Hili suala la CHADEMA kuwa na vyombo vyake vya habari sijui linakwamishwa na nini? Hivi kweli inashindikana kuwa na radio kila mkoa? How much does it cost to run it? Najua TV linaweza kuwa ni suala kubwa mno, lakini Radio? Au kuongeza gazeti lingine zaidi ya hili la mwenyekiti wa chama? Wenzetu CCM wana Uhuru na Mzelendo na wana magazeti dada ya Jambo leo na Habari leo ambayo yote kwa pamoja yanafanya kazi ya kuiuza CCM? Sasa sisi tuna Tanzania daima pekee, tunashindwa nini kupata gazeti lingine la ziada? Ikiwezekana, la aina kama ya Kiu au Mwanasport ambalo tutaliuza kwa bei chee, ili limfikie kila mtu.