CHADEMA, kwanini Dr. Slaa hachukuliwi hatua?

CHADEMA, kwanini Dr. Slaa hachukuliwi hatua?

Mkuu, wewe una kompyuta na keyboard yako ipo sawa, kwanini usianzishe thread kuhusu mada ulizozitaja?

Mimi nachofahamu wahusika wote wenye hizo tuhuma walijiuzuru, sasa niweke thread ya nini?

Huyu Dr Slaa ambae mpaka sasa ni katibu mkuu wa CDM ingawa tuhuma kibao zina mkabili ndio yapaswa kuhoji!

hapo kwenye red kaka?
waliomuua Mwangosi wamejiuzulu?
walioua kule Morogoro na Arusha wamejiuzulu?
waliokamatwa na rushwa waziwazi wkt wa uchaguzi wa CCM wamejiuzulu?
wezi wa kagoda,meremeta wamejiuzulu?
mawaziri wakiohusika na rushwa wamejiuzulu?
mbona wapo na wanadunda hadi leo?
hata waliolazimishwa kujiuzulu si hao hao wanagawa zile pesa makanisani na misikitini?
kama dr slaa nae ana tuhuma na zikathibita atajiuzulu pia
Nape na kampeni yake ya kuwangoa mafisadi ndani ya siku 90 imeishia wapi?
mangula nae kadakia lakini akafyata mkia..
mkishajisafisha sasa ndio mtaonekana wasafi mbele ya upinzani.
CCM haijatoa borit bado haiwezi kuona kibanzi cha mwingine.
 
Hakuna jipya ni mwendelezo wa blah blah toka lumumba kwa udhamini wa ajira ya HAMY-D

Hizo unazotaja kuwa kashfa ndio zimekifanya Chadema kuwa tishio kwa ccm hadi mkaajiriwa kukesha JF kujaribu kukiokoa chama chenu cha kifisadi kinachoingia kaburini kila kukicha.
Kwa mtu anayetumia akili yake kufikiri na kutafakari huwezi kumdanganya kuwa umefanya uchambuzi wowote hapa zaidi ya muendelezo wa kampeni za propaganda mfu dhidi ya tishio lenu Dkt. Slaa!
 
Last edited by a moderator:
WanaJF!

Dhana hii ya kuwajibika na kuwajibishwa imekuwa ikielekezwa upande mmoja tu, nako ni CCM na serikali yake. Tena mara kwa mara mashinikizo yamekuwa yakitokea CHADEMA, kuwa serikali iwawajibishe viongozi wenye kasoro.

Lakini kama ilivyo ada, CHADEMA imesahau kwa makusudi kabisa katika kuwawajibisha viongozi wake hasa wale wenye muelekeo wa kukichafua chama.

Kwa mfululizo wa matukio haya yaliyo muandama Dr Slaa, kama CHADEMA kingekuwa chama makini basi kingemchukulia hatua Dr Slaa za kinidhamu kwa lengo la kulinda hadhi ya chama.

Mfululizo wa matukio yenyewe ni kama ifuatavyo;

1. TUHUMA YA KUKWAPUA MKE WA MTU. Hii tuhuma sio tu kwamba imemchafua Dr Slaa na Josephine, bali imechafua CHADEMA kwa kiasi kikubwa sana mbele ya jamii ya watu wenye heshima na wastaarabu.

2. TUHUMA YA KUMPA JOSEPHINE MAMLAKA NDANI YA CHADEMA. Hii pia imeshusha heshima ya CHADEMA kwani watanzania kwa sasa wanaona CHADEMA ni kama chama cha familia.

Haiwezekani mchumba wa katibu mkuu kupewa fedha za chama kwa ajili ya ziara za mikoani. Josephine ni nani mpaka akakague uhai wa chama mikoani?

3. TUHUMA YA KUJIKOPESHA FEDHA YA CHAMA. Hii tuhuma tangu imetolewa haijawahi kupatiwa maelezo, zaidi ya kupiga piga chenga. Hali iliyo pelekea CHADEMA kuonekana kama sio chama cha siasa bali ni 'saccoss' ya watu wachache.

Kwa tuhuma hizo na nyingine nyingi dhidi ya Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA, ingekuwa ni vyema kama chama kingechukua hatua za kinidhamu dhidi yake, hata kwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo ili chama kiweze kurejesha hadhi yake kwenye jamii, ambayo kimsingi kwa sasa hadhi ya CHADEMA imeshuka sana kutokana na matukio haya ya aibu.

Waambie CCM Kinana awajibishwe kwa kuwa anatuhumiwa kuua tembo na kusafirisha pembe zake, waambie CCM Kikwete awajibishwe kwa kuingiza nchi katika mkataba wa kinyonyaji unaogharimu nchi mabilioni ya fedha kila kukicha (IPTL), waambie CCM wamuwajibishe Mwigulu kwa kuwa anatuhumiwa kuwa gaidi, waambie CCM wamuwajibishe Kandoro kwa kuingiza mkoa wa Mbeya katika vurugu za wamachinga. nk. Waambie kila mwanaCCM ajiwajibishe kwa kuwa wameshindwa kutekeleza ilani yao.
 
WanaJF
Kwa tuhuma hizo na nyingine nyingi dhidi ya Dr Slaa kama katibu mkuu wa CHADEMA, ingekuwa ni vyema kama chama kingechukua hatua za kinidhamu dhidi yake, hata kwa kumuondoa kwenye nafasi hiyo ili chama kiweze kurejesha hadhi yake kwenye jamii, ambayo kimsingi kwa sasa hadhi ya CHADEMA imeshuka sana kutokana na matukio haya ya aibu.
Hakika utumwa wa kiakili ni mbaya sana,Watanzania wenzako tupo busy kujenga Tanzania tuipendayo,wewe upo busy kuchafua watu na kurudia ngonjera zile zile. Nakukumbusha kuwa wahenga walisema; Sow the Wind,Reap the Whirlwind.
 
Ama kweli ukiwa CCM akili yako inafanana na ile ya panya!Mnaendelea kuimba wimbo uliokwisha chuja wa dhana ya 'mke' wa mtu, wakati huu hata baada ya mahakama kuamua hakuna kesi!
Ingekuwa propaganda yenu hii ina mshiko JK wenu asingelazimika kutumia TISS, Polisi na majeshi kuiba kura ili amzidi Dr. Slaa!
Ni uwajibikaji upi mnaoutaka? mnahangaika na habari nyepesi nyepesi wakati nchi iko katika msiba wa kiuchumi kwa kuongozwa na majangili kina Kinana ambaye hajajiuzulu licha ya kukiri kuhusika kwa meli zake kusafirisha tani za meno ya tembo? Kuna uwajibikaji hapo?
Matokeo ya ujangili unaoratibiwa na CCM sasa tembo waliokuwa zaidi ya laki mbili na nusu miaka kumi tu iliyopita sasa wamepungua hadi makumi ya elfu! Na sasa mmehamia kuwamaliza simba baada ya hiyohiyo CCM kuwafuta faru kwenye ramani ya nchi na kuwauza twiga na pundamilia wazima wazima uarabuni ili mabwana zenu wakawafanye kitoweo na wengine wawafuge ili wapunguze "bughudha" za kufunga safari ili kuwaona wakiwa Mabyara, Ngorongoro au Mikumi!
Uwajibikaji si sera wala lugha ya kiCCM! hebu angalia; wauaji wa raia wasio na hatia kama Kamuhanda na yule mtekaji wa Dr. Ulimboka walivyotunukiwa vyeo! Mmoja sasa ni RPC wa Simiyu! na Kamuhanda ni DCP!
Bila shaka RPC wa Arusha karibuni atapewa cheo kikubwa kwa kuratibu na kutekeleza aliyoyatekeleza kwa maelekezo ya chama chake CCM.
Chini ya CCM ni unafiki kwa kwenda mbele na hakuna hata chembe ya kinachoitwa "uwajibikaji"
Ingekuwa CCM ni wawajibikaji Mwenyekiti wao angeshaunda tume ya kimahakama, inayoshirikisha wanasheria wa pande zote za vyama vya siasa na asasi za kutetea haki za binadamu kuchunguza utekaji nyara, kushambuliwa na kuuwawa kwa raia wasio na hatia Zanzibar, Morogoro, Iringa, Songea, Arusha na kwingine ambako serikali yenu ya CCM imetuhumiwa kuhusika!
Mnashindwa kuzungumzia uwajibikaji wa kwelikweli na kutubabaisha na ishu binafsi tena zilizo x-pire za 'mke' wa mtu ambazo viongozi wa CCM na serikali ndiyo sera zao na hawaishi kukamatwa ugoni au kupatikana na masahibu ya kuibiwa na malaya gesti; na yote hayo hupita bila ya wito wa kuwataka wajiuzulu! Badala yake, Rais ambaye ni "msikivu" kwa makada wake watembea ovyo huwapandisha vyeo na kuwapongeza.
Shame on you CCM! Your death is imminent.

nimepoteza muda wangu mwingi kusoma huu upuuzi Wako, afadhali ningecheza tu mwanangu
 
Back
Top Bottom