CHADEMA jifunzeni kwenye Ziara ya Makamu wa Rais Kahama

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,889
35,901
Habari kutokea Kahama zinasema Dr. Mpango yupo wilayani humo tokea juzi.

Uwepo wake umekuja na adha itakayobakia mioyoni mwa wakazi wa huko Kwa muda mrefu.

Taarifa zinasema jana barabara zote za maana kwa zaidi ya masaa 4 zilikuwa zimefungwa. Hii ikiwa kuanzia saa mbili hadi baada ya saa nne asubuhi na saa tisa hadi zaidi ya saa kumi na moja jioni.

Kwamba mji wote na shughuli ngapi za watu zilisimamishwa? Kwamba hadi ma school bus na watoto wa shule wamefika mashuleni na majumbani wakiwa wamechelewa mno? Kwamba ni kwa lipi au security alert level ipi kumhusu nani hata watoto wa shule za msingi na mabasi yao kuzuiliwa?

Ma CCM yamejisahau. Kujisahau huku kwa hakika ni fursa.

Chadema jifunzeni tokea kwenye kadhia hizi. Wananchi hawazipendi hali hizi.

Kwa hakika Chadema jipangeni zaidi kwenye kero kama hizi ambazo kwa mamwinyi waliojisahau hawatakaa wagutuke!

Habari zaidi kutokea huko zinasema leo tena kutokea saa moja asubuhi, yale ya juzi na jana yanashuhudiwa tena. Kama mchezo wa kuigiza vile, tayari kazi inaendelea. barabara za huko zishapigwa munda hata ma school bus nayo kwa mara nyingine na vitoto vya shule wala si muhimu tena.

IMG-20230119-WA0001.jpg


Lini barabara zitafunguliwa na watoto kama hawa kufika mashuleni, wadau wameahidi kutuletea mrejesho.

Chadema wananchi wanahitaji sera mbadala.

------
Mrejesho: Hatimaye saa nne asubuhi kama ilivyokuwa jana, ndipo barabara zifliunguliwa na watoto hawa, kama Kalume Kenge wakapata sasa fursa ya kwenda shule.
 
Atakuwa chawa huyo sio bure, inakera sana kusimamisha shughuli za kiuchumi kwa siku nzima kisa kiongozi anayezindua Choo cha soko
Wameambiwa wajibu kwa hoja. Wazipate wapi kuhalalisha kuwazuia watoto wadogo hadi wa chekechea barabarani badala ya kuwaacha kwenda shule?
 
Tujifunze nini zaidi ya kusimamisha magari masaa 3 kisa yeye.
Kahama huduma ni mbovu,barabara tatizo.mmejazana na vijezi vyenu vya kijani
 
Tujifunze nini zaidi ya kusimamisha magari masaa 3 kisa yeye.
Kahama huduma ni mbovu,barabara tatizo.mmejazana na vijezi vyenu vya kijani
Cha kujifunza ni kutambua mambuzi yanakojichumia chuki.

Beberu anasisitiza:

"Kujifunza kutokana na makosa ya wengine."

Kwa hakika Hashim Rungwe akija na sera mbadala ya kuondoa adha kama hizi zitatuvutia wengi kuliko hata Ile ya ubwabwa.
 
Ni ujinga tu. Huko kungine kusiko na mambo haya ya kipuuzi, kwapata viongozi ni rahisi sana?

Kwa fikrazako mfu, yaani wananchi kutosimamishwa shughuli zao wakati wa ziara za viongozi ina maana kiongozi huyo atakufa?

Anguko lao haliko mbali. Kulewa kwao kwa mamlaka walq wasidhani kuwa wananchi hawawaoni na eti kuwa labda wanawashangilia mno.
 
Ni ujinga tu. Huko kungine kusiko na mambo haya ya kipuuzi, kwapata viongozi ni rahisi sana?

Kwa fikrazako mfu, yaani wananchi kutosimamishwa shughuli zao wakati wa ziara za viongozi ina maana kiongozi huyo atakufa?
Usalama Kwanza acha fujo mzee. Halafu how often inatokea hii. Mara moja kwa miaka mitano Kuna shida gani mkuu
 
Leo mimi nimekutana na adha hiyo,yaani natoka singida kwenda Kahama,tulipofika Igunga mnadani tunasimamishwa eti kuna msafara wa makamo wa Rais na tumesimama kuanzia saa tano mpaka saa nane mchana ndo anapita
 
Usalama Kwanza acha fujo mzee. Halafu how often inatokea hii. Mara moja kwa miaka mitano Kuna shida gani mkuu

Bado unaikimbuka post yako Hii? Au timu sifia sifia tayari ushatoka kivingine?
 
Tujifunze nini zaidi ya kusimamisha magari masaa 3 kisa yeye.
Kahama huduma ni mbovu,barabara tatizo.mmejazana na vijezi vyenu vya kijani

BIla shaka haya sasa huna cha kujifunza.

Tatizo la mtanzania ni ujuaji mno hadi chefu.

Hapa ni mtanzania wewe sasa kwenye ubora wako. Komaa hapo hapo mjomba.

Cc: WALOLA VUNZYA
 
MBONA MNAHANGAIKA SANA NA CHADEMA KWANI TANGANYIKA INA CHAMA KIMOJA CHA UPINZANI?

BIla shaka utakuwa umejua kwa nini tulikuwa tuna hangaika na Chadema. Ila Kwa ujinga wetu tutakaa hapo hapo na kukumbuka shuka asubuhi.

Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom