

Nyie huko ccm mna madikteta wangapi??? Ya chadema tuachieni wenyewe hayawahusu.... Tunawapenda madikteta wetu mbowe na slaa!
 
Haya ndiyo maneno yatakayokimaliza CHADEMA, ZITTO na wenzake wanajua uchungu walio nao juu ya matumizi mabaya ya madaraka ndani ya chama, wapambe mnawavimbisha kichwa SLAA na MBOWE kuwa ZITTO anatumiwa na CCM, hakika hili linawafanya akina ZITTO kuwa na hasira sana kwa vile wanaujua ukweli kulikoni ambavyo wanachama wa kawaida wanavyojua.

Utasubiri sana kuona chadema ikimalizika!.... Yaani kama wale wafuasi wa kibwetere walochomwa moto ndani ya kanisa!
 
Mzee tupatupa hapo umeeleweka, hasama hizi zilianza toka uchaguzi uliopita zimekuwa za chini chini sasa zimeanza kukua taratibu, kisa ni kundi moja dogo kuhisi linanyanyaswa!.

Sasa hebu tuweke sawa na hawa viongozi wa CDM waandamizi wanaolalamika kupitia vyomba vya habari kwamba wanaonewa badala ya kuripoti malalamiko yao kwenye vikao rasmi vya chama - je chama kiwachukulie hatua gani zinazofaa bila kuacha majeruhi?

Sidhani kama kuna dawa zaidi ya kuwepo uwazi ndani ya Katiba ya chama, taarifa za fedha, na mgawanyo wa madaraka badala ya kurusha ngumi pale wanapoambiwa ukweli.
 
Back
Top Bottom