CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi

inawezekana ukawa unapoint kweli ila ningekuona pia unamsimamo atleast ungekua side mbali na cdm na ccm, lakini umedhihirisha upande ulioshika wazi wazi, mamvi katokea ccm , kalelewa huko, mpaka kazeekea huko, siku zote hakuona kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko,? mpaka jina lake lilipokatwa??? watanznia tuna lawama saana na hatuangalii wapi pa kutokea nna uhakika leo hii ccm ingemsimamisha mamvi mngelalamika na kusema cjhama gani kimeleta fisadi, ila leo hii ccm imemkata mnasema mnataka mabadiliko??/ mbona mnajichanganya?? hii inadhihirisha mnafanya kitu bora iende tu, ambayo itawaumiza baadae vizazi vyetu, tujitahidi kufanya uamuzi sahihi, na tukae tukumbuke , the decisions we make today might have effects tomorrow

umeona mbali saana, wakiwa haweajui nini wanataka bado
 
Taratibu kamanda..,umekuja kwa hasira sana..povu linakutoka na spelling unakosea. Taratibu Kamanda.

Kwa tafsir yako Tafiti ni nini..? Kwangu mimi yale majibu ya TWAWEZA, SYNOVATE na LOTUS ni majibu ya kitafiti.,yanatuambia kuwa nani anauelekeo gani katika uchaguzi huu.

Haya hata maoni ya BBC nayo haujishughulishi nayo..? Au nao wamenunuliwa na CCM..?

Na wewe unemponda mwenzako kwa spelling ...haya Synovate ndio kampuni gani siku hizi? Haa haa halafu na wewe kabisa umezianalyze hayo majibu ya "tafiti zinazoitwa za BBC" ...ukizichunguza na ukiweka na demographic weithage utaona ipo tofauti na wewe unavyodhani...lakini nakubaliana na wewe kutafakari sijui CDM itakuwaje baada ya uchaguzi...
 
Ni suala la uwezo wa ufikiri na kuamua...ndugu yangu unaonekana uko vizuri na uko sahihi kabisa kutokuhitaji USHAURI ili uendelee kubaki kama ulivyo.
Ulishaondoka Chadema siku nyingi, sijui huko uliko hivi sasa wamekupa cheo gani. Lakini kuna msemo wa Wasukuma, ya Ngoshwe mwachie Ngoshwe. Mambo ya kuangalia angalia nyuma utageuka kuwa jiwe. Ni ushauri tu.
 
Kila mtu na aminicho.Na kila mtu akikatakacho.I wish hata hao wafanya kampeni waCCM wangejikita katika kutetea ILANI yao zaidi ya kupamba mikutano na KAULI mbiu moja tu LOWASSA fisadi.

Mwanz,ningekuona kweli wewe una UTAIFA kama ungeona kwamba si CCM wala CDM wana a right candidate wa URAIS.

Rudi nyumba angalia wale walioingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge 99% wamehonga wajumbe ili wapate nafasi husika.

Simlaumu mtu nailaumu CCM kulea RUSHWA,ndiyo maana nasema tena with confidence,Magufuli hawezi na hataweza kupiga vita RUSHWA wala UFISADI.

Walioingia kwa RUSHWA lazima watataka kurudisha pesa zao.Bahati mbaya sana nilikutana na Mgombea mmoja ambaye alinihakikishia kwamba pesa yake itarudi kwa maana atapata UWAZIRI na siyo kwa kuhisi ni kwa kunihakikishia LAZIMA atapata,na kweli baada ya UCHAGUZI 2010,alipata UWAZIRI na nimeona wizara yake ilivyogubikwa na rushwa,ufisadi na ujangili wa maliasili zetu.

Ndiyo maana kwa sauti kabisa Mwanz nasema ni BORA mmoja aliyetubu maana hata SAULI aliopolewa akawa PAULO.

Sawa, nimekuelewa, ni nani kama SI Magufuli, atakayeweza kupambana na UFISADI, RUSHWA na UBADHILLIFU.
 
Sitachagua chama ambacho najua kwa uhakika hakioni thamani ya watu wake.Chama ambacho kwa miaka zaidi ya hamsini haioni maovu yake.

Chama ambacho kinaona maovu ya viongozi wake pale tu wanapohama toka chama chao kwenda chama kingine.

Ni bora nikapimwe akili na kuendelea kuitwa Mpumbavu na LOFA kuliko kuchagua tena Chama kile kile chenye maona yale yale,tabia ile ile,ikikumbatia wezi wale wale.

Nipo na imani na ninachokiamini hakuna na hakutakuwa na maendeleo kamwe chini ya CCM mpaka pale wanaCCM walio wengi na ambao ni MALOFA na WAPUMBAVU kama mimi watakapojitambua kuwa na wao pia wako kama mimi.

Hayo ni maoni yako, na hao wanaosema mkichagua CCM au UKAWA, ni maoni yao, kila mtu ana imani na sababu au hoja zinazomfanya aendelee lkuwa muumini au mshabiki wa chama fulani, hivyo basi, na mimi sitaweza kuruhusu chama cha watu wanafiki ambao walituaminisha ufisadi wa baadhi ya viongozi, halafu leo waniambie eti wale watu wamekuwa ni wasafi na wana maendeleo (mabadiliko), ni heri nibaki na maendeleo yangu ya mwendo wa kinyonga, nimeridhika na maendeleo yaliyopo ndani ya serikali kupitia chama cha mapinduzi, japo changamoto ni nyingi kama hizo za ufisadi, LAKINI SIWEZI KUMPA FISI MFUPA, NYAMA KAILA NA MFUPA NIMPE? bora nilambe hata mfupa
 
Hakuna shida.Sababu I value my vote.Pole.Ndiyo maana situmii matusi kukujibu.

If you value your vote, then i will be supprised if you vote for someone who has bad scandals
 
Basi CCM kuna sijui shimo au tuite pango la uongozi kabisaaaaa. Heri wenye ombwe. Majirani wameshatumbukia kwenye hilo pango la uongozi
 
Nashukuru kwa mawazo na mchango wako..

Kuna wakati lazima tujifunze kuwa wakweli na tuuzungumze ukweli wote, sio kwa kuficha ficha, sio kwa kuoneana haya wala si kwa kusimangana bali kwa nia njema ya kujenga.

Yericko Nyerere - A story teller kumtaja hadharani kuwa ana IQ ndogo sio tusi..,kuna wakati nilikuwa nae kwenye group moja ya WhatsApp akawa kila asubuhi na jioni analeta taarifa za uzushi na uongo, na mkimkosoa leo asubuhi jioni anarudia tena kuwaletea kisa kingine..nikamwambia wazi kuwa shida aliyokuwa nayo ni UWEZO mdogo wa UBONGO wake..sio tusi ni UKWELI.

Kama kweli mdogo wangu unaju kuwatusi watu jaribu kumuita Nape matusi uliyokuwa ukiyatoa au unayoyatoa kwa kwa Yeriko tuone hata kama utaruhusiwa kuvaa hata shati la kijani

Ama kuhusu MBOWE, kabla ya hapo, naomba nikuthibitishie kuwa hakuna mtu ambaye hakuwahi kutofautiana na MBOWE katika uendeshaji wa Chama kwa muda mrefu kuliko mimi pale ambapo alitenda sawasawa, nilisimama kila wakati kwenye vikao vyetu, nikatanguliza neno SHUKRANI Mwenyekiti umetuvusha kwa hili na hili, nilimsifu katika kila jema, lakini bahati mbaya sana kwa Wafalme wetu hawajui kuwa kuna kusifiwa na kukosolewa..kwao kukosolewa ni kuvunjiwa heshima...

Pia jaribu kumtukana Mwenyekiti JK kama ambavyo ulimtukana Mbowe ndipo utaona rangi zote. Si kuwa kila aliyekaa kimya ndani ya chama au taasisi anakubalina kila kitu na viongozi wa juu. Tatizo hapa ni kuwatusi wakubwa zako na ninavyokufahamu tayari umeshang'atwa na nyoka hata ujani utuogopa. Laiti kama waliokulea wangekuacha uendelee na tabia ya kuwatusi viongozi wako usingeweza kuwa kiongozi unayejisisfia kuwa. Big UP CDM for bringing you!!!

Siku ya Kwanza kabisa kutofautiana na MBOWE ni siku ambayo VIJANA WAWILI wa BAVICHA walipotakiwa kwenda UGANDA kwa mafunzo ya Kiungozi na Utawala (PYPA), Mimi na Mwenyekiti(HECHE) tukapanga wawakilishi wetu, ambao ni Vijana wapambanaji ambao tumekuwa tukiwatumia kwa muda mrefu bila kuwalipa fadhila yeyote, tukadhani nafasi ya kuwaendeleza, kuwaandaa imefika, tukapendekeza majina yao..SIKUAMINI kilichotokea.

Siku tatu kabla ya Safari, yaliletwa MAJINA ya watu ambao siwajui, sikuwahi kuwaona popote pale katika mapambano na harakati za BAVICHA, nikaambiwa watakwenda hao badala ya wale tuliowapitisha Mimi na Mwenyekiti (Moja ya jina nililoletewa ni JOHN MALLYA - Ambaye kwa sasa ndio mwanasheria wa Chama) BINAFSI nilipingana na MBOWE katika hili, tena wazi wazi...nikihoji UHALALI wa John Mallya na Mwenzake kwenda kwenye mafunzo hayo

Lakini kama hilo halitoshi, wakati kuna mfarakano na mvutano mkubwa wa kimtazamo ndani ya Chadema 2012, kuhusu kutosha kwa Mwenyekiti katika nafasi yake..Binafsi nilieleza kwa hoja ndani ya Kikao kwanini nadhani MBOWE asiendelee kwenye nafasi hiyo na badala yake ZITTO achukue kijiti..nilitoa sababu na vigezo (ambavyo kama itabidi nitavisema hapa siku moja) Huu ukawa ndio mwanzo wa VITA kamili kati yangu na MBOWE na TIMU yake.

Nilivumilia mengi mpaka kufikia hatua hiyo ya kumuiya ZERO ndani ya Kikao, na actually ni baada ya kuja na barua (fake) eti ya kukihujumu Chama, nikamwambia ikiwa Mwenyekiti u with all resource that U have bado unakubaliana na uzushi uliomo ndani ya barua hiyo na umefanya maamuzi based on that piece of sh&***t then wewe ni ZERO...ilikuwa hakuna namna nyingine ya maelezo, isipokuwa kuuweka UKWELI ninaouamini mbele ya wote.

Sikia, I believe on myself na naendelea kuona kuwa i'm an asset popote pale nilipo, the good thing CCM nimeaminiwa, nikakubaliwa na nikaruhusiwa kufanya na kutenda ninachokiamini....nimepelekwa shule, nimepelekwa darasa la itikadi ya CCM, nikapikwa upya namna bora ya kufanya siasa, nikaondolewa Uhanaharakati nikafundishwa siasa..nikajaribiwa na nikafuzu.

Hizo shule siku hizi ni short courses, tulikuwa tunahudhuria miezi 12 ili kuwa mwanachama wa CCM ya wakulima na wafanyakazi. Toka ikengeuke na kuwa ya wafanyabiashara uanachama ni vodafasta ndio maana Merehemu Kolimba halideclare openly kuwa CCM imepoteza dira na mwelekeo.

watanzania wa sasa wanachotaka ni mabadiliko na sio blah blah za chama fulani, na ninashukuru sana hata mgombea wenu amelitambua hilo ndio maana ana behave kama mgombea binafsi. Huo ni ushindi mkubwa kwa M4C japokuwa ni kweli baadhi ya makamanda wake wamejitosa baharini na kuliwa na mamba!!

Imani yao kwangu ni kubwa, ninachokiandika hapa kuhusu CHADEMA, kama ningekiandika nikiwa CHADEMA kuhusu CCM ningefukuzwa CHAMA, kwa sababu maamuzi yao yanazingatia zaidi mihemko na hisia.

Na ndivyo ilivyo....na ndivyo walivyo....wanaamua bila KUFIKIRI.

Watanzania sasa hawataki blah blah wanataka mabadiliko na ninashikuru sana hata mgombea wenu amelitambua hilo kuwa hakuna mtu anataka kusikia kitu inaitwa CCM ila wanataka mabadiliko!!!
 
inawezekana ukawa unapoint kweli ila ningekuona pia unamsimamo atleast ungekua side mbali na cdm na ccm, lakini umedhihirisha upande ulioshika wazi wazi, mamvi katokea ccm , kalelewa huko, mpaka kazeekea huko, siku zote hakuona kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko,? mpaka jina lake lilipokatwa??? watanznia tuna lawama saana na hatuangalii wapi pa kutokea nna uhakika leo hii ccm ingemsimamisha mamvi mngelalamika na kusema cjhama gani kimeleta fisadi, ila leo hii ccm imemkata mnasema mnataka mabadiliko??/ mbona mnajichanganya?? hii inadhihirisha mnafanya kitu bora iende tu, ambayo itawaumiza baadae vizazi vyetu, tujitahidi kufanya uamuzi sahihi, na tukae tukumbuke , the decisions we make today might have effects tomorrow

magufuliforpresident,what ever the case,issue hapo hakuna chama kilichomleta RAIS msafi wote ni wachafu.Mbaya zaidi kwa sasa tutatafuta sana kupata MSAFI.

Tunapoletewa wezi wawili kwenye uchaguzi mkuu ni lazima mmoja apite,tupende tusipende.Basi nilichokiangalia ni mbali zaidi ya kuwaangalia watu hawa wawili.Nimeangalia haya:

1.Nikimchagua Magufuli,jopo lake la Mawaziri ni wale waliotoa RUSHWA kwenye kura za maoni,sasa hivi pia wako busy wanamwaga pesa na kunua shahada za mpiga kura,ninajiuliza ni kweli atafanikiwa kupiga VITA RUSHWA na UFISADI?Nikaliona changa la macho nikipigwa nalo usoni.

2.Nikakaa nisikilize ule wimbo wa CCM Mbele kwa mbele unanieleza kinagaubaga kwamba CCM ni ile ile,na hapa wameniambia kwa uhakika CCM haiwezi kubadilika hata Nyerere arudi,hivyo nikapata mshtuka yale maovu yataendelea.

3.Nimeangalia nguvu kubwa inayotumiwa na waliopembeni akina JK mpaka kutumia matusi,kutudhalilisha watanzania bila kujua kwamba ili kupata URAIS lazima KURA zote zichanyike wasio na vyama,toka vyama vya upinzani na kutoka CCM sasa kama sisi wanachama wa vyama vya upinzani tunaitwa MALOFA,MBUMBU,WAPUMBAVU,NYUMBU,WAKASKAZINI nknk ,nikajiona kwamba hapa issue ya UBAGUZI haitakwisha kamwe,kama tunabaguliwa leo wakati wa UCHAGUZI kesho itakuwaje???

4.Kwa sasa ninaona bora niende vyama vyetu vya MALOFA maana atleast kuna mmoja ameona umuhimu wa kufikia makubaliano na maelewano ili kuondoa chuki zilizojengwa kati yetu kwa miaka mingi.Asante Juma Duni Haji aliyeona umuhimu wa kuwa na MARIDHIANO katika TAIFA.

Kwa unisamehe bure tu,nipo pamoja na MALOFA wenzangu kwenye TEAM ya MALOFA.
 
If you value your vote, then i will be supprised if you vote for someone who has bad scandals

Hata Magufuli anazo,tena mbaya zaidi,unapomtamkia mtu wa kawaida ambaye hata kula yake ya kesho haijui,unamwambia eti APIGE MBIZI kuvuka kwenda kigamboni ni dhihaka ya hali ya juu.

Pili wizi wa mabilioni ya pesa yaliyolipwa kwa WAKANDARASI hewa sijui inahesabiwa kama kitu gani.

Hebu tuone na huu uuzaji wa nyumba za serikali ambapo leo watu wanakaa kwenye mahoteli wengine wakilipiwa $300 kwa siku kwa miaka mitano sijui serikali imelipa kiasi gani na hasara kiasi gani imepata.

Wizara ya Magufuli imenunua kivuko cha mwaka 1970 kwa bilioni 8, na mpaka hii leo hakitembei je na hii nayo tunaiitaje???

Nasema hivi Mwanz tumepewa wezi wawili tuwapigie kura na mmoja ni ndiyo atakayepita,hivyo usidhani sisi watanzania tunavyoitwa MALOFA ,WAPUMBAVU na MAMBUMBU ni kweli tuko hivyo,bali ni baada ya hawa tuliodhani wako kwa ajili ya TAIFA kumbe wako kwa ajili ya matumbi yao na leo wakitutukana sioni ajabu.Waliingia wakiwa wasafi wametoka wachafu,wanaonuka UFISADI,WIZI, na RUSHWA,leo bora tumuingize MCHAFU anaweza akabadilika maana kwa Mungu kila kitu chawezekana maana hata SAULI leo wakristu tunamuita MTAKATIFU PAULI.....
 
Hayo ni maoni yako, na hao wanaosema mkichagua CCM au UKAWA, ni maoni yao, kila mtu ana imani na sababu au hoja zinazomfanya aendelee lkuwa muumini au mshabiki wa chama fulani, hivyo basi, na mimi sitaweza kuruhusu chama cha watu wanafiki ambao walituaminisha ufisadi wa baadhi ya viongozi, halafu leo waniambie eti wale watu wamekuwa ni wasafi na wana maendeleo (mabadiliko), ni heri nibaki na maendeleo yangu ya mwendo wa kinyonga, nimeridhika na maendeleo yaliyopo ndani ya serikali kupitia chama cha mapinduzi, japo changamoto ni nyingi kama hizo za ufisadi, LAKINI SIWEZI KUMPA FISI MFUPA, NYAMA KAILA NA MFUPA NIMPE? bora nilambe hata mfupa

Kuna mawili unarithika na maendeleo unayodhani yapo lakini ni mfaidika mkubwa wa system mbovu iliyopo.Miaka 54 watu wanalala chini hospitali.Miaka 54 watanzania hawana maji safi na salama ya kunywa.Nimekaa Mbeya mjini kwa siku tatu mfufulilizo hakuna maji hata tone na wanalalamika wanamwaka maji hawapati,sasa najiuliza kama mijini hakuna maji vijijini kukoje???

Sijaona cha maana kilichopo ambacho naweza kuisifia CCM.Tulichangishwa kwa lazima CCM ikafungua Supermarket (SUKITA) ilikufa kifo cha mende,Mabasi ya wanafunzi ya kafa kifo cha mende,RTC zikafa kifo cha mende,shule za wazazi sidhani hata kama zinathamani ya kuitwa shule leo,viwanda hakuna vyote vimeuzwa na kila kiongozi kajipatia fungu lake.

Hakika napata hasira zaidi na zaidi,ni bora hawa unaowaita wanafiki na wao waingie tuone watatuvusha mpaka wapi.Na CCM wakae chini wajitafiti kuona ni wapi wanaweza kujirekebisha,ili kisife kabisa kibaki kama kumbukumbu ya Nyerere.
 
Sawa, nimekuelewa, ni nani kama SI Magufuli, atakayeweza kupambana na UFISADI, RUSHWA na UBADHILLIFU.

Hawezi sababu yeye mwenyewe ni FISADI kwenye ngozi ya KONDOO,na kati ya hao atakao wateua kuwa mawaziri pamoja na waziri wake mkuu wamepata UBUNGE kwa RUSHWA.Hebu ona wale ambao hawakutumia RUSHWA kwenye kura za maoni ndiyo wengi wametemwa,99% ya wanaogombea ubunge leo kwa CCM wametoa RUSHWA kwenye kura za maoni na sasa wako busy kununua wapiga kura maana wanajua hali za watanzania hivyo wanatumia pesa walizoiba kuendelea kukaa madarakani.

Hivyo in short MAGUFULI hawezi na hataweza kamwe,labda hiyo MAHAKAMA ya mafisadi na wala rushwa na muundia LOWASSA tu.

Juzi tu ameenda kumpigia debe CHENGE na kumsifia sana wakati ana skendo nyingi sana,leo utaniambia eti MAGUFULI ataweza labda wabunge wote waliotoa rushwa wafe kabla ya kuapishwa na wengine waje.
 
Fisi apewe mfupa, siyo, hayo unayoyanena, ningepende uje na ushahidi kwamba baadhi walipata uwaziri kwa rushwa na bla blaa nyingine, wewe ni shabiki wa LOWASSA bila shaka, umeshikwa masikio
 
Fisi apewe mfupa, siyo, hayo unayoyanena, ningepende uje na ushahidi kwamba baadhi walipata uwaziri kwa rushwa na bla blaa nyingine, wewe ni shabiki wa LOWASSA bila shaka, umeshikwa masikio

Hivi Mbunge anapoingia BUNGENI akiwa na asilimi 100 ya kuingia huko kwa kutumia RUSHWA tumuitaje?Tumuite SHUJAA au???

Ni vyema mtu akanishika MASIKIO kuliko wewe uliyeshikwa UBONGO maana hata kufikiri ni sifuri.Pole.

For your information mimi siyo Pro-Lowassa wala Pro-Magufuli kwangu mimi wote hawa wawili ni wezi,huyu mmoja anajulikana na huyu mwingine amejivika NGOZI ya kondoo.Usilolijua ni kama usiku wa kiza.

Bora huyu anayejulikana ni rahisi kumcontroll kuliko huyu aliyevaa ngozi ya kondoo.

Pole sana.
 
Sasa wewe inaonesha ni sawa na mtu aliyekuwa njia panda haelewi afanye nini, maana kwa hali ilivyo tunahitaji kufanya uamuzi wa nani anakuwa rais, kwa kuwa hujaniambia hasa unachokilalamikia ni nini, bila ya kujua njia ya kutatua. Mf ukisema huna pesa, inajulikana watu watakutafutia kazi, sasa unalalamika halafu kichwani kwako hujui hata cha kufanya. Umesema wewe siyo PRO wa Lowassa wala Magufuli, sasa hizo taarifa ulizozitoa ya kwamba wao ni wezi umezitoa wewe kama nani, hakimu au polisi?
 
kama wakiwa wakiendelea tu kwenda kwenda tu bila muelekeo na kufanya mambo bora liende, wataishia pabaya saana, na kama hawatajipanga vizuri, nakuishia kutetereka kwa migogoro yao, tutawazika oktoba, hii .....
 
Back
Top Bottom