CHADEMA mmekuwaje tena???

CHADEMA mmekuwaje tena???

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Sasa mnayumba;mnapoteza mwelekeo. Nyinyi tunawategemea kama wapinzani wakuu Tanzania. Wabunge wenu 49 Bungeni Dodoma wanafanya kazi inayotukuka na kukonga nyoyo za watanzania wengi.Wabunge wenu ni watetezi,wajenzi wa hoja,waibua mijadala ya kujenga Taifa,walinda maslahi ya nchi,hawayumbishwi haraka na sifa nyinginezo wazistahilizo viongozi wa kupigiwa mfano. Lakini chamani ni tofauti.

Iweje myumbishwe na masuala madogo madogo ya kisiasa kirahisi namna hiyo? Kweli nawaambia, mtatingishwa na wapinzani wenu kirahisi msipojirekebisha. Kiukweli, mmepambana vya kutosha. Kuanzia kuitwa chama cha kikabila,kikanda,kidini na kigaidi. Mapambano hayo mkayashinda. Sasa wanatumiwa watu kufitisha viongozi chamani. Wanatumiwa akina Zitto,Shibuda na sasa Samson Mwigamba. Hawa wanatumiwa tu.Wanachorwa kwenu kama wasaliti na waropokaji. Nanyi mnaelekea kuamini. Mtasambaratika kiuongozi.

Kwa Zitto ilitosha kauli yake kuwa 'anachonganishwa na viongozi wake na aachwe afanye siasa'. Kwa Shibuda inatosha kunyamaa kama mfanyavyo. Kwa Mwigamba, yatosha kusimamia tamko lenu la kichama la Kanda ya Kaskazini na taratibu nyingine kufuata. Milango hii hatari kwenu ifungwe haraka. Laasivyo, itaingiza maadui na uadui.

Sasa mnashupaliwa kuhusu Katiba ya chama. Itoshe kusema kuwa mtanzania yeyote mwenye ushahidi wa ubatili wa Katiba ya CHADEMA aende na nyaraka zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kuilalamikia.Msajili atafuata sheria.Atashughulikia suala hilo haraka na hadi mwisho wake.Jaji Mutungi anamsubiri mtanzania huyo!

CHADEMA niwaambie, kuna watu hapa Lumumba na Ofisi nyingine wamenunuliwa 'Ipads' na 'Iphones' kupambana nanyi mtandaoni. Hasa hapa JF. Watawalia muda wenu na kuwasimamisha. Mkichelewa kuchukua hatua,mipango yenu mingi itakwama.Mtadhoofu.Wapenda demokrasia kama mimi tutabaki na huzuni kuu.Tunahitaji upinzani bora nchini ili CCM yetu ifanye bora zaidi.Tunahitaji CCM yetu ibanwe ili itoe matunda vutizi.

Kwa kifupi, CHADEMA hamna haja ya kuchonganishwa kila kukicha. Please, do not expose your weak points easily. Wanaotajwa watajwe;wanayosema yaripotiwe;anayelalama alalame lakini CHADEMA songeni mbele mjenge demokrasia. Tunatarajia mechi kali ya kisiasa hapo 2014 na 2015. CHADEMA beware!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
asante sana mzee tupatupa wa Lumumba. ushauri murua kabisa huu.
 
Aisee, Mzee Tupatupa kweli una busara sana!
 
Mambo hadharani hakuna chama hapo ila ni genge la wajanja wachache waliojiunga na kuanzisha kikundi chao.kwa mwendo huo mlio nao hamtoweza kamwe kuingia magogoni.

mnajifanya mnapigania democracy kumbe mnapigania matumbo yenu,Big up ZITO ZUBERI KABWE MWANA MWANDIGA umeamua kujiweka pembeni na siasa za maji mataka.:smile-big:wana uana wenyewe kwa wenyewe.
 
Tatzo wengne hawaelewi. Kazi kumponda zitto tu kisa anasifiwa na maccm.kwani yeye aliomba asifiwe? Siku tundu lissu akisifiwa na maccm naye mtasema anatumiwa? Tunachonganishwa nasisi tunakubali.
 
Mambo hadharani hakuna chama hapo ila ni genge la wajanja wachache waliojiunga na kuanzisha kikundi chao.kwa mwendo huo mlio nao hamtoweza kamwe kuingia magogoni.

mnajifanya mnapigania democracy kumbe mnapigania matumbo yenu,Big up ZITO ZUBERI KABWE MWANA MWANDIGA umeamua kujiweka pembeni na siasa za maji mataka.:smile-big:wana uana wenyewe kwa wenyewe.
Yale yale! Ndio kama hawa sasa
 
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

CHADEMA ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
 
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
Kada mwenzangu ZeMarcopolo,naona leo ni maneno haya haya tu threads zote.Kulikoni?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

naona unacopy na kupesti sasa tutakulipaje hapa lumumba naona unafanya kazi katika misingi ya kilaghai...
 
CCM itachukua nchi tena kwa sababu ya maendeleo inayowaletea wananchi na siyo sababu ya wadau wa kwenye key boards hawafikii hata asilimia 0.00000000001 Nyie kaeni na hesabu zenu na kitoto mwisho wa siku mtakuja lalamika mmeibiwa kura.
 
Nazani hapa point inaeleweka na wahusika wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mambo yanakwenda poa japo sio mbaya kukumbushana.
 
Nadhani wamekusikia mzee wetu.ila ulipokosea ni uliposema "CCM yetu"mimi nadhan ungexema "CCM yangu".hatuhtj CCM ifanye vizuri.mda wbke umekwisha,it should go now!kwa ujumla wake ni vema wanaCHADEMA tukafuata ushauri huu.tusikubali kuwapopularize hawa magamba kwa Kuunga mkono thread zao nying za kuiatack CHADEMA
 
Sasa ndiyo ujue kuwa waliokuwa wakiita chama cha ukabila, udini na Ukanda hawakuwa wanakosea.
 
VUTA-NKUVUTE Mzee Tupa Tupa wa Lumumba,

Kuna suala moja linaniumiza kichwa ambalo ni CCM watafurahi kuona CHADEMA inakufa, lakini Watanzania watafaidika nini kwenye Mfumo wa siasa wa vyama vingi ambako chama kimoja ndio kinaishi?
 
Nadhani wamekusikia mzee wetu.ila ulipokosea ni uliposema "CCM yetu"mimi nadhan ungexema "CCM yangu".hatuhtj CCM ifanye vizuri.mda wbke umekwisha,it should go now!kwa ujumla wake ni vema wanaCHADEMA tukafuata ushauri huu.tusikubali kuwapopularize hawa magamba kwa Kuunga mkono thread zao nying za kuiatack CHADEMA

Mbona mnasingizia CCM? mbona mambo yako wazi jamani? jibuni hoja za Mwigamba badala ya kulalamika tu.
 
Back
Top Bottom