Mimi nimesoma magazeti mwananchi, the guardian na daily news nimeshtushwa na kauli ya Mbowe. Mimi nilihisi lazima atakuja kuilemba lemba kitendo cha kutoka nje ya bunge, moja wapo ni maslahi bainafsi na kupenda vya dezo ambayo ni kila nmwanasiasa hata kwa wale wasiona wanasiasa na wale ambao wanajifanya kuwa na misismamo mikali hata pata JF hasa wale wachadema.
Mbowe baada ya kupata habari kuwa CCM itapeleka hoja ya kuwatoa katika uongozi wa upinzani,
- ameogopa kukosa gari ambalo halina namba limeandika KUB ambalo ni ishara ya 'ukubwa' kila takapo pita
- pamoja na dereva
- atakosa ofisi kubwa tu aliyopewa na
- wafanyakazi na stationaries
Vyote hiyo kwa gharama ya mlipa kodi na marupurupu kibao yanayoendana na nafasi hiyo. Kama ambavyo mawaziri wanavyotanua. Pamoja na kwamba yeye kama F. Mbowe anapesa za kumtosha lakini hana tofauti na wanasiasa wengine wanaopenda ukubwa na marupurupu yake.
Nilijua na niliona ni kiini macho kumkataaa rais wakati unaendelea kutumikia bunge ambalo rais ni mmoja wa wabunge kulingana na katiba ya jamhuri ya muungani wa tanzania,
Unamkataa rais wakati unaendelea kula posho na kuchukua magari ya ubunge. Kweli ilikuwa danganya toto, sasa Mbowe anasema hawamkatai rais ila walitaka tu kupeleka ujumbe basi hivyo wanataka waongee na serikali ya Dr. Jakaya Kikwete wayamalize mapema ili CCM wasije kuwaondoa kwenye uongozi wa upinzani maana tayari mbowe ameunda baraza la mawaziri kivuli anasuburi tu Rais JK atangaze la kwake nayeye afanye mabadiliko kidogo kulingana na Rais JK alivyounda wizara zake.
Ama kweli siasa ni kiini macho kikubwa, wakereketwa wa chadema wenye kupinga kila kitu ambacho hakiendani na chadema ama kinaelekea upande wa ccm baadhi yao hawaamini na watakuja na kauli kali na wale wa kutukana kwa kukosa ustaarabu watatukana ila ukweli ubaki pale pale "never trust a politician" they always change and refine statments to justify their interests and keep on saying " we do not have permanent enemy or friend, "your big enemy in the morning will turn to be a big friend in the afternoon."