CHADEMA, Lowassa apewe onyo mara moja

Nikweli, hizi "NIME", "NITA" hazifai kwa afya ya Chama chochote.
Ila kwa sasa Lowassa ana jifariji baada ya kuporwa ushindi. Mimi naamini baadae ata tulia na kurudi kwenye mstari.
Fact
 
Hayakuhusu hata kidogo wewe hangaika na kupiga rushwa ktk chama chenu kilichoelemewa na wala rushwa na mafisadi.
 
CCM walifanya kazi kubwa sana kumdhibiti Lowassa na genge lake,kumzuia asiwe rais wa nchi hii haikuwa kazi ndogo. Tatizo la Lowassa hapendi kuwa chini,anataka awe juu ya wote wakati wote.Wakati alipokuwa Waziri mkuu alifanya kila namna kum_outshine Mkwere mpaka Mkwere akaonekana kama amewekwa na Lowassa madarakani,ikabidi Mkwere afanye maamuzi magumu ya kumchinjia baharini swahiba wake huyu la sivyo angelizwa.CHADEMA mlivyo wajinga mkaamua kuwasaidia CCM kuutua msalaba huu na kujitwika kichwani,haya kazi kwenu sasa.
 
huoni mbali. unapoelezwa mambo ya msingi, yachambue, yatafakari ndo ujibu. sio kukurupuka tu. angalia, utajamwagiwa mebendazole.
 

Kaka yangu unaumia bure bila sababu.Kitu kimoja kiweke kichwani BILA LOWASSA,MBOWE,LISUU etc inawezekana kuwepo au kuendelea kuwepo kwa CHADEMA lakini bila WANACHAMA CHADEMA haiwezi kuwepo aslani...............

Awe na nguvu ya aina yoyote lakini bila WANACHAMA ni kazi bure.Waweza mjibu pia BILA WEWE LOWASSA asingeiona CHADEMA.Kwanini upate shida ya kuwaza nakuumiza kichwa chako
 
Kwani ukinunua ng'ombe mwenye mimba si unanunua na ndama wake akizaliwa? Ndivyo ilivyotokea kwa CHADEMA na Lowasa. Kanunua chama na kila kitu kizuri kinachotokea kimetokana na ushawishi wake
exactly mkuu
 
me nadhani LOWASSA hawezi kutaka uongozi ndani ya CDM,uwaziri mkuu ulikua uongozi mkubwa sana hana njaa ya uongozi.mnaomshambulia mtakuja kushika vichwa pale chama kitakavyoanza kupaa zaidi ya hapa."time will tell"
 
Mjinga aliyekutuma mwambie hana akiri mtakesha sana kuimba lowasa njaa ndo zinawazumbua kisa buku 7
 
Basi mwambieni aunde chama chake aongoze zaidi mwaka 2020
Kwani wewe CHADEMA ni chama chako? Katiba na sheria zinampa mtu uhuru wa kushiriki siasa kupitia chama anachokitaka.

Mimi nashauri kwa vile ACT haikukidhi matakwa ya hujuma za CCM anzisheni chama kingine chenye ujinga unaokidhi matakwa ya CCM.
 
Well said, ila wale watoka povu wataendelea kuropoka kama kawaida yao! Kwa mpenda maendeleo ya TZ analijua enzi za EL zishaisha n wakati wa CHADEMA na UKAWA kukaa chini na kujipanga upya
 

Well said mkuu, hapo hakuna cha COLLECTIVE RESPONSIBILITY/LEADERSHIP kila kitu kimegehuka kuwa a ONE MANSHOW na inaonekana yuko determined ku-run SOLO kila kitu ndani ya chama, anataka vile vile achukuliwe kama yeye ni Alpha na Omega - hizi si dalili nzuri kwa mstakhabali wa CHADEMA tukiwa wakweli.
 
Ameruhusiwa kutumia NIME kwa sababu ametoa pesa nyingi sana chamani.....inampunguzia machungu.
 

Inaonesha una uelewa wa mambo, hebu tusaidie ni kipi kimemnyamazisha Maembe, February mawaya, Usisahau kutoa salamu za pole kwa EDO FIL KU ENJO.
 
CHADEMA kinapaswa kuwa chama cha kitaifa unless wewe ni mbumbumbu wa siasa au unatoka kaskazini

Kama hadi leo hufahamu kuwa chadema ni chama cha kitaifa , sio kosa lako tatizo ni chama chako kukunyima elimu.

Na sisasa zako za maji taka. Pandu kificho wewe.
 
Binafsi kama kuna mwanasiasa ninae mwona yupo very creative basi mwanasiasa huyo ni Freeman Aikael Mbowe; kupitia uongozi wake ndio kwa mara ya kwanza Chadema kimesimamisha mgombea Uraisi, kabla hajawa mwenyekiti wa hiki chama Chadema walikua wanaunga mkono vyama vingine. Kila uchaguzi mkuu unapofika amekua anatoa changamoto kubwa na mpya si kwa wapiga KURA tu bali hata huko ccm kwenyewe; nani asiyejua kilichotokea mwaka 2010. Wakiwa kwenye kikao chao cha kumtafuta mgombea wao wa uraisi (Ikumbukwe mwenyewe Mbowe aliisha sema mapema kua hatagombea urais tena) mara aliyekua katibu mkuu wa Chadema akapatwa na safari ya kwenda jimboni kwake akikiacha kikao kinaendelea, wengi tulijua Samuel John Sitta angegombea urais kupitia Chadema kwasababu mzee huyo alipatwa na matatizo makubwa ya uanachama wake wakati wa awamu ya kwanza ya JK, mara huyo Dr. Wilbrod Peter Silaa akatangazwa kua mgombea wao, hi kitu kwa wenye kumbukumbu nzuri (na wawe wanasema ukweli) ilileta shida sana ndani ya ccm na hata baadhi wakasikika wakisema kua kama wangejua Chadema watamsimamisha Dr. Silaa na wao wangetafuta mgombea mwingine na sio JK, well yote yalipita na again ukaja mwaka 2015, kama kawaida yake Mbowe, kawa kimya tu, upande wa Cuf wao tayari walimtangaza Profesa Lipumba kwamba angegombea lakini Chadema kimyaaaa, dalili zilikua zinaonesha kua Dr. Silaa angesimama but Dr mwenyewe aliwahi kusikika mara kadhaa huko nyuma akisema hatagombea tena nafasi hiyo; hakuna aliyejua kama Lowassa angechukuliwa Ukawa (Chadema) Sina hakika uchaguzi wa mwaka 2020 nani atakua kiongozi wa Chadema lakini kama ikitokea Mbowe ndio atakua still kiongozi siwezi shangaa akija na mbinu mpya. Huyu jamaa ni genius sana kwenye level ya siasa. Kwangu mimi bado nampongeza sana yeye na sio mwingine; tukiwa wakweli hata hao waanzilishi wa ACT ni product yake, I mean umaarufu wao una mikono ya Mbowe, Mbowe amekua na mchango mkubwa sana wa wao kufika hapo walipo.
 
Lakini kuna kaukweli kwamba kama si lowasa isingekua rahisi chadema kuzoa kura zaidi ya ml 6 na kukamata jiji la dar. Magufuli hata yeye kwenye mabango na hotuba zote alisisitiza chagua Magofuli na serikali ya Magufuli itafanya kadha. Watu walipiga kura za urais kipindi hiki kwa kuangalia zaidi wagombea na si vyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…