Mheshimiwa Judi wa Kishua,
Nakuomba usome tena mchango wangu juu ya Tume ya Katiba. Hakuna mahala popote nimesema CDM wapinge na tuendelee na maandamano, eti kwa vile Tume ina Waislamu wengi.
Nilisisitiza kuwa J.K. alizingatia Katiba ktk kuteua Wajumbe. Katika conclusion nilishauri kuwa hata baada ya kupata Katiba Mpya, itabidi Tanzania iendelee na mjadala ili demokrasia ya kweli iweze kupatikana nchini mwetu. Kuna rafiki yangu mmoja amenipigia simu akisema kwa sasa tutaendelea kuwa na mfumo ambao "The tail wags the dog, rather than the dog wagging the tail".