rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,412
Dar es Salaam. Wakati Ukawa ikiendelea na ziara yake mikoani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeandaa Kongamano la Wazee zaidi ya 500 kutoka Kanda ya Pwani na Dar es Salaam leo kwa lengo la kuendeleza ushawishi kuhusu muundo wa Serikali.
Hatua hiyo imekuja wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba(Ukawa na Tanzania kwanza), wakiendeleza mijadala ya kuvutana juu ya muundo wa Serikali, (mbili ua tatu), unaotakiwa kupitishwa na Bunge hilo katika mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee katika chama hicho, Erasto Singila alisema kuwa hoja ya muundo wa Serikali ni miongoni mwa mijadala iliyobeba hisia za Watanzania wengi, hivyo ni vyema kushirikisha wazee watakaojadiliana ili kupata mitazamo yao.
Hoja hiyo itakuwa sehemu ya ajenda zetu kesho(leo), siyo vibaya kukumbusha wazee juu ya hoja hiyo kutokana na mvutano uliopo, wazee tujadiliane na kupata ufafanuzi wa majibu ya hoja mbalimbali, alisema Singila na kuongeza:
Wazee tunaotarajia kuwa nao pale Ukumbi wa Msimbazi Center ni zaidi ya 500 kutoka mikoa ya Pwani, wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Aidha, Singila aliongeza akisema ajenda nyingine zitakazojadiliwa na wazee hao ni pamoja na namna ya ushiriki wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Lakini pia, tutakuwa na ajenda itakayohusu hatima yao katika ujenzi wa taifa, wazee wamekuwa watu muhimu katika historia ya taifa letu, lakini hatima ya maisha yao katika huduma za kijamii imekuwa mbaya. Kwa hiyo tutaangalia hilo pia, alisema Singila.
Aliongeza kuwa makongamano kama hayo yamekuwa yakifanyika ikiwa sehemu ya utekelezaji wa sera ya chama.