SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,841
- 1,843
Chadema ilikuwepo kabla ya Lowassa kuhama CCM, na tena ilikuwa ni chama imara, pendwa na chenye nguvu na ushawishi wa kutosha, hasa katika miji mikubwa ya Tanzania.
Hata Ukawa iliasisiswa kabla ya Lowassa kukatwa na kuhamia CDM. Kwa misingi hii hamna mtu anayeweza kuja na takwimu halisia eti bila Lowassa mambo yangekuwaje UKAWA?? Kama yupo azilete.
Hoja yangu ni hii;
Lowassa mpaka sasa amegeuza kila aina ya mafanikio ya UKAWA kuwa yake binafsi na kujinasibu kuwa yeye ndo ameyaleta. Amekuwa akijinasibu kwa kauli za kujisifia binafsi kana kwamba Chadema na Ukawa havikuepo na yeye ndo alikuja kiuasisi Chadema na muungano wa Ukawa.
Kauli za Lowassa zinakiweka chama mikononi mwake, na si mikononi mwa wanachama waliosumbuka kukijenga chama hiki kwa machozi, jasho, damu, vifo, njaa, na kudhalilishwa na Nguvu za Dola.
Mfano wa kauli za Lowassa;
Swali ni je, kwanini hizi "nime" zisiwe "chama kime"? Halafu toka lini Lowassa amefuta taratibu za kumpata mgombea urais ndani ya chama na kujihakikishia nafasi ya kugombea uchaguzi mkuu 2020??
Lowassa apewe onyo, na afunzwe kuwa siasa ni collective and intergrated efforts na sio One man show or else mtwambie kama amekabidhiwa chama mikononi mwake, na lini ilifanyika hivyo.

- "Nimewawezesha wapinzani kufikisha wabunge zaidi ya 100, tukiweka na viti maalum"
- "Nimewasaidia kushikilia jiji la Dar es salaam"
- "Nitagombea 2020, najiandaa na uchaguzi mkuu "
- "Nimeufanya upinzani kuwa na nguvu kuliko wakati wowote"