Uchaguzi 2020 CHADEMA mkiweza kulinda kura ambazo Watanzania tutawapigieni, basi Ikulu ni yenu

"mshahara nikulipe, gari nikupe halafu umtangaze mpinzani kashinda? by jiwe akiikemea TumeCCM.
kumbuka alitamka hivo akiwa Rais na sasa yeye ni mgombea na ni mteuzi wa hiyo Tume...
dah!!
 
"mshahara nikulipe, gari nikupe halafu umtangaze mpinzani kashinda? by jiwe akiikemea TumeCCM.
kumbuka alitamka hivo akiwa Rais na sasa yeye ni mgombea na ni mteuzi wa hiyo Tume...
dah!!
Tume inalipwa na serikali kwa mujibu wa sheria na bajeti iliyopitishwa na bunge, hailipwi na CCM!
 
Tume inalipwa na serikali kwa mujibu wa sheria na bajeti iliyopitishwa na bunge, hailipwi na CCM!
sasa kama ndivyo hiyo jeuri anaipata wap ya kuitishia Tume eti ikimtangaza mpinzani itakiona cha mtema kuni!!!!
 
Naendelea kuyaamini kwa dhati maneno yako mkuu....
Tuko tayari kulinda kura zetu
 
Yaani mpoteze rasilimali za chama kulinda kura 200,000 za Lissu dhidi ya 18,000,000 za ccm. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha
 
Yaani mpoteze rasilimali za chama kulinda kura 200,000 za Lissu dhidi ya 18,000,000 za ccm. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha
2015 ccm Tulishinda kwa bao la mkono..by mwanaccm na mgombea ubunge kwa tiketi ya hiyo hiyo ccm nape nnauye

Uchaguzi ukiwa huru na wa haki ccm ijiandae kukabidhi ikulu...by Katibu Mwenezi wa CCM "TAIFA" na mmoja wa waratibu wakuu wa kampeni za uchaguzi za hiyo hiyo ccm.
 
MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI ZANZIBAR AKIOMBA KURA PEMBA

Bonyeza link hiyo chini kuona shamra shamra zote zinazoendea. Hakika ni Neema tupu kuwa na Dr Hussein Mwinyi
 
Aijipii alisha toa tahadhari kwamba, kulinda kura ni kazi ya jeshi la polisi. Hivyo alisisitiza kwamba waTazania wajiepushe na kujiingiza kwenye matatizo yasio ya lazima.
Shida sio kazi ya IGP. Shida ni kujenga imani kwa watanzania kwamba watatenda haki. Matumizi makubwa sana ya nguvu sometimes sio lazima
 
Aandae mawakala wasio na njaa wala taamaa ili wasije kupokea mlungula toka maccm
Majimbo ambayo chama tawala wamepita bila kupingwa nawashauri vyama vya upinzani kwenye kura za urais waweke mawakala wenye ngozi ngumu, Kuna mambo huwa yanafanyika hata Shetani anashangaa Mf Jimbo la Bumbuli ni uchochoro wa kupitishia kura chafu za rais upinzani msiseme hatukuwaambia.Kwa mfano eti jimbo linawapiga kura laki mbili ila kula za rais zimepigwa laki sita duh.
 
Shida sio kazi ya IGP. Shida ni kujenga imani kwa watanzania kwamba watatenda haki. Matumizi makubwa sana ya nguvu sometimes sio lazima
Minafikiri, hata kama aijipii atatoa angalizo kwa nia njema....
Lakini kwasasa tayari wananchi wengi hawana imani na jeshi hilo, and tayari akili za wanachi wengi zinekwisha jijengea kwamba jeshi litatumika kukikinda chama kilichopo madarakani pamoja na maslahi yake.
 
Hatari sana iyo comrade, tunaomba ushahidi au ni mfano tu umetoa?
 
Hawa CHADEMA wana mtandao mdogo hasa vijijini kulinganisha na Chama Cha Mapinduzi katika nchi hii kubwa kieneo na utawala. Hivyo, ni ndoto kupata mawakala wa kutosha kila kituo cha kupigia kura; labda mapindikizi kwa maeneo ya vijiji; tofauti na katika miji na tena wakishirikiana na vyama vingine.

Kwa mfano ukifatilia CCM wana mabalozi wa nyumba kumi kila kona ya Tanzania wanaowatambua watu wao na kuhakikisha watapiga kura kwao; tofauti na vyama vya siasa vinavyoishia katika miji na vijiji vichache. Pia wana mtaji wa viongozi wengi wa serikali za mitaa na vijiji wanaotumia kuhakikisha ushindi wa uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…