CHADEMA, mchukueni HAMADI RASHID

SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
195
Wakati umefika wa CDM kutafuta namna ya kujiimarisha kule Zanzibar,kwangu mimi Hamad Rashid atakuwa ni kete nzuri sana kwa cdm katika kukijenga chama kule Zanzibar, hivyo nashauri cdm tumchukue huyu jamaa,maana sijaona dhambi kubwa aliyofanya.Critical /Great thinkers watatoa maoni ya kujenga na si matusi.

Wana jf mnasemaje?
 
Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
500

CHADEMA kinajengwa kwa kujenga sera zake,kuelimisha watz na kuwafanya watz kuona chama ni mali yao.Chadema hakihitaji watu wanaotoka ktk vyama vyao kwa vurugu ili kujijenga.Chadema ni zaidi ya viongozi,wao wanapewa jukumu kla kuongoza wala si kwamba chama ni mali yao.Hamad Rashid hatumuhitaji ili kujijenga Zanzibar,kwa chadema ni busara kuwaacha wazanzibar kuwapa fursa ya kuelewa sera za chama na itikadi za chadema na wao kuchagua kujiunga kwa ridhaa yao na si kwa kulazimishwa na Mtu,maana akiondoka ataondoka nao.

So chama hakijengwi kwa majina ya watu bali kwa uzalendo wa wanachama.Nadhani hoja hii inakosa uzito wa kimjadala kwa manufaa ya chama na Tanzania tuitakayo!
 
FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Umnajua tatizo moja vijana wa chadema hamjiamini kabisa Hamadi rashidi wa nini sasa naamini tuna wazanzibar wazuri wenye nguvu kuliko hamad.

Niweke wazi sipendezi na vijana hata wazee wanaotoka chama fulani baada ya kutoswa kwenye uchaguzi hao hawatusaidia tatizo letu ni moja tunapenda sana majina.

Tujiulize zitto kabla ya 2005 kuna aliye mjua,Dr slaa naye je,kina mnyika kina mdee tutengeneze watu wetu kukumbatia oil chafu haifai jiulize walikuwa wapi siku zote kuona chadema inafaa.

Mimi nimejiunga na chadema 2009 nikiwa na miaka 19 hakuna yoyote aliyenijua wakati nachukua kadi niliumizwa kuona vijana wachache wanapambana peke yao.

Wengi wanaoingia sasa wengi wanatafuta madaraka tujiulize ole millya angepita kwenye kura za maoni ccm leo angekua chadema tunapokea oil chafu nyingi sana ndani ya chama si maana ole millya ni oil chafu,je shibuda angepita kura za maoni.

Tunahitaji kujenga chadema bila kutumia majina ya watu wakubwa chadema ijengwe na sisi kina fredy,hamis,haruna,juma wala tusiwatumie kina mnyika wala mdee waje kutusaidia.

Wewe kama una uchungu wa kweli kuishika zanzibar na imani hakuna ngome ngumu duniani kupitika unahitajika ubunifu kidogo tu kuipenya zanzibar.

Naomba mnipe wiki mbili nitakuja na mbinu za kuiteka zanzibar weka kichwani huhitaji jina kubwa na mtu mkubwa kupenya sehemu sera zetu,hoja zetu na ilani bora ya uchaguzi zitatupenyesha zanzibar.

Je zitto alipoenda kigoma ya kaskazini alikua na jina kubwa maswali ya kujiuliza kina wenje,mnyika je walikua na majina.

Naamini kuna vijana wengi sana wazuri kuliko Hamadi wanahitaji muda na kujengwa tuna yule mbunge wa viti maalumu kutoka huko sema naona naye yuko kimya sana.

Fred kavishe
 
Kimagege

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
283
225
ni vizuri umejaribu kufikiri lakini mm naona huyo bwana ana tamaa kubwa ya madaraka na pia ana ndimi mbili.ni muhimu kukumbuka kuwa aliwahi kuteuliwa na mkapa ua mbunge sasa kama unataka kuiondoa ccm na unataka kuwatumia watu wanoishi kwa fadhila za ccm utakuwa unachekesha.
 
S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,408
2,000
Wakati umefika wa CDM kutafuta namna ya kujiimarisha kule Zanzibar,kwangu mimi Hamad Rashid atakuwa ni kete nzuri sana kwa cdm katika kukijenga chama kule Zanzibar, hivyo nashauri cdm tumchukue huyu jamaa,maana sijaona dhambi kubwa aliyofanya.Critical /Great thinkers watatoa maoni ya kujenga na si matusi.

Wana jf mnasemaje?
Mimi naona huyu aende kwa akina magamba pengine anaweza kuwasaidia wao. Huku CDM ataleta giza tu.
 
SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
195
Majanikv Mkuu cdm imeanzishwa mwaka gani na hadi sasa imeshindwa kupenya vilivyo kule zanzibar.Wakati mwingine tuangalie hasara iliyo ndogo.
 
Last edited by a moderator:

FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Mkuu cdm imeanzishwa mwaka gani na hadi sasa imeshindwa kupenya vilivyo kule zanzibar.Wakati mwingine tuangalie hasara iliyo ndogo.

Chama kimeanza 1992 kumbuka hakikusimamisha mgombea wa uraisi hadi 2005 na 2010 na 2005 chama ndo kidogo kilikua na viti vingi cha slaa,zito,ndesa,afri kabla ya 2010 kupata viti zaidi 23 kwahiyo chama kinakua.

Mimi naaimani kabisa zanzibar tutapenya kabla ya huu muda lakini pia kimahesabu zanzibar kura zinagaiwa kwa cuf na ccm nusu nusu kwa hiyo si eneo muhimu la ushindi kwetu kivile kama cuf itakufa tutaingia zenji.

Tunahitaji kuwekeza nguvu kwenye maeneo yenye kura nyingi kanda ya ziwa,dsm,kaskazini,mbeya+iringa,
 
mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
1,195
Hamad Rashid kwa Zanzibar hana mvuto na ndio maana anaogopa hata kukanyaga, nawashauru CHADEMA kama munataka mtu mwenye mvuto na Wazanzibari ni vyema mukamchukua na Amani Karume CCM hawamtaki tena na ndio maana wameamua kumchania picha zake.
 
Kiutawala hatutakiwi kuipuuza Zanzibar.Kumbuka sasa cuf na ccm ni nusu kwa nusu,na unaweza kuona matatizo yaliyopo,je tukiichukua nchi 2015 kama ccm hawatatumia uhuni(God forbid),huoni ya kuwa kiutawala itakuwa ngumu sana kwa serikali ya cdm kui-manage znz? Au wewe unaonaje?
 
Hatutaki mtu asiyekubalika nyumbani.Kumbuka tunajenga chama,hivyo labda akijiunga tu kwa hiari yake lakini si kuombwa kujiunga.Sijafika znz na hivyo siwezi kuzungumzia mvuto wa hamad huko,ninachoelewa ni kuwa ni kati ya wabunge wenye ushawishi na ni miongoni mwa walioshinda kwa ushindi mnono.Lakini pia ukimlinganisha na waznz wengi anaoneka kuwa walau ana hoja.
 
THE STRONG

Senior Member
Jan 21, 2012
107
195
mi sioni huyu jamaa kama anafaa sana kwa cdm because huyu jamaa ana uchu sana wa madaraka so asipochaguliwa atahama sio mtu mzuri kwa msimamo wa chama
 
FredKavishe

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,090
1,195
Kiutawala hatutakiwi kuipuuza Zanzibar.Kumbuka sasa cuf na ccm ni nusu kwa nusu,na unaweza kuona matatizo yaliyopo,je tukiichukua nchi 2015 kama ccm hawatatumia uhuni(God forbid),huoni ya kuwa kiutawala itakuwa ngumu sana kwa serikali ya cdm kui-manage znz? Au wewe unaonaje?

Sijaipuza zanzibar ni muhimu sana kwetu nipe week mbili niandae kitu cha kuikatamata zanzibar mkuu sawa halafu kama una vijana wa chadema unawajua wa huko utaniambia uwape ndo uwe muongozo huwezi tegemea kina mbowe kila kitu
 
SAGANKA

JF-Expert Member
Jun 9, 2012
313
195
mi sioni huyu jamaa kama anafaa sana kwa cdm because huyu jamaa ana uchu sana wa madaraka so asipochaguliwa atahama sio mtu mzuri kwa msimamo wa chama
Huoni kwamba akihama atatuacha na wanachama kwani tayari umakini wa cdm utakuwa tayari umeonekana zanzibar kwa kiwango kikubwa.Tumikia kafiri upate mradi wako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom