Chadema jihadharini na watu wa usalama wa taifa

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Nilikuwa nazungumza na mtu wa usalama akanieleza jinsi walivyoiua nccr na kuidhoofisha cuf wakati ule. anasema chadema wanajaribu lakini ina ugumu maana lazima uingize watu wenye ushawishi wakavuruge vikao vya chama ili chama kigawanyike. chadema inapaswa kuepuka matatizo waimarishe sana demokrasia ndani ya chama hivyo maamuzi yote makubwa yatokana na vikao hata mtu akipinga anakuwa hana nguvu. pili waimarishe kitengo cha propaganda. tafuteni wasomi wenye kiwango kama dr lwaitama mlipeni vizuri awe anapiga
http://www.google.com
 
propanganda kujibu hoja na kupeleka hoja. anzisheni vyombo vya habari kama magazeti, radio na tv. anzisheni blog ili mpate maoni ya watu na myazingatie. wapeni vijana nafasi ya kutoa mawazo na mzazingatie wajisikie chama cha kwao. nendeni kwa watu mijini na vijijini waulizeni wanataka sera gani ili sera zitokane na watu. mwisho muwe na intelligence kwenye vyama vingine ili mjue wana hujuma gani dhidi yenu ili mchukue hatua.
 
Huyo m-usalama wa taifa anatoa hoja gani ya faida kwa nchi kuvuruga vyama vya upinzani? Yeye pamoja na watanzania watafaidi nini kuibakiza CCM madarakani? Basi safari ya kumkomboa Mtanzania kutoka dimbwi la umaskini na hali duni ni ndefu. Hongera yao hao wanaUsalama...
 
wanalipwa tu kufanya kazi za waliowaajiri. hapa wanaangalia zaidi maslahi binafsi. tangia mfumo wa vyama vingi uanze usalama wa taifa umebadilika kuwa usalafa wa ccm. sioni kama kuna kazi nyingine wanafanya.
http://www.google.com
 
Kumbe kazi yao ni kuvuruga vyama vya upinzani, kwani wameajiriwa na chama tawala?
 
Naona walijaribu sana kuwavuruga kwa kutumia UWT lakini wapi, CDM wamefanikiwa kujipenyeza karibu kila kona mpaka UWT, ilikuwaje Dr. Slaa alijua kuwa amewekewa vinasa sauti kwenye chumba cha hoteli wakati ule alipokuwa bungeni Dodoma? Ni hao wanausalama walimtonya.
Hata sasa hivi CCM wanahaha kwa sababu wanajua UWT waliokuwa wanawasaidia sasa wanagonga mwamba.
 
hyo ni fact kwani usalama siku hzi ni tawi la ccm ...heko kwa wazo la Tv,Radio
 
, ilikuwaje Dr. Slaa alijua kuwa amewekewa vinasa sauti kwenye chumba cha hoteli wakati ule alipokuwa bungeni Dodoma.

hii ungeachana nayo maana hata yeye asingependa yazungumzwe kulinda heshima yake na ya chama, kwa hiyo yaache hivyo hivyo.
 
Kwa nyoneza itakuwa vizuri kama CDM watawatumia hao hao usalama wa taifa kwa manufaa yao
 
Nilikuwa nazungumza na mtu wa usalama akanieleza jinsi walivyoiua nccr na kuidhoofisha cuf wakati ule. anasema chadema wanajaribu lakini ina ugumu maana lazima uingize watu wenye ushawishi wakavuruge vikao vya chama ili chama kigawanyike. chadema inapaswa kuepuka matatizo waimarishe sana demokrasia ndani ya chama hivyo maamuzi yote makubwa yatokana na vikao hata mtu akipinga anakuwa hana nguvu. pili waimarishe kitengo cha propaganda. tafuteni wasomi wenye kiwango kama dr lwaitama mlipeni vizuri awe anapiga
Google

Lamuhimu ni kuepuka UDINI na UKABILA ndio wengi wanakilaumu CHADEMA na kama haitajivua koti hilo chafu huenda ndio ukawa mwisho wa CDM!!!
 
Lamuhimu ni kuepuka UDINI na UKABILA ndio wengi wanakilaumu CHADEMA na kama haitajivua koti hilo chafu huenda ndio ukawa mwisho wa CDM!!!

tatizo wewe ni mhanga v wa propaganda za kusema chadema chama cha udini. jiulize hiyo dini imeanza lini? mbona hao hao walikuwa wanasema ni chama cha wachagga kimehama lini kuwa cha udini? huyo wanayesema padri slaa alijiunga chadema lini? acha kuamini bila kuchambua
 
Tatizo unakuwa reactive sana, kwani wewe unaishi wapi ambapo maneno hayo hakuna? kuwa jambo linasemwa ni suala moja na kuwa jambo hilo lina ukweli ni jambo jingine, sasa hii atitude yenu haitokisaidia chama badala yake ni kuwatafuta hao wanaoambiwa kuwa ninyi ni wakabila na wadini mkawaelimisha. i hope utoto huu wa hapa JF haupo kwenye chama chenu.
 
hilo wazo lilishatolewa humu siku nyingi wakati wa kujadili mada za Zitto Kabwe na Mabere Marando
 
Ninge waelewa CCM wakiseme walimkataa Dr. Slaa kwa sababu alikuwa analeta michango ya ufadhili toka kanisa Katoliki
 
Back
Top Bottom