Ndugu ThinkTwice
Mkwawa, Mirambo, Mputa,Rumanyika, Mangi Sina, Mandara, n.k walikuwa viongozi wazuri na hawakuwa na shule yeyote leader is born, and we all have such ability naturaly because real leadership starts at home!
Hivi yule Mbunge wa CCM jimbo la Rolya ni darasa la ngapi eti?Ndio maana mkawafanya watanzania wajinga kuwaletea darasa la 7, SHAME ON YOU !!
Tangia kampeni kuanza za uchaguzi mkuu, Ndg. Slaa alikuwa peke yake kwenye kampeni bila ya kusaidiwa na Mgombea mwenza, tofauti na vyama vingine, je huu sio ubinafsi?. Na habari za uhakika zilizozopo ni kuwa Mgombea mwenza wa Slaa alikuwa na elimu ya darasa la 7 tu, ili hali yeye mwenyewe alikuwa anahubiri elimu ya awali iwe ni form six. Hivi alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa anakimaanisha kweli ? inakuwaje utuletee mgombea mwenza wa darasa la 7 ili hali wewe wahubiri elimu ya awali ni form six ?. Huu ni upotoshaji dhahiri ambao CDM waliufanya kwa wananchi, na yaonyesha Slaa alichokuwa anakisema sicho ambacho angetenda endapo angepata urais. Bora Mungu alituepushia mbali mtu huyu !
Magazeti yote ya leo yameandika kilicho jiri kwenye mkutano wa wabunge wa CHADEMA uliofanyika kule Bagamoyo. Tutizame yaliyojiri kwa ufupi :
Kwa hali hii CHADEMA kweli ni shwari au ni kauli za kisiasa tu ?
- Shibuda kukwidana na Wenje na kutangaza rasmi kuwa atakwenda mwanza kumshitaki kwa wapiga kura kuwa mbunge wao hana adabu , na aheshimu wazee wa kisukuma
- Zitto kabwe kungolewa katika nafasi ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni
- Wabunge wa CHADEMA kugawanyika kuhusu kususia hotuba ya JK
- Shibuda atishia kukihama chama na kusema ushindi wake wa Jimbo la Maswa ulitokana na umaarufu wake na wala siyo CHADEMA
- Shibuda awaambia CHADEMA haina haja ya kudai katiba wakati chenyewe hakiendeshwi kwa kufuata katiba
- Shibuda amwambia Lissu kuwa hana sababu ya kuwashambulia wenzani kwani hata yeye anayo maovu mengi ambayo watu wanayajua ingawa hawayasemi
- Godbless Lema amwambia Shibuda kuwa ni pandikizi la CCM kwa kuwa anatambulika hivyo mkoani Arusha
- Shibuda aamini kuwa CHADEMA si Chama, bali ni kikundi cha watu, waliokuwa na misimamo yao kutoka nyumbani, na hawako tayari kujadiliana
Hivi inawauma nini? Kajichimbieni huko CCM.Chadema hakuna ushwari. Mbowe na Slaa, kwa kuwa hawa wote ni system, wameshapewa amri ya kukisambaratisha. Amini usiamini. Vyama vya siasa Tanzania vichukulie kama Simba na Yanga, walaaa usiwe na hamasa.
Hivi inawauma nini? Kajichimbieni huko CCM.
Mie niliisha yasema haya kitambo kuwa kwa mizizi hii ya CHADEMA wanayo iotesha ya kutumia udini, ukabila, upendeleo na ubinafsi katu hawawezi kuwa chama sahihi cha kisiasa cha kuiondoa CCM madarakani. Kwa hii hali CCM itatutawala milele. Na haya mliyo yaona ni ya firauni tu , ya Mussa yanakuja, wait !!!