Uchaguzi 2020 CHADEMA mkiweza kulinda kura ambazo Watanzania tutawapigieni, basi Ikulu ni yenu

moshdar

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
2,416
1,219
CHADEMA, na wapinzani wote kwa ujumla, kila dalili inaonesha nyie ni zaidi, mshindani wenu Mkuu CCM anaonesha kila dali ya uoga, kutokujiamini na kukata tamaa. Hana uwezo tena, anajishika na kila aina ya tawi mpaka matawi wasanii, matawi malori, matrekta, mabasi, kuhonga nauli bali hayo matawi kamwe hayaoneshi kufua dafu popote. Tawi pekee la kuwatisheni CHADEMA ni ile kauli ya mshindani wenu mkuu kuwa "nimekupa cheo mshahara mzuri halafu umtangaze mpinzani?! Utanitambua"

CHADEMA ni Hiyo kauli pekee tu ndiyo ya kuishughulikia kwa sasa. Pangeni vizuri ishu za mawakala wenu, zichambueni vilivyo teknikalitizi za ujanja ujanja na wizi wa kura, tumieni kila mbinu halali ndani na hata nje ya nchi, msianzishe fujo lakini kamwe kamwe asilani msikubali tena kugeuza shavu la pili, msikubali tena kumwachia Mungu, watayarisheni vilivyo wapiga kura wote Bara na Visiwani, hata wanaccm ambao dalili zinaonesha wengi wao watakupigieni kura kisirisiri, wajiandae kukataa kura zao kuchakachuliwa na Tume isiyo huru ya uchaguzi. CHADEMA mkiweza hilo historia mpya inakwenda kuandikwa tarehe 24 Oktoba 2020.

Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.

Mungu ni mwema Wanamageuzi, kuna kila dalili nchi Itakombolewa Oktoba mwaka 2020.
 
Aijipii alisha toa tahadhari kwamba, kulinda kura ni kazi ya jeshi la polisi. Hivyo alisisitiza kwamba waTazania wajiepushe na kujiingiza kwenye matatizo yasio ya lazima.
CDM mnamuona mshindani wenu alivo muoga kila inapozungumziwa ishu ya wananchi kukataa uchakachuwaji wa kura? mnamuona lakin? hapa ndipo pekee wanapopategemea kwa sasa. CDM ACT mkiachia hili tobo hapa mmekwisha mapema asubuhi.

Ndugu Lisu umesema wananchi wakishapiga kura wasubiri matokeo vituoni, sisitiza hilo kwa nguvu zote kila saa kila siku, ni la muhimu mnooooo.
 
Ili upinzani kukubali matokeo lazma mambo kadhaa yafanyike na Tume:

1: Lazma mawakala wa vyama wshiriki kuhesabu kura pasipo vitisho na mtu ama taasisi yeyote,
2: Lazma baada ya kuhesabu kura wapewe nakala ya matokeo ya vituo vyao Mara tu ya baada kumalza kuhesabu na wasaini ,
3: Baada ya kusaini lazma matokeo yote kwa kila kituo yabandikwe kwenye bodi za vituo ili wapga kura waone matokeo ya kazi yao.

Hapa kutakua na check and Balance hata Chama kikilalamika kuibiwa kura, vingnevo kuna Chama hakitakubali kushindwa!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
 
Kura kutoka wapi? Chadema haiwezi kuchukua nchi kama itashindwa kuchukua majimbo 70% jua kwamba majimbo ambayo CCM imepita bila kupingwa chadema hawana chao.
 
Ili upinzani kukubali matokeo lazma mambo kadhaa yafanyike na Tume:

1: Lazma mawakala wa vyama wshiriki kuhesabu kura pasipo vitisho na mtu ama taasisi yeyote,

2: Lazma baada ya kuhesabu kura wapewe nakala ya matokeo ya vituo vyao Mara tu ya baada kumalza kuhesabu na wasaini

3: Baada ya kusaini lazma matokeo yote kwa kila kituo yabandikwe kwenye bodi za vituo ili wapga kura waone matokeo ya Kaz yao.

Hapa kutakua na check and Balance hata Chama kikilalamika kuibiwa kura..vingnevo kuna Chama hakitakubali kushindwa!!

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Huu ndiyo utaratibu wa kisheria ambao ni lazima wapiga kura wote waambiwe ili wahakikishe unafuatwa. Kama ambavyo nitawashangaa CDM au mpinzani yeyote atakayelalamika kushindwa wakati utaratibu huo umefuatwa ndivyo nitakavyowashangaa CDM na ACT kama utaratibu huo utakiukwa halafu wabaki eti kumchekea nyani wakitarajia watavuna mahindi. Wana wa Nchi watayarishwe kabisa mapema kwa mtiti mtiti pale taratibu zitakapokiukwa.

Na enyway, kwa kuwa nao ni washindani basi tufanye hata ccm wanayo nafasi ya kushinda lakin sasa wanatakiwa washinde kihalali. bao la mkono alilotuambia mwanaccm nape kuwa ndilo walishinda nalo 2015 kamwe lisikubalike tena.
 
Nafikiri kama tunaunga mkono kuiondoa madarakani CCM hii iliyochakaa, lazima tutambue hii si kazi ya CHADEMA pekee...tutumie wingi wetu, sisi sisi! Tukiiachia Chadema pekee hawataweza.
Mkuu ukisoma vizuri utaona nimesema wapiga kura wote hata wasio wapinzani wakiwemo wale wasio na chama. kumbuka kule kijani pia wapo wengi tu wako kule ama kimaslah tu au kwa kulazimishwa kibabe lakin mioyo yao ipo upinzani ( hasa CDM sehemu kubwa ya bara na ACT sehemu kubwa ya visiwani).
 
Ukitaka kuona nyeti za nyumbu ,subiri upepo upulize hapo October ,28.

Itakuwa fundisho kwa wapinga maendeleo wote.
Hivi mnaposema Chadema ni wapinga maendeleo mnatumia akili au kufuata upepo wa kauli za mropokaji wenu?

Hivi Chadema na CCM nani anawanachama na wafuasi wenye maendeleo binafsi, elimu na ukwasi?

Sasa iweje hao wenye hadhi hizo ndio wawe wapinga maendeleo ndio wenye nafuu ya maisha na hao kondoo wenu masikini ndio wapenda maendeleo?

Jiwe kawafanya wapumbavu sana
 
Kulinda kura ndo kiunzi cha mwisho cha ushindi wa CDM.

Wawekeze kwenye tech hasa kamera na vinasa sautu vya mawakala wao.

Lissu lazima aingie Ikulu ama barabarani.
 
Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.
Umeongea jambo la maana sana, kilichobaki ni kwa CDM kulinda kura zisiibwe na watu, wakiweza hili ushindi ni wao mapema November.
 
8b8772af65a848b2211cc750a1e7211b.jpg
 
Back
Top Bottom