CHADEMA kushinda uchaguzi 2025

Safari hii watapewa, kinachotakiwa ni wananchi kupiga kura nyingi kwa Cdm mpaka wezi wa kura waone aibu
Ukitegemea mwizi wa kura kuona aibu, utasubiri sana.
Njia pekee inayoweza kuhakikisha vyama hivi vya upinzani vinapata haki yao ni kukataa kwa njia zote, kura zao kuchezewa na mtu yeyote yule, hata awe polisi.
Chama kama kina wanachama wa kweli milioni sita, watashindwa vipi kuhakikisha kura zao hazichezewi?

Hakuna binaadam yeyote asiyetaka haki,; lakini ili kuipigania haki ni lazima mtu awe na ujasiri wa kufanya hivyo; na ujasiri unatokana na kuwa na viongozi wanaosimamia njia za kulinda haki hiyo.
 
Kwa Katiba ipi?
Kwa tume ya uchaguzi ipi?

Acha kuwafamya watanzania mazombi ?
 
CCM itaondolewa madarakani kwa amani 2025 , hii ni kwa sababu ya Katiba mpya na Tume Huru ya uchaguzi inayokuja , ccm bila Polisi hakuna kitu , hilo wewe unalijua vizuri sana
 
Eti kushinda uchaguzi....mshinde mara ngapi??
Ebu kuweni serious na mabadiliko ya msingi kabla ya haya mapambio yenu ya kutaka ushindi!
 
CCM itaondolewa madarakani kwa amani 2025 , hii ni kwa sababu ya Katiba mpya na Tume Huru ya uchaguzi inayokuja , ccm bila Polisi hakuna kitu , hilo wewe unalijua vizuri sana
Hakuna kitu kizuri kama kuukubali ukweli jinsi ulivyo,
Kwanza kwa kazi nzuri anayoifanya Chief Hangaya, nani wa kushindana naye na kushinda?.

Pili, kuna chama gani cha upinzani cha kukabidhiwa nchi hiyo 2025?!.
P
 
Reactions: Tui
Halafu chadema sio chama kikuu cha upinzani kina kiti kimoja bungeni hakina kambi rasmi ya upinzani msijimwambafai
 
Mnafikiri chadema mkiendeleza vita vya kumkejeli na kumtukana marehemu Magufuli mtapata mafanikio kisiasa?
 
Tabu ya ndoto hii ni kama sinema tunayojua mwisho wake.
 
Mkuu Chadema itachukua nchi 2025 na hakuna atakayeleta fyokofyoko , hangaya hatogombea (nakung'ata sikio) , Ila wewe hautoshughulikiwa kwa unafiki wako , hivyo ondoa shaka , na wala chadema haitolipa kisasi kwa yeyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…