Mkuu, wewe una kompyuta na keyboard yako ipo sawa, kwanini usianzishe thread kuhusu mada ulizozitaja?
Mimi nachofahamu wahusika wote wenye hizo tuhuma walijiuzuru, sasa niweke thread ya nini?
Huyu Dr Slaa ambae mpaka sasa ni katibu mkuu wa CDM ingawa tuhuma kibao zina mkabili ndio yapaswa kuhoji!
Ama kweli ukiwa CCM akili yako inafanana na ile ya panya!Mnaendelea kuimba wimbo uliokwisha chuja wa dhana ya 'mke' wa mtu, wakati huu hata baada ya mahakama kuamua hakuna kesi!
Ingekuwa propaganda yenu hii ina mshiko JK wenu asingelazimika kutumia TISS, Polisi na majeshi kuiba kura ili amzidi Dr. Slaa!
Ni uwajibikaji upi mnaoutaka? mnahangaika na habari nyepesi nyepesi wakati nchi iko katika msiba wa kiuchumi kwa kuongozwa na majangili kina Kinana ambaye hajajiuzulu licha ya kukiri kuhusika kwa meli zake kusafirisha tani za meno ya tembo? Kuna uwajibikaji hapo?
Matokeo ya ujangili unaoratibiwa na CCM sasa tembo waliokuwa zaidi ya laki mbili na nusu miaka kumi tu iliyopita sasa wamepungua hadi makumi ya elfu! Na sasa mmehamia kuwamaliza simba baada ya hiyohiyo CCM kuwafuta faru kwenye ramani ya nchi na kuwauza twiga na pundamilia wazima wazima uarabuni ili mabwana zenu wakawafanye kitoweo na wengine wawafuge ili wapunguze "bughudha" za kufunga safari ili kuwaona wakiwa Mabyara, Ngorongoro au Mikumi!
Uwajibikaji si sera wala lugha ya kiCCM! hebu angalia; wauaji wa raia wasio na hatia kama Kamuhanda na yule mtekaji wa Dr. Ulimboka walivyotunukiwa vyeo! Mmoja sasa ni RPC wa Simiyu! na Kamuhanda ni DCP!
Bila shaka RPC wa Arusha karibuni atapewa cheo kikubwa kwa kuratibu na kutekeleza aliyoyatekeleza kwa maelekezo ya chama chake CCM.
Chini ya CCM ni unafiki kwa kwenda mbele na hakuna hata chembe ya kinachoitwa "uwajibikaji"
Ingekuwa CCM ni wawajibikaji Mwenyekiti wao angeshaunda tume ya kimahakama, inayoshirikisha wanasheria wa pande zote za vyama vya siasa na asasi za kutetea haki za binadamu kuchunguza utekaji nyara, kushambuliwa na kuuwawa kwa raia wasio na hatia Zanzibar, Morogoro, Iringa, Songea, Arusha na kwingine ambako serikali yenu ya CCM imetuhumiwa kuhusika!
Mnashindwa kuzungumzia uwajibikaji wa kwelikweli na kutubabaisha na ishu binafsi tena zilizo x-pire za 'mke' wa mtu ambazo viongozi wa CCM na serikali ndiyo sera zao na hawaishi kukamatwa ugoni au kupatikana na masahibu ya kuibiwa na malaya gesti; na yote hayo hupita bila ya wito wa kuwataka wajiuzulu! Badala yake, Rais ambaye ni "msikivu" kwa makada wake watembea ovyo huwapandisha vyeo na kuwapongeza.
Shame on you CCM! Your death is imminent.