Uchaguzi 2020 CHADEMA mkiweza kulinda kura ambazo Watanzania tutawapigieni, basi Ikulu ni yenu

Nina elimu kubwa sana ndugu yangu; tatizo ni kuwa walalamikaji wengi kama wewe hukimbilia kusema "tume huru" bila kujua maana yake bali kutumia maneno hayo kama scapegoat ya kulalamikia maamuzi ya tume ile. Maana halisi ya tume huru ni kuwa iko pale kwa mujibu wa sheria na inafanya kazi kwa mujibu wa sheria- yaani kuna sheria zinazotawala utendaji kazi wa tume ile. Wanachama wa tume hiyo ni watanzania wenzetu walioteuliwa kuwa kwenye tume hiyo kufuatana na katiba, na wanafanya kazi kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo. Sasa wewe unapoidscredit kuwa siyo tume huru maana yake ni kuwa haikuundwa kwa mujibu wa sheria bali ilindwa na mtu mmoja kwa manufaa yake tu na wala haifuati sheria za nchi. Kuna haja kubwa ya kuelewa unalodai kuliko kudai maneno tu. Kabla ya kufikia madai ya tume huru inabidi pia ufikirie pia kama tuna bunge huru na mahakama huru chini ya definition yako. Conclusion kuwa hatuna tume huru, ni mwendelezo wa kuwa hatuna mahakama huru na hatuna bunge huru, na hapo ndipo unapofikia kisiki; kwani maana yake ni kuwa hakuna structure katika uongozi wa nchi, jambo ambalo binafsi sikubaliani nalo.
"mshahara nikulipe, gari nikupe halafu umtangaze mpinzani kashinda? by jiwe akiikemea TumeCCM.
kumbuka alitamka hivo akiwa Rais na sasa yeye ni mgombea na ni mteuzi wa hiyo Tume...
dah!!
 
"mshahara nikulipe, gari nikupe halafu umtangaze mpinzani kashinda? by jiwe akiikemea TumeCCM.
kumbuka alitamka hivo akiwa Rais na sasa yeye ni mgombea na ni mteuzi wa hiyo Tume...
dah!!
Tume inalipwa na serikali kwa mujibu wa sheria na bajeti iliyopitishwa na bunge, hailipwi na CCM!
 
Tume inalipwa na serikali kwa mujibu wa sheria na bajeti iliyopitishwa na bunge, hailipwi na CCM!
sasa kama ndivyo hiyo jeuri anaipata wap ya kuitishia Tume eti ikimtangaza mpinzani itakiona cha mtema kuni!!!!
 
Naendelea kuyaamini kwa dhati maneno yako mkuu....
Tuko tayari kulinda kura zetu
 
Yaani mpoteze rasilimali za chama kulinda kura 200,000 za Lissu dhidi ya 18,000,000 za ccm. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha
 
Yaani mpoteze rasilimali za chama kulinda kura 200,000 za Lissu dhidi ya 18,000,000 za ccm. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha
2015 ccm Tulishinda kwa bao la mkono..by mwanaccm na mgombea ubunge kwa tiketi ya hiyo hiyo ccm nape nnauye

Uchaguzi ukiwa huru na wa haki ccm ijiandae kukabidhi ikulu...by Katibu Mwenezi wa CCM "TAIFA" na mmoja wa waratibu wakuu wa kampeni za uchaguzi za hiyo hiyo ccm.
 
Hivi mnaposema Chadema ni wapinga maendeleo mnatumia akili au kufuata upepo wa kauli za mropokaji wenu?
Hivi Chadema na CCM nani anawanachama na wafuasi wenye maendeleo binafsi, elimu na ukwasi?
Sasa iweje hao wenye hadhi hizo ndio wawe wapinga maendeleo ndio wenye nafuu ya maisha na hao kondoo wenu masikini ndio wapenda maendeleo?
Jiwe kawafanya wapumbavu sana
MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI ZANZIBAR AKIOMBA KURA PEMBA

Bonyeza link hiyo chini kuona shamra shamra zote zinazoendea. Hakika ni Neema tupu kuwa na Dr Hussein Mwinyi
 
Aijipii alisha toa tahadhari kwamba, kulinda kura ni kazi ya jeshi la polisi. Hivyo alisisitiza kwamba waTazania wajiepushe na kujiingiza kwenye matatizo yasio ya lazima.
Shida sio kazi ya IGP. Shida ni kujenga imani kwa watanzania kwamba watatenda haki. Matumizi makubwa sana ya nguvu sometimes sio lazima
 
Aandae mawakala wasio na njaa wala taamaa ili wasije kupokea mlungula toka maccm
Majimbo ambayo chama tawala wamepita bila kupingwa nawashauri vyama vya upinzani kwenye kura za urais waweke mawakala wenye ngozi ngumu, Kuna mambo huwa yanafanyika hata Shetani anashangaa Mf Jimbo la Bumbuli ni uchochoro wa kupitishia kura chafu za rais upinzani msiseme hatukuwaambia.Kwa mfano eti jimbo linawapiga kura laki mbili ila kula za rais zimepigwa laki sita duh.
 
Shida sio kazi ya IGP. Shida ni kujenga imani kwa watanzania kwamba watatenda haki. Matumizi makubwa sana ya nguvu sometimes sio lazima
Minafikiri, hata kama aijipii atatoa angalizo kwa nia njema....
Lakini kwasasa tayari wananchi wengi hawana imani na jeshi hilo, and tayari akili za wanachi wengi zinekwisha jijengea kwamba jeshi litatumika kukikinda chama kilichopo madarakani pamoja na maslahi yake.
 
Majimbo ambayo chama tawala wamepita bila kupingwa nawashauri vyama vya upinzani kwenye kura za urais waweke mawakala wenye ngozi ngumu, Kuna mambo huwa yanafanyika hata Shetani anashangaa Mf Jimbo la Bumbuli ni uchochoro wa kupitishia kura chafu za rais upinzani msiseme hatukuwaambia.Kwa mfano eti jimbo linawapiga kura laki mbili ila kula za rais zimepigwa laki sita duh.
Hatari sana iyo comrade, tunaomba ushahidi au ni mfano tu umetoa?
 
CHADEMA, na wapinzani wote kwa ujumla, kila dalili inaonesha nyie ni zaidi, mshindani wenu Mkuu CCM anaonesha kila dali ya uoga, kutokujiamini na kukata tamaa. Hana uwezo tena, anajishika na kila aina ya tawi mpaka matawi wasanii, matawi malori, matrekta, mabasi, kuhonga nauli bali hayo matawi kamwe hayaoneshi kufua dafu popote. Tawi pekee la kuwatisheni CHADEMA ni ile kauli ya mshindani wenu mkuu kuwa "nimekupa cheo mshahara mzuri halafu umtangaze mpinzani?! utanitambua"

CHADEMA ni Hiyo kauli pekee tu ndiyo ya kuishughulikia kwa sasa. Pangeni vizuri ishu za mawakala wenu, zichambueni vilivyo teknikalitizi za ujanja ujanja na wizi wa kura, tumieni kila mbinu halali ndani na hata nje ya nchi, msianzishe fujo lakini kamwe kamwe asilani msikubali tena kugeuza shavu la pili, msikubali tena kumwachia Mungu, watayarisheni vilivyo wapiga kura wote Bara na Visiwani, hata wanaccm ambao dalili zinaonesha wengi wao watakupigieni kura kisirisiri, wajiandae kukataa kura zao kuchakachuliwa na Tume isiyo huru ya uchaguzi. CHADEMA mkiweza hilo historia mpya inakwenda kuandikwa tarehe 24 Oktoba 2020.

Washirikisheni wananchi wote wa Tanzania na Pambaneni mpaka tone la mwisho. Wananchi wa Tanzania wapo nyuma yenu, nyinyi pamoja na ACT Wazalendo (kwa upande wa Zanzibar) ndo tegemeo letu pekee wana wa nchi hii lililobaki, tarehe 24 oktoba ni nafasi ya dhahabu (golden chance), itumieni vema.

Mungu ni mwema Wanamageuzi, kuna kila dalili nchi Itakombolewa Oktoba mwaka 2020.


Hawa CHADEMA wana mtandao mdogo hasa vijijini kulinganisha na Chama Cha Mapinduzi katika nchi hii kubwa kieneo na utawala. Hivyo, ni ndoto kupata mawakala wa kutosha kila kituo cha kupigia kura; labda mapindikizi kwa maeneo ya vijiji; tofauti na katika miji na tena wakishirikiana na vyama vingine.

Kwa mfano ukifatilia CCM wana mabalozi wa nyumba kumi kila kona ya Tanzania wanaowatambua watu wao na kuhakikisha watapiga kura kwao; tofauti na vyama vya siasa vinavyoishia katika miji na vijiji vichache. Pia wana mtaji wa viongozi wengi wa serikali za mitaa na vijiji wanaotumia kuhakikisha ushindi wa uhakika.
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom