CHADEMA kukusanya wazee 500 Dar es Salaam, Pwani leo

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,842
2,000
Dar es Salaam. Wakati Ukawa ikiendelea na ziara yake mikoani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeandaa Kongamano la Wazee zaidi ya 500 kutoka Kanda ya Pwani na Dar es Salaam leo kwa lengo la kuendeleza ushawishi kuhusu muundo wa Serikali.

Hatua hiyo imekuja wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba(Ukawa na Tanzania kwanza), wakiendeleza mijadala ya kuvutana juu ya muundo wa Serikali, (mbili ua tatu), unaotakiwa kupitishwa na Bunge hilo katika mabadiliko ya Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee katika chama hicho, Erasto Singila alisema kuwa hoja ya muundo wa Serikali ni miongoni mwa mijadala iliyobeba hisia za Watanzania wengi, hivyo ni vyema kushirikisha wazee watakaojadiliana ili kupata mitazamo yao.

“Hoja hiyo itakuwa sehemu ya ajenda zetu kesho(leo), siyo vibaya kukumbusha wazee juu ya hoja hiyo kutokana na mvutano uliopo, wazee tujadiliane na kupata ufafanuzi wa majibu ya hoja mbalimbali,” alisema Singila na kuongeza:

“Wazee tunaotarajia kuwa nao pale Ukumbi wa Msimbazi Center ni zaidi ya 500 kutoka mikoa ya Pwani, wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es Salaam.”

Aidha, Singila aliongeza akisema ajenda nyingine zitakazojadiliwa na wazee hao ni pamoja na namna ya ushiriki wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Lakini pia, tutakuwa na ajenda itakayohusu hatima yao katika ujenzi wa taifa, wazee wamekuwa watu muhimu katika historia ya taifa letu, lakini hatima ya maisha yao katika huduma za kijamii imekuwa mbaya. Kwa hiyo tutaangalia hilo pia,” alisema Singila.

Aliongeza kuwa makongamano kama hayo yamekuwa yakifanyika ikiwa sehemu ya utekelezaji wa sera ya chama.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Kwao akiongea na wazee wa Dar es salaam maneno lukuki halafu nao wanafuata humohumo!!!!
Mkiambiwa hamna upinzani maneno, wenyewe wakiwaambia wao ndio role model wenu maneno!!!!

Haya kila la heri
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Sasa hii ni UKAWA au CHADEMA.

Hawa wanadai wameungana kwenye suala la katiba na kwa maana hiyo, ukiongea kuhusu katiba, basi lazima jina UKAWA liwe zaidi ya jina la chama kama CHADEMA.

Au ndiyo yale yale ambayo ni mwendelezo wa misingi ya kibaguzi
na ubinafsi kwa maana kwamba chako ni changu na changu ni changu.

Wewe CUF au NCCR-Mageuzi ukiandaa tunaita UKAWA lakini mimi nikiandaa tunaita CHADEMA!.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) tunawaona na kuwasikia nchi nzima wakifanya mikutano kuhusu katiba mpya. Kwa upande mwingine Tanzania kwanza, hatuwasikii wala kuwaona wakifanya mikutano na badala yake tunawaona akina Nape na Kinana waki counter attack hoja za UKAWA kuhusu katiba mpya. Swali langu, Je, Tanzania kwanza ndio akina Nape na Kinana?
 
mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
4,058
1,195
Sasa hii ni UKAWA au CHADEMA.

Hawa wanadai wameungana kwenye suala la katiba na kwa maana hiyo, ukiongea kuhusu katiba, basi lazima jina UKAWA liwe zaidi ya jina la chama kama CHADEMA.

Au ndiyo yale yale ambayo ni mwendelezo wa misingi ya kibaguzi
na ubinafsi kwa maana kwamba chako ni changu na changu ni changu.

Wewe CUF au NCCR-Mageuzi ukiandaa tunaita UKAWA lakini mimi nikiandaa tunaita CHADEMA!.

vipi mkuu mbona jimboni kwa tundu lisu tulipata watu wachache kwenye mkutano halafu wazee zaidi
 
Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700

Umechanganyikiwa kama kinana , unafikiri kuwa shughuli za vyama zimekufa? Mwaka huu utataga tu, ndio,maana CUF wanaendelea na uchaguzi wa ndani, chadema hivyo hivyo , na NCCR nao wanaendelea na majukumu yao ndio maana ofisi hazijafungwa .........UKAWA in kupa taabu sana sio
 
MwanaDiwani wewe ni kiongozi mkubwa CCM, naomba unijibu maswali yangu, Hivi Kinana na Nape ndiyo TANZANIA KWANZA? Kama Kinana Nape sio Tanzania kwanza mbona hao Tanzania kwanza hatuwasikii? Kama Nape na Kinana sio Tanzania kwanza katika, mbona basi katika mikutano yao wamebeba agenda za TANZANIA KWANZA? Kama maswali haya ni magumu basi nipotezee, maana mara nyingine ni busara kuficha ujinga kwa kukaa kimya.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
vipi mkuu mbona jimboni kwa tundu lisu tulipata watu wachache kwenye mkutano halafu wazee zaidi

Ndugu, ungeeleza kwanza watu wachache ndiyo wangapi kwenye jimbo la Tundu Lissu na katika msingi huo ndiyo ungejenga hoja yako.

Kwa kukusaidia zaidi, nikisema india ina watu wachache kuliko China nadhani utaelewa maana yangu.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Umechanganyikiwa kama kinana , unafikiri kuwa shughuli za vyama zimekufa? Mwaka huu utataga tu, ndio,maana CUF wanaendelea na uchaguzi wa ndani, chadema hivyo hivyo , na NCCR nao wanaendelea na majukumu yao ndio maana ofisi hazijafungwa .........UKAWA in kupa taabu sana sio

Ndugu, hakuna shughuli kuu na muhimu katika chama kama kufanya uchaguzi kama zilivyo taratibu na katiba.

Hivi unafahamu kuwa Ratiba ya chaguzi za CHADEMA iliyotolewa baada ya sakata la Zitto, Dr. Kitila na Mwigamba inaonyesha kuwa mwezi huu ni ngazi za Mkoa. Cha kushangaza hata uchaguzi wa kata haijafanyika/kumalizika. Hawa ndiyo CHADEMA. Kwenye ulaghai wanaongoza!. Baada ya kuona maji ya kisiasa ndani ya chama yako shingoni, wakaja na hoja ya uchaguzi ndani ya chama ili kuwafumba macho wanachama.

Sijaona vyama vya kuachiana wagombea na hasa ikichukuliwa kuwa kura za urais zinaleta pesa kama ruzuku za vyama.

Kura za Urais za Prof. Lipumba ambazo ni 9.80% zinakipatia CUF 57.9 million wakati kura za Urais za Dr. Slaa ambazo ni 24% kinakipatia CHADEMA 146 million every month.

Nani atataka kuziachia hizi pesa wakati vyama vingine tunaambiwa vilianzishwa kibiashara.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
MwanaDiwani wewe ni kiongozi mkubwa CCM, naomba unijibu maswali yangu, Hivi Kinana na Nape ndiyo TANZANIA KWANZA? Kama Kinana Nape sio Tanzania kwanza mbona hao Tanzania kwanza hatuwasikii? Kama Nape na Kinana sio Tanzania kwanza katika, mbona basi katika mikutano yao wamebeba agenda za TANZANIA KWANZA? Kama maswali haya ni magumu basi nipotezee, maana mara nyingine ni busara kuficha ujinga kwa kukaa kimya.

Ndugu, Mimi ni mwanachama wa kawaida ndani ya CCM.

Kinana ni Katibu Mkuu wa CCM na Nape ni Katibu wa NEC Taifa wa Itikadi na Uenezi.

TANZANIA KWANZA haina uhusiano wowote na CCM kama chama.

Ziara za Katibu Mkuu zimepangwa kabla hata ya Bunge la Katiba halijaundwa.

Kwa kukusaidia, ukienda kwenye mikutano ya kikundi kinachojiita UKAWA, utagundua kuwa majina ya Mzee Kinana na Nape yanatajwa mara nyingi zaidi ya neno Katiba ambalo ndiyo wanadai ni ajenda mama. Kwa maana nyingine, Mzee Kinana na Nape ndiyo imekuwa ajenda kuu kwenye mikutano ya kikundi kinachojiita UKAWA.

Fanya huo uchambuzi na utakubaliana na hiki ninachokisema.
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,530
2,000
Dar es Salaam. Wakati Ukawa ikiendelea na ziara yake mikoani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeandaa Kongamano la Wazee zaidi ya 500 kutoka Kanda ya Pwani na Dar es Salaam leo kwa lengo la kuendeleza ushawishi kuhusu muundo wa Serikali.

Hatua hiyo imekuja wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba(Ukawa na Tanzania kwanza), wakiendeleza mijadala ya kuvutana juu ya muundo wa Serikali, (mbili ua tatu), unaotakiwa kupitishwa na Bunge hilo katika mabadiliko ya Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee katika chama hicho, Erasto Singila alisema kuwa hoja ya muundo wa Serikali ni miongoni mwa mijadala iliyobeba hisia za Watanzania wengi, hivyo ni vyema kushirikisha wazee watakaojadiliana ili kupata mitazamo yao.

“Hoja hiyo itakuwa sehemu ya ajenda zetu kesho(leo), siyo vibaya kukumbusha wazee juu ya hoja hiyo kutokana na mvutano uliopo, wazee tujadiliane na kupata ufafanuzi wa majibu ya hoja mbalimbali,” alisema Singila na kuongeza:

“Wazee tunaotarajia kuwa nao pale Ukumbi wa Msimbazi Center ni zaidi ya 500 kutoka mikoa ya Pwani, wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es Salaam.”

Aidha, Singila aliongeza akisema ajenda nyingine zitakazojadiliwa na wazee hao ni pamoja na namna ya ushiriki wao katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015.

“Lakini pia, tutakuwa na ajenda itakayohusu hatima yao katika ujenzi wa taifa, wazee wamekuwa watu muhimu katika historia ya taifa letu, lakini hatima ya maisha yao katika huduma za kijamii imekuwa mbaya. Kwa hiyo tutaangalia hilo pia,” alisema Singila.

Aliongeza kuwa makongamano kama hayo yamekuwa yakifanyika ikiwa sehemu ya utekelezaji wa sera ya chama.

Safi sana kisha muandae ya kina mama!upinzani inahitaji nguvu ya ziada kuwapata kina mama ambao ni muhimu sana
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,864
1,250
Sasa hii ni UKAWA au CHADEMA.

Hawa wanadai wameungana kwenye suala la katiba na kwa maana hiyo, ukiongea kuhusu katiba, basi lazima jina UKAWA liwe zaidi ya jina la chama kama CHADEMA.

Au ndiyo yale yale ambayo ni mwendelezo wa misingi ya kibaguzi
na ubinafsi kwa maana kwamba chako ni changu na changu ni changu.

Wewe CUF au NCCR-Mageuzi ukiandaa tunaita UKAWA lakini mimi nikiandaa tunaita CHADEMA!.

Mawazo na msimamo wako siku zote ni kupotosha .Chadema kama chama wanaweza kuendelea kuongelea muundoa wa serikali nje ya UKAWA what is so wrong bro . Think bigger
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom