CHADEMA, lini mtajifunza kuacha kukurupuka?

CHADEMA, lini mtajifunza kuacha kukurupuka?

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Posts
8,271
Reaction score
9,114
Kila mara ni matamko na mihemuko isiyo na impacts yoyote, hili hamjifunzi?, mnategemea wazungu wawasaidie?, "shame"

Toka muanze kususa nini kimebadilika?

Siwezi taja matamko na mihemuko yenu iliopita na haikuzaa matunda,kwani inajulikana wazi na kila mtanzania.

Ona sasa mmetegwa kwa pumba kirahisi mkakamatika.
Kilichofanyika ni nyie kutangulizwa chambo,ili ionekane Kama mnaweza kula matapishi yenu.
Utaratibu wa kisheria upo wazi kabisa wa namna ya kutatua kero za uchaguzi.hili halina ubishi.

Rejeeni tamko la Lipumba,lipo kijanja Sana,Ina maana serikali inaweza kufanyia kazi maombi yao ili mkaangwe,hali kadhalika ACT Wazalendo,sidhani kama wataungana nanyi.
Mmemsikia waziri mwenye dhamana, katoa ufafanuzi mzuri Sana wa namna ya kufanya kwa asie ridhika na maamuzi,

Sasa ngojeni serikali iyafanyie kazi maoni ya kina Lipumba na Zitto tuone kama mtakana maapizo yenu.

Njia ya kususa haijawahi fanikiwa,jirekebisheni,inawezekana mnahujumiana nyie wenyewe ndani ya chama chenu.
 
Tuwe wakweli Chadema imetolewa kwenye uchaguzi au imejitoa?
 
Tunajua CCM imeumia sana baada ya CHADEMA kujitoa. CCM watawashawishi hivi vyama vidogo wasijitoe wajifanye wanaenda mahakamani halafu rufaa zao zote, wote wapewe ushindi kisha warudishwe kuwa wagombea kamili na wale wa chadema kule vijijini watarudishwa kimyakimya,baada ya CHADEMA kujitoa, unajua sasa hivi kinachofanyika ni sawa na Liverpool wakutane Anfield na Twiga stars kutafuta mshindi wa kuchukua kombe
 
Back
Top Bottom