Chadema jihadharini na watu wa usalama wa taifa

Lamuhimu ni kuepuka UDINI na UKABILA ndio wengi wanakilaumu CHADEMA na kama haitajivua koti hilo chafu huenda ndio ukawa mwisho wa CDM!!!

Hii ni imani potofu ambayo ccm wamefanikiwa kuijenga kwa watz wengi ambao hawapendi kujituma kushugulisha halmashauri za ubongo zao. Udini na ukabila ni propaganda za kuturudisha nyuma ni lazima kuwaelimisha wote wanaoamini hivyo badala ya kuwa wakali. Chama lazima kiandae mipango ya lazima na semina za kukemea udini na ukabila.
 
kuna hoja..wenye masikio na wasikie!

Ni kweli NgumiJiwe, hoja ipo na personally nawaomba CDM wawe makini sana na hawa UWT.
Kumbukeni hawahawa UWT ndiyo waliosaidia KUCHAKACHUA KURA ZA UCHAGUZI MKUU 2010 ILI CCM washinde na walifanikliwa.
Na kwasasa bado UWT wanatumiwa na CCM/SERIKALI kuimaliza CDM. Mtu kama Zitto Kabwe yuko very close na baadhi ya vigogo wa UWT na yumkini anatumiwa sana na hawa watu kuiyumbisha CDM.

Fuatilieni kwa karibu mtagundua kuwa there is something fishy going around between Zitto and UWT. Matukio ya Zitto kutowaunga mkono wenzake CDM walivotoka Bungeni kupinga hotuba ya JK, Zitto kutokuwepo kwenye maandamano ya A Town kupinga uchaguzi wa Meya na kitendo cha Zitto kumpigia JK ili aendelee kuwa M/kiti wa POC are events which raises an eyebrow! CDM iweni makini na UWT na ZITTO. Something is cooking!

Wenye masikio na wasikie yale wana Jamiiforums wanasema.
 
Ni vyema cdm ikawa aware kuwa sasa ndiyo homa kuu ya ccm, wawe makini na kila mtu wasiyemfahamu vyema hasa watu wenye influence kubwa. Watu wenye influence huwa ndio vyombo muafaka vya kuchochea migawanyiko katika chama na kukipaka tope machoni mwa wapiga kura. Lakini pia kuwa na vyombo vya habari hasa radio na TV ni muhimu sana. Vinginevyo ikifika wakati wa uchaguzi tutazamie cheza ya rafu kupindukia kwa upande wa ccm kwa sababu wameshaona jinsi cdm kilivyo tishio. Wataakikisha kuwa wanavibana vyombo vyote vya habari visitangaze mikutano ya cdm. Msisahau mlivyotafuta kurusha kipindi cha mdahalo wa Dr. Slaa ile siku ya mwisho ya kampeni kwenye TV zote mkaambiwa TV zimekataliwa zisirushe hicho kipindi. Tafadhali msipuuze swala la kuanzisha radio na TV.
Nilikuwa nazungumza na mtu wa usalama akanieleza jinsi walivyoiua nccr na kuidhoofisha cuf wakati ule. anasema chadema wanajaribu lakini ina ugumu maana lazima uingize watu wenye ushawishi wakavuruge vikao vya chama ili chama kigawanyike. chadema inapaswa kuepuka matatizo waimarishe sana demokrasia ndani ya chama hivyo maamuzi yote makubwa yatokana na vikao hata mtu akipinga anakuwa hana nguvu. pili waimarishe kitengo cha propaganda. tafuteni wasomi wenye kiwango kama dr lwaitama mlipeni vizuri awe anapiga
Google
 
hii ungeachana nayo maana hata yeye asingependa yazungumzwe kulinda heshima yake na ya chama, kwa hiyo yaache hivyo hivyo.

Mkuu,

Hapa una maana gani? Tufafanulie kwanini Dr. Slaa asingependa suala hili lijadiliwe. Ni heshima ipi italindwa?

Tiba
 
Lamuhimu ni kuepuka UDINI na UKABILA ndio wengi wanakilaumu CHADEMA na kama haitajivua koti hilo chafu huenda ndio ukawa mwisho wa CDM!!!

Upupu mtupu, Anyway, Zubeda tunajua huko kazini lakini hapa sio sehemu rahisi ya kupenyeza huo ujinga wenu!!!!

Tiba
 
Lamuhimu ni kuepuka UDINI na UKABILA ndio wengi wanakilaumu CHADEMA na kama haitajivua koti hilo chafu huenda ndio ukawa mwisho wa CDM!!!

Kwani chama tawala wao wamejivua? Huoni kama udini ndio umeshamiri huko ? Hizo ni propaganda tu za kuishusha CDM lakini itachukua muda sana.
 
Huyo hawezi kuwa mtu wa usalama wa taifa ni tapeli mmoja aliyeamua kujipatia umaarufu kupitia mgongo wako. Vyama vya siasa ni taasisi sio rahisi kuua taasisi hii kama ilivyo kwa mtu mmoja mmoja....... kama ingekuwa rahisi kiasi hicho chadema kingekuwa kimekufa kwani ndicho chama kikuu cha upinzani hivi sasa, kwa maana ndicho chama tishio kwa CCM hivi sasa.

Vyama vya NCCR, TLP na UDP vimekuwa kama vimekufa kwa sababu ya migogoro yao ya ndani na uongozi mbovu ingawa wao wanaweza kusema migogoro hiyo ilipandikizwa na Usalama wa taifa lakini kama chama na uongozi ni imara watu wa Idara hiyo hawawezi kupenya.

Nionavyo mimi kila jambo baya hapa nchini hivi sasa linasababishwa na usalama wa taifa kiasi kwamba rejea hii inafinya uwezo wetu wa kufikiri kwa upana bila mipaka ya kuanisha viashiria vya matatizo yanayotukabili. Hii inaweza kuwa ni mbinu ya mafisadi kutaka watanzania tuwe na fikira moja tu kwamba tukio lolote baya linalotokea nchini linasabaishwa na Idara hiyo.

Sipingi Idara hiyo kuweza kufanya hivyo lakini tusilale usingizi tukaamini kuwa ndio sababu pekee inayoua vyama vya siasa hapa nchini. Hivi sasa CCM iko kwenye mtikisiko wa kisiasa, hivi majuzi tumeambia UVCCM wanailaumu Idara ya usalama wa Taifa kuwa haimsaidii Mwenyekiti wa CCM (Rais) kwa maana nyepesi ni kwamba Idara hiyo inataka kuua CCM. Mimi naona hayo yote ni mazingaombwe ya kushindwa kwa wanasiasa kuwajibika.
 
Wazungu wanasena Fear is the key!..
Hii habari ni ya kupotosha nakuwatia hofu CDM kama chama ili waogope nyoka hata wakiguswa na unyasi..

Hakuna kitu haramu wanachokifanya Chadema na mara zote tumeona CCM wakishtukizwa na maamuzi mengi ya CDM..
Kwa mfano Dr.Slaa alipotangazwa kuwa mgombea urais na hata haya maandamano ya kanda za ziwa..

Kama kweli UWTwangekuwa wamepangwa kuki maliza chama kupitia viongozi wake na hasa mgonvi wenu mkubwa Zitto basi bila shaka CCM wangekuwa na taarifa hizo mapema na kuyapiga vita...

Tunajua CCM sasa hivi wamejipanga kuzuia maandamano me gine yeyote ya CDM na tayari wamekwisha weka mikakati yao.. Hizi ni habari zimetoka CCM kwenda CDM hivyo sidhani kama UWT ni tatizo kwa CDM..

Mimi hadi leo siamini kabisa kwamba Zitto ni msaliti wa chama isipokuwa naamini Zitto ni mshindani na anawanyima watu wengi usingizi..
Yawezekana kabisa kwamba CCM wamepandikiza chuki ndani ya CDM kwa kupitia Zitto ambaye siku zote ameapa hapa mbele ya kijiwe hiki kwamba hanunuliki na kama kuna mtu anao ushahidi autoe hapa...

Sijaona ushahidi wowote JF zaidi ya maamuzi ya Zitto ambayo sisi hatuna uhakika kwamba chama hakikuwa na taarifa au hakuwa na majukumu mengine ya kichama..

Nachokiona mimi ndani ya CDM ni chama kinachokubalika na wengi na tatizo kubwa la CDM ni kujipenyeza ktk jumuiya za Waislaam kwa sababu CCM waliweza kuipenyeza chuki ya Udini na hata mtu kama Zitto na maswahiba wake kuamini kwamba hapendwi na wananchama na washabiki wa CDM pasipo sababu ila pengine labda dini yake..

Hizi habari za Zitto kuwa karibu na UWT na kutia hofu sijui kama mnafahamu kwamba karibu viongozi wote nchini wanatakiwa kujenga mahusiano na chombo hicho badala ya kuwaita maadui...

Hawa ni walinzi wetu na haitakiwi kuwaogopa hata kidogo kwani leo hii wanatumikia uongozi wa serikali iliyopo na kama CDM au mtu yeyote ana mpango mchafu dhidi ya serikali iliyopo madarakani watamshughulikia kwani ndio kazi na majukumu waliyokabidhiwa. Na watafanya hivyohivyo ikiwa Dr.Slaa na CDM wameunda serikali au mtu mwingine yeyote..
Tuacheni hizi nidhamu za woga!
 
Kwa mujibu wa mtoa hoja, Kama Idara hiyo iliweza kuingiza watu kwenye vyama vyenye nguvu kama CUF basi taarifa hii itakuwa na mapungufu kwamba Idara hiyo inashindwa nini kupenya chadema? eti kwa sababu imekosa watu wenye ushawishi!!!! Binafsi sioni ugumu wa Idara hiyo kukosa watu wenye ushawishi kama lengo ni kuivuruga chadema. Dhamira yangu ni kusisitiza kuwa kama ni kweli Idara hiyo imeshindwa kutimiza lengo kwa kukosa watu wenye ushawishi basi kimsingi hatuna taasisi ya ujasusi imara lakini kwa kuwa naamini taasisi hiyo ni imara sitaki kuamini kuwa hiyo ni sababu ya nguvu. kwa hiyo naamini habari ni ya kupikwa.

Nilikuwa nazungumza na mtu wa usalama akanieleza jinsi walivyoiua nccr na kuidhoofisha cuf wakati ule. anasema chadema wanajaribu lakini ina ugumu maana lazima uingize watu wenye ushawishi wakavuruge vikao vya chama ili chama kigawanyike. chadema inapaswa kuepuka matatizo waimarishe sana demokrasia ndani ya chama hivyo maamuzi yote makubwa yatokana na vikao hata mtu akipinga anakuwa hana nguvu. pili waimarishe kitengo cha propaganda. tafuteni wasomi wenye kiwango kama dr lwaitama mlipeni vizuri awe anapiga
Google
 
Back
Top Bottom