Uchaguzi 2020 CHADEMA mkiweza kulinda kura ambazo Watanzania tutawapigieni, basi Ikulu ni yenu

T2020JPM

JF-Expert Member
Sep 8, 2020
404
250
Majimbo ambayo chama tawala wamepita bila kupingwa nawashauri vyama vya upinzani kwenye kura za urais waweke mawakala wenye ngozi ngumu, Kuna mambo huwa yanafanyika hata Shetani anashangaa Mf Jimbo la Bumbuli ni uchochoro wa kupitishia kura chafu za rais upinzani msiseme hatukuwaambia.Kwa mfano eti jimbo linawapiga kura laki mbili ila kula za rais zimepigwa laki sita duh.
Hatari sana iyo comrade, tunaomba ushahidi au ni mfano tu umetoa?
 
KONGWASTONE

Member
Aug 29, 2020
14
45
CHADEMA, na wapinzani wote kwa ujumla, kila dalili inaonesha nyie ni zaidi, mshindani wenu Mkuu CCM anaonesha kila dali ya uoga, kutokujiamini na kukata tamaa. Hana uwezo tena, anajishika na kila aina ya tawi mpaka matawi wasanii, matawi malori, matrekta, mabasi, kuhonga nauli bali hayo matawi kamwe hayaoneshi kufua dafu popote. Tawi pekee la kuwatisheni CHADEMA ni ile kauli ya mshindani wenu mkuu kuwa "nimekupa cheo mshahara mzuri halafu umtangaze mpinzani?! utanitambua"

CHADEMA ni Hiyo kauli pekee tu ndiyo ya kuishughulikia kwa sasa. Pangeni vizuri ishu za mawakala wenu, zichambueni vilivyo teknikalitizi za ujanja ujanja na wizi wa kura, tumieni kila mbinu halali ndani na hata nje ya nchi, msianzishe fujo lakini kamwe kamwe asilani msikubali tena kugeuza shavu la pili, msikubali tena kumwachia Mungu, watayarisheni vilivyo wapiga kura wote Bara na Visiwani, hata wanaccm ambao dalili zinaonesha wengi wao watakupigieni kura kisirisiri, wajiandae kukataa kura zao kuchakachuliwa na Tume isiyo huru ya uchaguzi. CHADEMA mkiweza hilo historia mpya inakwenda kuandikwa tarehe 24 Oktoba 2020.

Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.

Mungu ni mwema Wanamageuzi, kuna kila dalili nchi Itakombolewa Oktoba mwaka 2020.

Hawa CHADEMA wana mtandao mdogo hasa vijijini kulinganisha na Chama Cha Mapinduzi katika nchi hii kubwa kieneo na utawala. Hivyo, ni ndoto kupata mawakala wa kutosha kila kituo cha kupigia kura; labda mapindikizi kwa maeneo ya vijiji; tofauti na katika miji na tena wakishirikiana na vyama vingine.

Kwa mfano ukifatilia CCM wana mabalozi wa nyumba kumi kila kona ya Tanzania wanaowatambua watu wao na kuhakikisha watapiga kura kwao; tofauti na vyama vya siasa vinavyoishia katika miji na vijiji vichache. Pia wana mtaji wa viongozi wengi wa serikali za mitaa na vijiji wanaotumia kuhakikisha ushindi wa uhakika.
 
Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,175
2,000
CHADEMA, na wapinzani wote kwa ujumla, kila dalili inaonesha nyie ni zaidi, mshindani wenu Mkuu CCM anaonesha kila dali ya uoga, kutokujiamini na kukata tamaa. Hana uwezo tena, anajishika na kila aina ya tawi mpaka matawi wasanii, matawi malori, matrekta, mabasi, kuhonga nauli bali hayo matawi kamwe hayaoneshi kufua dafu popote. Tawi pekee la kuwatisheni CHADEMA ni ile kauli ya mshindani wenu mkuu kuwa "nimekupa cheo mshahara mzuri halafu umtangaze mpinzani?! Utanitambua"

CHADEMA ni Hiyo kauli pekee tu ndiyo ya kuishughulikia kwa sasa. Pangeni vizuri ishu za mawakala wenu, zichambueni vilivyo teknikalitizi za ujanja ujanja na wizi wa kura, tumieni kila mbinu halali ndani na hata nje ya nchi, msianzishe fujo lakini kamwe kamwe asilani msikubali tena kugeuza shavu la pili, msikubali tena kumwachia Mungu, watayarisheni vilivyo wapiga kura wote Bara na Visiwani, hata wanaccm ambao dalili zinaonesha wengi wao watakupigieni kura kisirisiri, wajiandae kukataa kura zao kuchakachuliwa na Tume isiyo huru ya uchaguzi. CHADEMA mkiweza hilo historia mpya inakwenda kuandikwa tarehe 24 Oktoba 2020.

Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.

Mungu ni mwema Wanamageuzi, kuna kila dalili nchi Itakombolewa Oktoba mwaka 2020.
Chadema na wapinzani ni nani, mbona kama unajitoa wakati umesema utawapa kura? Wewe upige kura yako usiilinde useme 'chadema' na wapinzani wailinde? Hakikisha unailinda kura yako, usitafute kisingizio.
 
Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,175
2,000
Ukitaka kuona nyeti za nyumbu, subiri upepo upulize hapo October ,28.

Itakuwa fundisho kwa wapinga maendeleo wote.
Sijui hizi akili mnazitoa wapi. Wewe lazima ulibemendwa. Lete hoja yenye mashiko. Nyeti za nyumbu na upepo vina uhusiano gani? Acha ujinga.
 
Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
701
500
Ni jukumu la wananchi kulinda kura zao siyo jukumu la CDM! Wanaoibiwa kura ni wananchi wenyewe.
siasa sio mwananchi, siasa ni uongozi na uongozi unao weza kubeba agenda muhimu za wananchi kama chama kinajali wapiga kura wao.

Leo hii hakuna siku Mbowe au Chadema waligawa pesa japokuwa walipewa ruzuku ya mabilioni na serikali.

usiwa vike vilemba vya ukoka wapiga kura.
 
moshdar

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
1,833
2,000
Hawa CHADEMA wana mtandao mdogo hasa vijijini kulinganisha na Chama Cha Mapinduzi katika nchi hii kubwa kieneo na utawala. Hivyo, ni ndoto kupata mawakala wa kutosha kila kituo cha kupigia kura; labda mapindikizi kwa maeneo ya vijiji; tofauti na katika miji na tena wakishirikiana na vyama vingine.

Kwa mfano ukifatilia CCM wana mabalozi wa nyumba kumi kila kona ya Tanzania wanaowatambua watu wao na kuhakikisha watapiga kura kwao; tofauti na vyama vya siasa vinavyoishia katika miji na vijiji vichache. Pia wana mtaji wa viongozi wengi wa serikali za mitaa na vijiji wanaotumia kuhakikisha ushindi wa uhakika.
chadema mi msingi imeenea kila pembe nchi hii.
viongozi wa serikali za mitaa wengi wao ni mapandikizi ambayo hayakuchaguliwa na wananchi, hayakubaliki kwa wananchi na wanachi huwa hawayasikilizi.
 
sysafiri

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
256
250
siasa sio mwananchi, siasa ni uongozi na uongozi unao weza kubeba agenda muhimu za wananchi kama chama kinajali wapiga kura wao.

Leo hii hakuna siku Mbowe au Chadema waligawa pesa japokuwa walipewa ruzuku ya mabilioni na serikali.

usiwa vike vilemba vya ukoka wapiga kura.
Kumbuka wananchi ndiyo wanaoenda kupiga kura kuchagua chama kitakachoongoza serikali yao! Sasa kama Serikali na vyombo vyake watapora haki yao ya kuchagua chama wanachokitaka wana haki hata ya kuandamana kudai haki yao!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom