Tetty
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 26,355
- 21,418
Sasa wewe inaonesha ni sawa na mtu aliyekuwa njia panda haelewi afanye nini, maana kwa hali ilivyo tunahitaji kufanya uamuzi wa nani anakuwa rais, kwa kuwa hujaniambia hasa unachokilalamikia ni nini, bila ya kujua njia ya kutatua. Mf ukisema huna pesa, inajulikana watu watakutafutia kazi, sasa unalalamika halafu kichwani kwako hujui hata cha kufanya. Umesema wewe siyo PRO wa Lowassa wala Magufuli, sasa hizo taarifa ulizozitoa ya kwamba wao ni wezi umezitoa wewe kama nani, hakimu au polisi?
Kwa hiyo kwa kunipa kazi ndiyo niipigie CCM au Magufuli???Hivi kujua kwamba mtu mwizi mpaka umuoane anaiba??Hivi Audit report inaposema wizara ya Ujenzi imelipa Bilioni 262 Wakandarasi hewa maana yake nini???SIyo pesa zimepigwa???Waziri wa ujenzi alijikatia ngapi??Maana nina uhakika ndiye aliyeidhinisha malipo au??Ili labda kama wewe ni mfanyakazi wa serikali utatueleza namna pesa nyingi kama hizi zikitoka nani anaziidhinisha....
Pili hivi unapotoa idhini kuuzwa nyumba za serikali na nyingine ungawa kwa ndugu na jamaa unataka tukuone wewe ni mwema mno au???
Hivi unaponunua meli isiyotembea kwa bilioni 8,meli ya mwaka 1970 wakati Azam ananunua Brand new kwa bilioni 6,nani muidhinishaji ni waziri wa ujenzi,tufikirire nini???
Sina PHD lakini nina imani 2+2=4, na 1+1 =2 japo 2x2=4 lakini 1x1 si 2....
Pole sana siyo Pro-Lowassa wala Pro-Magufuli,sababu wote wawili ni wachafu,lakini kama Mtanzania nimeambiwa nichague kati ya wachafu wawili hawa.Basi bado sijaamua nani wa kumchagua lakini siwezi kuipoteza kura yangu kwa kuipigia KURA CCM,hivyo basi sina sababu ya kusema nitampigia KURA Magufuli ambaye leo amejitanabaisha kwamba na yeye pia anaizimia M4Chadema