CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

CHADEMA isiposhinda Urais 2015 itakufa

Dah, Lizaboni, nipe tano!! Leo umeongea vizuri. Kesho si unamaliza mfungo? Nitafute nikupe serengeti baridi!
Hapo pa serengeti sipo pamoja na wewe labda kiasi hicho cha fedha ambacho ulitaka kuninunulia serengeti basi uongeze kwenye posho za hawa vijana wa kinondoni mtaa wa ufipa ambao hata shilingi elfu moja ya kulipia laini ya simu inawashinda ndo maana walianzisha mgomo ambao ulishindikana baada ya watanzania wengi kuwagomea
 
Chadema Kama hakitashinda urais na kikawa na wabunge wengi kitapita salama na hakiwezi sambaratika
Mkuu, nakuhakikishia kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wa sasa wa CHADEMA hawatarudi tena bungeni kwani wameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye majimbo yao
 
tunawapenda wapinzani wa aina hii mnaojadili kwa hoja na hii ndiyo siasa ya demokrasia

sio hawa watukanaji ambao siasa wameanza kufuatikia karne ya 21 wanajijua

anyway ngoja waje na wengine tusikie maoni yao ila binafsi mie nimekuelewa
 
Mimi ninachohitaji ni maisha bora. Hata raisi akitoka CCJ au mgombea binafsi, kwangu ni sawa. Sitapiga kura kuchagua chama, nitapiga kura kuchagua mtu makini kwa nafasi ya diwani, mbunge na hata Raisi. Kuendekeza mahaba kwa vyama badala ya mtu makini ndo yamemwingiza Kikwete ikulu muhura wa Pili.
 
Jenga hoja zaidi ya hapa.....!

Lukolo:Shukrani sana kwa angalizo hili Kamamda
ndugu ben nimependa uhamasishaji wako kwa mdau kujenga hoja. nawaomba wanaa JF tujiepushe na majibu ya mkato kama alivyojibu kazitunayo. tujenge hoja kwa kuunga mkono uzi au kuukata / kuukosoa kwa hoja zilizo thabiti
 
Mkuu Lukolo, inavyoelekea wewe hujui kabisa nini maana ya chama kuitwa cha upinzani. Kwako unaona kuwa upinzani ni uadui au unaona kuwa wapinzani ndo wana sera nzuri kuliko chama tawala. Mkuu Lukolo, kusema kuwa CHADEMA kinaongoza nchi nje ya system huko ni kukosa kuelewa. Ujue kuwa viongozi wa CHADEMA na CCM wote ni watanzania na wanapigania maendeleo ya mtanzania. Kwako unaona kuwa jambo zuri likitekelezwa na serikali basi ni la CHADEMA. nilidhani utaipongeza serikali kwa kuwa sikivu kusikiliza hoja za wananchi kumbe nawe ni kama hawa bavicha ambao uelewa wao ni pungufu
Ujue nilichojifunza leo, ni kwamba wewe Lizaboni, una uelewa mkubwa sana, lakini kuna wakati huwa unaamua kuondoa uelewa wako ili kucheza ngoma ya akina Mwigulu Nchemba. Yaani hoja uliyoijenga hapa imekaa vizuri sana, kwamba CHADEMA na CCM wote ni watanzania, na kila tunachokifanya ni kwa ajili ya watanzania, whether ni CCM au ni CHADEMA wote wana haki sawasawa ya kushika madaraka na kuongoza nchi. Kwahiyo hatuna haya ya kuchukiana kibinadamu bali tushindane kwa hoja. Na yeyote kati yetu akiwa na hoja nzuri basi asikilizwe. Hii ni message mhimu sana kwa Mwigulu Nchemba. Huwa anadhani wapinzani ni watu wa kutoka nchi jirani, na wakiongea jambo anawachukulia kwamba ni wageni wanaoingilia mambo ya ndani ya watanzania.

Mimi binafsi sina mtizamo huo. Bali nilichojaribu kukieleza katika post yangu ni ukweli kwamba CHADEMA wana dira, na si kweli kwamba hawana dira kama ambavyo wewe unataka kutusadikisha. Kama wasingekuwa na dira, ni dhahiri wasingeweza kutoa mawazo kwa chama tawala na yakakubaliwa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, umegusia maeneo ya msingi japokuwa kuna upotofu katika hoja juu ya vyama vikuu vya upinzani kupoteza nguvu baada ya kushindwa uchaguzi. Vyama kama NCCR Mageuzi na CUF havikupoteza nguvu kwa sababu ya CCM kuimarika bali kwasababu ya uongozi wa vyama hivyo kudhoofika.Vyama hivyo vilikuwa mifukoni mwa viongozi ndiyo hadi sasa ujiulize CUF bila Lipumba kinaendaje? Mpaka sasa, CHADEMA kwa asilimia zaidi ya 70 kimevuka mstari huo kwani kinazidi kujengwa katika mfumo wa kitaasisi na ndiyo maana kuna viongozi wanaosimamia chama kutoka kila kanda. Lakini pia focus ya CHADEMA siyo Ikulu tu bali pia kuongeza idadi ya wabunge na madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo nguvu ya chama haipo mikononi mwa mgombea urais kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF. Kuna watu wanadhani Mhe.Kikwete peke yake ndiye aliyeshindwa lakini si kweli kwani ni CCM.

Mkuu Makala Jr, CHADEMA nao wamefuata nyayo za CUF na NCCR MAGEUZI. Huwezi kutegemea chama kiwe shindani wakati hata demokrasia ya ndani inawashinda. Kuna watu ndani ya CHADEMA wanaona kuwa chama hicho ni mali yao. Hivyo hawataki hata kdogo kusikia kuwa watu wanataka kuwania nafasi zao. Haiingii akilini kuona chama kikubwa kinaahirisha uchaguzi wa ndani simply akina zitto kabwe wametangaza nia ya kuwania nafasi ya mwenyekiti. Kwa utaratibu huu chadema hawafiki mbali kwani kitendo hicho kinatengeneza makundi ndani ya chama ambayo ndiyo kiini cha ccm kudhoofika kwa sasa
 
Kwa sasa CCM ilipofika ni ngumu kaka mleta mada.
Hilo litawezekana kama ndani ya CCM hakutakuwa na mgawanyiko au UFISADI coz at this time when u talk about CCM ina maana u talk about ufisadi.
Sasa JE, ni nani wa kuzuia UFISADI ndani ya CCM wakati ufisadi ndiyo unatumika kumpata Mgombea wa Urais ndani ya CCM???
Hata kama Rais atakuwa ni wa kutoka huko CCM hakuna atakayeweza kuleta maisha bora ya Kweli ya mtanzania.
e.g: mfano rahisi na halisia: Nani wa kurudisha reli njia zote zifanye kazi, cement, mafuta ya petrol na diesel zibebwe na treni, naaaniiii!¿???? Ajitokeze.
 
Maneno yako ya mwisho nimeyaelewa na kujifunza pia.
 
Ujue nilichojifunza leo, ni kwamba wewe Lizaboni, una uelewa mkubwa sana, lakini kuna wakati huwa unaamua kuondoa uelewa wako ili kucheza ngoma ya akina Mwigulu Nchemba. Yaani hoja uliyoijenga hapa imekaa vizuri sana, kwamba CHADEMA na CCM wote ni watanzania, na kila tunachokifanya ni kwa ajili ya watanzania, whether ni CCM au ni CHADEMA wote wana haki sawasawa ya kushika madaraka na kuongoza nchi. Kwahiyo hatuna haya ya kuchukiana kibinadamu bali tushindane kwa hoja. Na yeyote kati yetu akiwa na hoja nzuri basi asikilizwe. Hii ni message mhimu sana kwa Mwigulu Nchemba. Huwa anadhani wapinzani ni watu wa kutoka nchi jirani, na wakiongea jambo anawachukulia kwamba ni wageni wanaoingilia mambo ya ndani ya watanzania.

Mimi binafsi sina mtizamo huo. Bali nilichojaribu kukieleza katika post yangu ni ukweli kwamba CHADEMA wana dira, na si kweli kwamba hawana dira kama ambavyo wewe unataka kutusadikisha. Kama wasingekuwa na dira, ni dhahiri wasingeweza kutoa mawazo kwa chama tawala na yakakubaliwa.

Mkuu Lukolo, inawezekana kabisa ndani ya CHADEMA kuna watu ambao wana malengo mazuri na mtazamo hasi dhidi ya taifa hili. Binafsi kuna wakati namkubali sana Freeman Mbowe kwani ni mtu anayeshaurika na wakati fulani hujivalisha uzalendo. Ila sikubaliani kabisa na dr slaa ambaye kwake upinzani ni uadui. Mathalan, huwezi kuwa na malengo ya kwenda ikulu huku ukitukana viongozi waliopo madarakani na wa vyombo vya dola. Huko ni kufilisika kabisa kimawazo. Hata kama mtu humpendi lakini si kila kitu unampinga. Binafsi nilifarijika sana kuona mathalan mbowe na cuf walifikia muafaka mzuri kwa maslahi ya taifa baada ya kutokea mgogoro wa ushoga baina ya vyama hivi viwili. Ingekuwa dr slaa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni, ni wazi kuwa jambo lile lingeleta mtafaruku mkubwa sana nchini.

Pia CHADEMA wana tatizo kubwa la kupoteza uaminifu kwa watu ambao hawatoki mikoa ya kaskazini. Mathalan, zitto kabwe ni Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA, lakini kwa zaidi ya miaka 3 sasa hajawahi kufanya kazi zake kama naibu hata pale dr slaa anapokuwa nje ya nchi. Badala yake John Mnyika ndiye huaminiwa na kupewa mikoba yote. Hata mbowe anaposafiri pia majukumu yakehutekelezwa na Mnyika na si Said Arfi. Kwa mtindo huu bwana Lukolo usitegemee kuwa CHADEMA watakuja kuwa chama imara na shindani kwa siku zijazo. Mie nakubaliana na wewe kuwa endapo hawatajirekebisha na hatimaye kushinda uchaguzi wa 2015, ni wazi kuwa huo ndio utakuwa mwisho wao
 
Mkuu, umegusia maeneo ya msingi japokuwa kuna upotofu katika hoja juu ya vyama vikuu vya upinzani kupoteza nguvu baada ya kushindwa uchaguzi. Vyama kama NCCR Mageuzi na CUF havikupoteza nguvu kwa sababu ya CCM kuimarika bali kwasababu ya uongozi wa vyama hivyo kudhoofika.Vyama hivyo vilikuwa mifukoni mwa viongozi ndiyo hadi sasa ujiulize CUF bila Lipumba kinaendaje? Mpaka sasa, CHADEMA kwa asilimia zaidi ya 70 kimevuka mstari huo kwani kinazidi kujengwa katika mfumo wa kitaasisi na ndiyo maana kuna viongozi wanaosimamia chama kutoka kila kanda. Lakini pia focus ya CHADEMA siyo Ikulu tu bali pia kuongeza idadi ya wabunge na madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo nguvu ya chama haipo mikononi mwa mgombea urais kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF. Kuna watu wanadhani Mhe.Kikwete peke yake ndiye aliyeshindwa lakini si kweli kwani ni CCM.
Ni kweli natamani sana chama chetu kifikie kuwa chenye nguvu kama vile vyama vya labour na conservatives vya UK au Republicans na democrats ya USA. Na kwa hakika tunakoelekea CHADEMA ni huko. Ni jambo la kutia moyo sana, lakini bado tunahitaji kuwekeza zaidi.

Kuhusu uongozi nakubaliana na wewe kwamba NCCR ilikufa kutokana na kuparanganyika kwa uongozi, kulikopelekea Mrema kuhama chama. Lakini sina hoja ya msingi ya kujenga hapa dhidi ya CUF, maana haijawahi kuwa na mtikisiko wa kiuongozi.

Hoja ya nguvu ya rais haikwepeki katika muktadha wa Tanzania. Maana Rais imara hujenga chama imara, uongozi imara, na maisha bora na hivyo imani zaidi ya wananchi kwa chama tawala. Rais mbovu hujenga utawala mbovu, chama kibovu, serikali legelege, maisha magumu na hatimaye hasira za wananchi dhidi ya chama tawala.

Kwahiyo tukubali au tukatae, kama Rais wa mwaka 2015 kutoka CCM atakuwa imara, wapinzani hatutakuwa na hoja za msingi za kuikosoa serikali ambazo zitatosha kuwashawishi wananchi watuchague. Wananchi wanachagua upinzani kama wanaona hakuna tumaini katika chama tawala. Hii ndiyo imani yangu. inawezekana kwamba CHADEMA haitakufa hata baada ya kiongozi makini kutoka CCM kushika nchi mwaka 2015, lakini hakitakuwa na nguvu kubwa kama ambavyo kinayo hivi sasa ambapo nchi haina Rais.
 
Kwa sasa CCM ilipofika ni ngumu kaka mleta mada.
Hilo litawezekana kama ndani ya CCM hakutakuwa na mgawanyiko au UFISADI coz at this time when u talk about CCM ina maana u talk about ufisadi.
Sasa JE, ni nani wa kuzuia UFISADI ndani ya CCM wakati ufisadi ndiyo unatumika kumpata Mgombea wa Urais ndani ya CCM???
Hata kama Rais atakuwa ni wa kutoka huko CCM hakuna atakayeweza kuleta maisha bora ya Kweli ya mtanzania.
e.g: mfano rahisi na halisia: Nani wa kurudisha reli njia zote zifanye kazi, cement, mafuta ya petrol na diesel zibebwe na treni, naaaniiii!¿???? Ajitokeze.

Mkuu, ogopa sana chama tawala. Hata kama ukione kina udhaifu kiasi gani, si vema kukidharau. Mathalan, nchini Zimbabwe, pamoja na Morgan Tsvangirai kupata support kubwa na mataifa ya magharibi kama cile wajerumani wanavyojitoa kwa CHADEMA, hali imekuwa mbaya sana kwa MDC. Hivi vyama tawala vina uwezo wa kujifunza na vikasimama baada ya kubaini kosa lao. Mathalan, sote tutakubaliana kuwa CCM ya akina Makamba na Mukama ni tofauti kabisa na CCM ya akina Kinana. Kwa sasa chama kimetulia ja unaona kabisa kuwa wana malengo fulani. Hali hii chadema wanapaswa kuitafakari zaidi badala ya kujiaminisha kuwa ccm wanaelekea kufa. Huko ni kujidanganya
 
Mkuu Lukolo, inawezekana kabisa ndani ya CHADEMA kuna watu ambao wana malengo mazuri na mtazamo hasi dhidi ya taifa hili. Binafsi kuna wakati namkubali sana Freeman Mbowe kwani ni mtu anayeshaurika na wakati fulani hujivalisha uzalendo. Ila sikubaliani kabisa na dr slaa ambaye kwake upinzani ni uadui. Mathalan, huwezi kuwa na malengo ya kwenda ikulu huku ukitukana viongozi waliopo madarakani na wa vyombo vya dola. Huko ni kufilisika kabisa kimawazo. Hata kama mtu humpendi lakini si kila kitu unampinga. Binafsi nilifarijika sana kuona mathalan mbowe na cuf walifikia muafaka mzuri kwa maslahi ya taifa baada ya kutokea mgogoro wa ushoga baina ya vyama hivi viwili. Ingekuwa dr slaa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni, ni wazi kuwa jambo lile lingeleta mtafaruku mkubwa sana nchini.

Pia CHADEMA wana tatizo kubwa la kupoteza uaminifu kwa watu ambao hawatoki mikoa ya kaskazini. Mathalan, zitto kabwe ni Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA, lakini kwa zaidi ya miaka 3 sasa hajawahi kufanya kazi zake kama naibu hata pale dr slaa anapokuwa nje ya nchi. Badala yake John Mnyika ndiye huaminiwa na kupewa mikoba yote. Hata mbowe anaposafiri pia majukumu yakehutekelezwa na Mnyika na si Said Arfi. Kwa mtindo huu bwana Lukolo usitegemee kuwa CHADEMA watakuja kuwa chama imara na shindani kwa siku zijazo. Mie nakubaliana na wewe kuwa endapo hawatajirekebisha na hatimaye kushinda uchaguzi wa 2015, ni wazi kuwa huo ndio utakuwa mwisho wao
Umeibua tuhuma nzito sana, ambazo sina uwezo wa kuzijibu. Naomba taarifa hii iwafikie Tumaini Makene, Ben Saanane, Kitila Mkumbo, @Dr Slaa, na Molemo naamini watakuwa na maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na utendaji kazi wa ofisi ya CHADEMA makao makuu.
 
Last edited by a moderator:
Mimi ninachohitaji ni maisha bora. Hata raisi akitoka CCJ au mgombea binafsi, kwangu ni sawa. Sitapiga kura kuchagua chama, nitapiga kura kuchagua mtu makini kwa nafasi ya diwani, mbunge na hata Raisi. Kuendekeza mahaba kwa vyama badala ya mtu makini ndo yamemwingiza Kikwete ikulu muhura wa Pili.

mimi hata jiwe liki niconvince nalichagua mahaba ya chama haya tupeleki popote ,, wazimbabwe baada ya kumuona tchangirai anawayeyusha wameamua kummwaga kiabu labda kuna wanachama wa chama chake pia ila wamemungalia yeye wakamuona majununi tu na kibaraka wa wazungu wakammwaga,, so mimi sio muumini wa chama walaaaa!!!!
 
Mleta mada , haya wahi lumumba ukachukue buku 7.
 
Lizaboni, unaongea kwa maslahi ya chama coz unafaidika na Ufisadi wenu wa kijinga(ubinafsi).
Kama taifa, mieleze leo nani mwenye uwezo wa kurudisha kiwanda cha matairi ya magari pale Arusha???? huu ni mfano mdogo tu.
Kila kiongozi wa chama cha madawa amekuwa mfanyabiashara. Kama kiongozi wa Chama cha Madawa ndiyo anafanya biashara ya kuingiza matairi kutoka China hicho kiwanda cha kwetu kitafufukia wapi??? Hivo kwanini kilikufa??? Jiulize coz kilikuwa kiko LIVE kinafanya kazi, Nyererw Kuda nacho kikafa, nini tatizo¿???
Zimbabwe ni tofauti sana na TZ, usifuate bendera usiyoijua.
Mugabe amekimbiza Wakoloni akitaka wazawa wamiliki ardhi na uchumi wa Zimbabwe, Tsivangirai hataki anataka wakoloni warudi kumiliki mali za Wazawa, Zamani CCM ilikuwa inakimbiza Kaburu leo inaomba kaburu aje na inamkaribisha kwa mikono mitatu kama si minne uchumi wa TZ imetawaliwa na watu wa nje leo hio tunategemea mmarekani atupe umeme mchina atupe kila kitu mpaka wembe sasa kama watanzania hatufanyi kazi US na CHINA tukiwa hapahapa utasemaje??
Hela yote inakwenda kwao, una kiwanda gani mtamzania zaidi ya bia na viroba(dirty gin), banana, kimorali, Sigara ambavyo ndiyo unajidai ni vyanzo vyako vya kodi.
Swali la kizushi: Lowasa anafanya biashara gani mpaka awe na hela ya kugawa makanisani na misikitini??
Tunaambiwa ni marafiki zake, JE ni wapi hao wanaoweza kuwa na hela za kugawa hivyo??
Ni Lowasssa tu mwenye marafiki wenye hela za kugawa Makanisani na Misikitini???
Hivi Richmond iliishaje???
Nani kamuweka JK pale??
Mbona hana Say kama President wa Nchi???
Membe, Six, Lowasssa vp mbona makundi¿???
Ukimwaga mboga mimi namwaga Ugali, wapi umoja ndani ya CCM???
 
Jenga hoja zaidi ya hapa.....!

Lukolo:Shukrani sana kwa angalizo hili Kamamda
Hii ni changamoto ya kuongeza nguvu kubomoa ngome ya ccm ambayo ni vijijini. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya vijijini CDM haijulikani. Watu ameisikia lakini CDM hawajafikisha elimu ya uraia huko. Hatuna wanachama wala matawi huko. Uelewa wa mjini ni tofauti na wa vijijini. Na hawa ndo wanaweza kuipa ccm ushindi miaka ijayo. Tusipoibomoa ngome hiyo, ni kweli twaweza tusishinde! Mikutano ihame mijini na kuhamia vijijini.
 
Lukolo,

Katika kuandika pumba zako, umeruka kuanzia 2000 mpaka 2010. Unashangaza, au unashindwa kusema "Chaguo la Mungu"?
 
Last edited by a moderator:
Nimeoteshwa Chadema imeisha kufa baada ya 2015, huu mjadala ni kama mnafanya matanga.
 
Mkuu uchambuzi wako ni mzuri, ila Kushindwa au kushinda kwa Cdm ni maamuzi ya wananchi.Either wanataka mabadiliko au wameridhika na hali mbaya iliyopo chini ya CCM.Kinachotukwamisha wa Tz ni maamuzi yetu wenyewe.jumlisha na hila za CCM.
 
Back
Top Bottom