CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

Watanzania wanaelewa na pia wew km haujafanya research ya kuweza kufahamu ccm kua haikubariki katika jamii ni wewe km Sio buti na kuiba kura ccm Ushindi hakuna ata vijijini na kaa ivoivo uone wabunge wote wa CDM wanarudi mjengoni na tunaongeza wengine wengi hiyo2015. Wewe huoni Arusha kwenye madiwano? Subiri mwakani kwenye Chaguzi za serikali za mitaa muone kz. CDM inatisha
 
Nilivyufunguwa hii thread tu nimepatwa na usingizi kabla sijaisoma,nalala mie.
 
Inashangaza nadharia hii ya mbegu kwa mfano wa nafaka kama maharage,mahindi,ngano,nk. Zinapokufa ndipo huzaa kwa wingi.Kifo cha NCCR-Mageuzi kilizalisha CUF, baada ya CUF...?

CHADEMA...hapa tutajadili vizuri baada ya 2015.Hata kama CCM itabaki madarakani bado tunahitaji chama cha upinzani chenye nguvu. Ladha ya kandanda la Tanzania ni kuwa na Simba vs Yanga imara.
 
Chamsingi ni CHADEMA kuendele kutoa elimu(M4C inahusika) ya urai kwa wananchi ili wazidi kuzijua haki zao,na kuwasisitiza wajitokeze kujiandikisha kwa wingi pindi dafutari la kupiga kura litakapokuwa likiboreshwa kwaajili ya uchaguzi,na kujitokeza pia kwa wingi siku ya kupigia kura.

Jambo jingine ni kuhakikisha sheria mbaya za uchaguzi zinafanyiwa marekebisho kabla ya kwenda kwenye uchaguzi wa 2015,ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa tume huru ya uchaguzi itakayokuwa tayari kusimamia uchaguzi bila upendeleo kwa chama chochote

Mwisho lakini muhimu sana ni CHADEMA kujizatiti "ki kamilifu" na kimkakati katika kusimamia,kulinda na kuhesabu kura.Hili ndio eneo ambolo mzizi wafitina wa kushindwa kwa vyama vya upinzani katika bara la Afrika umelala,tukiweza kuukata huo mzizi basi tutakuwa na uhakika asilimia 99% ya ushindi pasina shaka.Katika eneo hili la kusimamia kura zetu tunahitaji
1.LASLIMALI WATU
(i)kwa maana ya mawakala wazalendo(waminifu/waadirifu) na watakao kuwa wamepewa mafunzo ya kutosha ili kuweza kukabiliana na ulaghai wa aina yoyote katika chumba cha kupigia na kuhesabia kura
(ii)Walinzi wa chama RB watakao kuwa tayari kuwalinda raia dhidi ya wale wahuni ya wa Mwingulu
2.NYENZO
(i)Magari,pikipiki na hata kama uwezo utaturuhusu si vibaya vibaya tukaendele kutumia na helkopta kurahisha zaidi ufikaji wa wasimamizi wa chama kutoka eneo maja kwenda eneo jingine
(ii)VOMBO VYA MAWASIANO
Katika eneo hili tunahitaji kuwa na wataalam wazuri na wakutosha katika mawasiliano ya compu pamoja na vyombo vingine vya kisasa kulingana na wakati(bila kusaha kamera za kurekodia matukio)

Tukijipaga vizuri katika hayo mambo hapo juu,sioni cha kutuzui kuitoa nchi hii katika makucha ya hiki Chama Cha Madawa ya kulevya na kuirejesha mikononi mwa waTanzania wanyonge.
"KWA KUMTUMAINIA MUNGU HAKUNA KISICHO-WEZEKANA"

TULIANZA NA MUNGU
TUNAENDELEA NA MUNGU
NA
TUTAMALIZA NA MUNGU

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Chadema
 
Hii ni changamoto ya kuongeza nguvu kubomoa ngome ya ccm ambayo ni vijijini. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya vijijini CDM haijulikani. Watu ameisikia lakini CDM hawajafikisha elimu ya uraia huko. Hatuna wanachama wala matawi huko. Uelewa wa mjini ni tofauti na wa vijijini. Na hawa ndo wanaweza kuipa ccm ushindi miaka ijayo. Tusipoibomoa ngome hiyo, ni kweli twaweza tusishinde! Mikutano ihame mijini na kuhamia vijijini.

Programu ya CHADEMA ni msingi inatekelezwa na kanda zote na tutafikia vijiji vyote hadi mwisho wa mwaka huu.

Hii habari ya CHADEMA kutofika vijijini safari hii ni historia.Kazi ni kutoa elimu ya uraia na kuhakikisha wanapiga kura
 
Hii ni sawa na kusema chadema imeshakufa kwa sababu swala la kushinda Urais 2015 HALIPO...

huwa sipati jibu pale mbunge wa CCM anaposema "nipo hapa bungeni kuwatetea wananchi" swali: Nani anayewatesa au kuwadhulumu ???
 
Kwa hali ilivyo kila njia waliyokuwa wanatumia MDC Zimbabwe kujaribu kumwangusha babu Mugabe ndo njia zinazoaminiwa na kutumiwa na Chadema nchini hivyo basi naliona anguko la CDM mwaka 215. Na kwakuwa wakishindwa kuingia Ikulu CDM mwaka 2015 inakufa kabisa....sijui hatima ya demokrasia itakuaje nchini maana mdau muhimu amebakisha miaka miwili tu ya kuishi.

Magwanda acheni mapovu toeni hoja!
 
Mkuu Ben, heshima yako

Jitahidi .. Buku 7 zinakusubiri Lumumba..
Manake unajibu kila comments ,
Kasi ya CDM ni hatari.. Nyinyiem hamlali usiku mzima mnakesha kupiga chabo JF kuangalia ni uzi upi unawamaliza.... Ili mtoe Propaganda zenu.. Imekula kweni!! M4C twaaanga kotekote.. 2015 kitaeleweka tu!!
 
Uchambuzi murua ila kwa mantiki hiyo hiyo CHADEMA ni marehemu mtarajiwa.
 
watatuelewa tu hao mafisadi ccm lazima wakae tu tumechoka kuendeshwa kihuni ma mbulula wakubwa
 
Swala la kufa kwa chama haliko CHADEMA peke yake.Kifo kinaweza kutokea kwa chama chochote ili mradi tu kina mwanzo na hakiwezi kukosa mwisho wake.Iwe CCM,CHADEMA,NCCR au chama kingine kinaweza kikafa pia.Tusiamini asilimia mia kwa mia kuwa CCM kwa vile iko madarakani ndiyo tuseme kuwa haiwezi kufa la asha CCM inaweza ikafa kama vyama vyovyote vilivyo anzishwa ambavyo vinaweza vikafa.Ndiyo maana CCM nayo inatabia ya kupanda chati na kushuka hasa ukiangalia kwenye chaguzi mbalimbali ambazo zimepita utagunduwa kuwa kuna wakati CCM wanapata kiwango cha juu cha matokeo halafu pengine wanapata kiwango cha chini cha matokeo.Hapa kwenye kiwango cha kushuka cha CCM hapa ndipo inapoweza ikashuka nakufa moja kwa moja.Pia uhai mkubwa wa CCM uko kwenye muungano ambapo muungano ukifa tu CCM watakosa uhalali wa kuwa chama cha kisiasa ndiyo maana CCM wanapinga kufa na kupona serekali 3 si kwamba serekali 3 zinaleta athari yoyote kwa watanzania CCM wanajuwafika kuwa serekali 3 zinaweza kufanya muungano ukavunjika na kufanya chama hicho kufa.Siyo kweli kwamba CCM wanaupigania muungano eti labda ndiyotuseme kuwa unawasadia sana watanzania huo muungano unawasaidia sanasana CCM.Pia kizazi kilichopo siyo kizazi kile cha enzi zile za kudumisha fikra za mwenyekiti wa CCM ambapo kila mtu apende asipende alilazimika kuzidumisha hizohizo kwa vile kulikuwa hakuna chama kingine.Kwa kizazi hiki ambacho kimebaki kinasoma historia tu kwamba hapo zamani kulikuwa na chama kimoja ambacho ni CCM vijana wengi hawatakuwa tayari kuendelea kuongozwa na chama cha kihistoria ambacho kilianzishwa na mababu zao nao watataka wawe na chama chao walicho kianzisha wenyewe au kilicho anzishwa ndani ya uzao wao ili na wao wawe na cha kujivunia kuwa hiki tumekifanya sisi na si kimefanywa na mababu zetu.Hii hali inaonekana kwa vijana wengi wa lika mbalimbali waliyoko mashuleni na mitaani pia ni mara chache sana kuwakuta vijana wengi ambao wako CCM waliyo wengi utawakuta wako upinzani ishara ambayo inaonyesha kuwa CCM iko mbioni kufa au kutoweka pamoja na waanzilishi wake.Kufa kwa CHADEMA au chama chochote cha upinzani hilo linaweza likatokea isipokuwa kitu ambacho hakiwezi kufa ni ukombozi.Walio wengi wamechoka na chama cha CCM hivyo wanahitaji kujikombowa kutoka kwenye chama cha CCM kiwe kinafanya vizuri kipindi hicho au hakifanyi vizuri kipindi hicho ni lazima kitoke madarakani na watakao kiondoa madarakani ni hawa waliyochoshwa na CCM,wanao taka kuweka rekodi ya kuongozwa na kitu walichokianzisha wenyewe na wenye roho ya ukombozi ambayo huwa haifi.Kwa sasa walio wengi wanaona chama pekee ambacho kinaweza kuwafikisha kwenye malengo yao ni CHADEMA hata kama CHADEMA ikifa leo usitegemee kuwa watarudi CCM wataanzisha chama kingine ambacho kitawaongoza ili waweze kufikia lengo lao la ukombozi.
 
Lukolo,

Katika kuandika pumba zako, umeruka kuanzia 2000 mpaka 2010. Unashangaza, au unashindwa kusema "Chaguo la Mungu"?
Haha, FaizaFoxy, najua imekuuma kuona sijaitaja CUF kama chama chenye nguvu kilichotikisa mwaka 2000. Lakini ukweli ni kwamba, nimeeleza namna ambavyo Mkapa kura zake zilipanda kwa aslilimia kumi kati ya mwaka 1995 na mwaka 2000. So hata kama CUF ilikuwa na nguvu mwaka 2000, lakini bado wananchi wengi walirudisha imani kwa CCM. Na imani hiyo kwa CCM iliendelea hadi mwaka 2005 wakati Kikwete akiingia madarakani. Lakini katika muda wa miaka mitano ya Kikwete, hali ya mambo ilibadilika, na wananchi wakapoteza matumaini kwa Kikwete. Mwaka 2010, wakaiamini zaidi CHADEMA kura za Kikwete zikapungua kwa asilimia 20. Lakini hivi sasa wananchi wanaendelea kupoteza matumaini dhidi ya Kikwete, na CCM yake. Ni dhahiri kwamba mwaka 2015 wataipa kura CHADEMA. Ni wapi niliporuka sasa? Maana maelezo haya yote nimeyaandika katika thread yangu ya msingi.
 
Kwa hali ilivyo kila njia waliyokuwa wanatumia MDC Zimbabwe kujaribu kumwangusha babu Mugabe ndo njia zinazoaminiwa na kutumiwa na Chadema nchini hivyo basi naliona anguko la CDM mwaka 215. Na kwakuwa wakishindwa kuingia Ikulu CDM mwaka 2015 inakufa kabisa....sijui hatima ya demokrasia itakuaje nchini maana mdau muhimu amebakisha miaka miwili tu ya kuishi.

Magwanda acheni mapovu toeni hoja!
Si kweli kwamba CHADEMA wanafanya yale yale waliyokuwa wanafanya MDC. Nina imani kwamba CHADEMA hawatakubali ujinga wa kuunda serikali ya muungano kama walivyofanya akina Raila na Morgani. Maana kwa kuingia kwenye serikali ya umoja ndiyo umejimaliza. Ni kama CUF inavyoteketea hivi sasa kule Zanzibar.
Afterall Morgan Tsvangirai hakuwa presidential material. Hebu muone hapa chini alivyotia aibu!

 
Last edited by a moderator:
Siwezi kukupinga moja kwa moja katika hoja yako, ingawa nitakupinga kukifananisha CHADEMA na baadhi ya vyama vya upinzani vilivyotangulia katika mapambano ya ukombozi dhidi ya CCM. Nazungumzia kukifananisha vyama KAMA NCCR 1995, CUF 2000-2005, na hata TLP. Nasema nitakupinga kwa hili kutokana na mikakati ya kichama waliyokuwa nayo wapinzani wa zama hizo. Vyama vilikuwa na mipango mibovu sana, ni kweli vilikuwa ni vyama vya msimu kwani siasa zao zilikuwa zikifanywa siku miaka michache sana (1 au 2) kabla ya uchaguzi. Katika mdahalo uliofanyika kwenye hotel ya Moven Peak Dar es salaam, mwaka 2010 siku moja kabla ya uchaguzi ukiwashirikisha wagombea urais kasoro wa CCM ambae alikatazwa na chama chake. Katika mdahalo huo Dr. Slaa aliulizwa na mwandishi wa habari, kuwa CHADEMA kinamatumaini makubwa sana ya kushinda uchaguzi wa kesho, je mkishindwa mtachukua hatua gani? Dr. Slaa pamoja na mambo mengine aliyomweleza mwandishi yule, alimweleza pia huo ndio utakuwa mwanzo mzuri wa kuijenga CHADEMA na kuifanya iwafikie watu tangu kwenye ngazi ya msingi. Kauli yake ile ilionekana walipoanzisha operations mbalimbali za chama. Mfano operation sangara, Movement for Change M4C, operation vua gamba vaa gwanda, sera ya majimbo ambayo inaonyesha kufanikiwa. Lakini pia kuelekeza nguvu kubwa kwa vijana ambao ndio kizazi cha vyama vingi. Nikisema hivyo namaanisha kwa kijana aliezaliwa mwaka 1992 kipindi mfumo wa vyama vingi unaasisiwa atakuwa ametimiza miaka ya kumuwezesha kupiga kura kufikia 2015. Huku ndiko wanapowekeza CHADEMA. Lakini pia wapo waliosema kuwa CHADEMA kama kingeshindwa 2010 basi kingekufa kama vyama vilivyotangulia vya upinzani lakini huu ni mwaka 2013 na kasi ya mabadiliko inazidi kuwaingia watanzania na ndiyo maana nikakwambia KUKIFANANISHA CHADEMA NA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI NCHINI NI KUTOITENDEA HAKI. Ni vyema ungeifananisha na vyama vya upinzani vya Zambia na Kenya ambavyo vilifanikiwa kuviangusha vyama vikongwe kutokana na mikakati yake katika kuimarisha vyama vyao na hatimaye kuwapatia ukombozi kutoka kwa wakoloni weusi kama CCM. Chamsingi niwaombe viongozi wa CHADEMA waendelee na kasi hii na wasikatishwe tamaa na watu wachache wasioitakia mema Tanzania.
 
Mkuu Lukolo, inavyoelekea wewe hujui kabisa nini maana ya chama kuitwa cha upinzani. Kwako unaona kuwa upinzani ni uadui au unaona kuwa wapinzani ndo wana sera nzuri kuliko chama tawala. Mkuu Lukolo, kusema kuwa CHADEMA kinaongoza nchi nje ya system huko ni kukosa kuelewa. Ujue kuwa viongozi wa CHADEMA na CCM wote ni watanzania na wanapigania maendeleo ya mtanzania. Kwako unaona kuwa jambo zuri likitekelezwa na serikali basi ni la CHADEMA. nilidhani utaipongeza serikali kwa kuwa sikivu kusikiliza hoja za wananchi kumbe nawe ni kama hawa bavicha ambao uelewa wao ni pungufu

Ma CCM huwa wanaamini BAVICHA hawana hekima, lakini kwenye arguememnt utakuta wao ndio zero kabisaa
 
ni hoja nzuri kiongozi pokea bravo kwa kuakisi maendeleo ya cdm kwa mapana zaidi ya ushabiki.umekumbusha jambo la msingi hasa unaposema cdm inatakiwa kuwa na mikakati ya kutosha ili kukieneza chama kwa wananchi hata ikibidi kuwa vyombo vyake vya habari.
 
Back
Top Bottom