Hapo pa serengeti sipo pamoja na wewe labda kiasi hicho cha fedha ambacho ulitaka kuninunulia serengeti basi uongeze kwenye posho za hawa vijana wa kinondoni mtaa wa ufipa ambao hata shilingi elfu moja ya kulipia laini ya simu inawashinda ndo maana walianzisha mgomo ambao ulishindikana baada ya watanzania wengi kuwagomeaDah, Lizaboni, nipe tano!! Leo umeongea vizuri. Kesho si unamaliza mfungo? Nitafute nikupe serengeti baridi!
Mkuu, nakuhakikishia kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wa sasa wa CHADEMA hawatarudi tena bungeni kwani wameonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye majimbo yaoChadema Kama hakitashinda urais na kikawa na wabunge wengi kitapita salama na hakiwezi sambaratika
ndugu ben nimependa uhamasishaji wako kwa mdau kujenga hoja. nawaomba wanaa JF tujiepushe na majibu ya mkato kama alivyojibu kazitunayo. tujenge hoja kwa kuunga mkono uzi au kuukata / kuukosoa kwa hoja zilizo thabiti
Ujue nilichojifunza leo, ni kwamba wewe Lizaboni, una uelewa mkubwa sana, lakini kuna wakati huwa unaamua kuondoa uelewa wako ili kucheza ngoma ya akina Mwigulu Nchemba. Yaani hoja uliyoijenga hapa imekaa vizuri sana, kwamba CHADEMA na CCM wote ni watanzania, na kila tunachokifanya ni kwa ajili ya watanzania, whether ni CCM au ni CHADEMA wote wana haki sawasawa ya kushika madaraka na kuongoza nchi. Kwahiyo hatuna haya ya kuchukiana kibinadamu bali tushindane kwa hoja. Na yeyote kati yetu akiwa na hoja nzuri basi asikilizwe. Hii ni message mhimu sana kwa Mwigulu Nchemba. Huwa anadhani wapinzani ni watu wa kutoka nchi jirani, na wakiongea jambo anawachukulia kwamba ni wageni wanaoingilia mambo ya ndani ya watanzania.Mkuu Lukolo, inavyoelekea wewe hujui kabisa nini maana ya chama kuitwa cha upinzani. Kwako unaona kuwa upinzani ni uadui au unaona kuwa wapinzani ndo wana sera nzuri kuliko chama tawala. Mkuu Lukolo, kusema kuwa CHADEMA kinaongoza nchi nje ya system huko ni kukosa kuelewa. Ujue kuwa viongozi wa CHADEMA na CCM wote ni watanzania na wanapigania maendeleo ya mtanzania. Kwako unaona kuwa jambo zuri likitekelezwa na serikali basi ni la CHADEMA. nilidhani utaipongeza serikali kwa kuwa sikivu kusikiliza hoja za wananchi kumbe nawe ni kama hawa bavicha ambao uelewa wao ni pungufu
Mkuu, umegusia maeneo ya msingi japokuwa kuna upotofu katika hoja juu ya vyama vikuu vya upinzani kupoteza nguvu baada ya kushindwa uchaguzi. Vyama kama NCCR Mageuzi na CUF havikupoteza nguvu kwa sababu ya CCM kuimarika bali kwasababu ya uongozi wa vyama hivyo kudhoofika.Vyama hivyo vilikuwa mifukoni mwa viongozi ndiyo hadi sasa ujiulize CUF bila Lipumba kinaendaje? Mpaka sasa, CHADEMA kwa asilimia zaidi ya 70 kimevuka mstari huo kwani kinazidi kujengwa katika mfumo wa kitaasisi na ndiyo maana kuna viongozi wanaosimamia chama kutoka kila kanda. Lakini pia focus ya CHADEMA siyo Ikulu tu bali pia kuongeza idadi ya wabunge na madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo nguvu ya chama haipo mikononi mwa mgombea urais kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF. Kuna watu wanadhani Mhe.Kikwete peke yake ndiye aliyeshindwa lakini si kweli kwani ni CCM.
Kwa sasa CCM ilipofika ni ngumu kaka mleta mada.
Hilo litawezekana kama ndani ya CCM hakutakuwa na mgawanyiko au UFISADI coz at this time when u talk about CCM ina maana u talk about ufisadi.
Sasa JE, ni nani wa kuzuia UFISADI ndani ya CCM wakati ufisadi ndiyo unatumika kumpata Mgombea wa Urais ndani ya CCM???
Hata kama Rais atakuwa ni wa kutoka huko CCM hakuna atakayeweza kuleta maisha bora ya Kweli ya mtanzania.
e.g: mfano rahisi na halisia: Nani wa kurudisha reli njia zote zifanye kazi, cement, mafuta ya petrol na diesel zibebwe na treni, naaaniiii!¿???? Ajitokeze.
Ujue nilichojifunza leo, ni kwamba wewe Lizaboni, una uelewa mkubwa sana, lakini kuna wakati huwa unaamua kuondoa uelewa wako ili kucheza ngoma ya akina Mwigulu Nchemba. Yaani hoja uliyoijenga hapa imekaa vizuri sana, kwamba CHADEMA na CCM wote ni watanzania, na kila tunachokifanya ni kwa ajili ya watanzania, whether ni CCM au ni CHADEMA wote wana haki sawasawa ya kushika madaraka na kuongoza nchi. Kwahiyo hatuna haya ya kuchukiana kibinadamu bali tushindane kwa hoja. Na yeyote kati yetu akiwa na hoja nzuri basi asikilizwe. Hii ni message mhimu sana kwa Mwigulu Nchemba. Huwa anadhani wapinzani ni watu wa kutoka nchi jirani, na wakiongea jambo anawachukulia kwamba ni wageni wanaoingilia mambo ya ndani ya watanzania.
Mimi binafsi sina mtizamo huo. Bali nilichojaribu kukieleza katika post yangu ni ukweli kwamba CHADEMA wana dira, na si kweli kwamba hawana dira kama ambavyo wewe unataka kutusadikisha. Kama wasingekuwa na dira, ni dhahiri wasingeweza kutoa mawazo kwa chama tawala na yakakubaliwa.
Ni kweli natamani sana chama chetu kifikie kuwa chenye nguvu kama vile vyama vya labour na conservatives vya UK au Republicans na democrats ya USA. Na kwa hakika tunakoelekea CHADEMA ni huko. Ni jambo la kutia moyo sana, lakini bado tunahitaji kuwekeza zaidi.Mkuu, umegusia maeneo ya msingi japokuwa kuna upotofu katika hoja juu ya vyama vikuu vya upinzani kupoteza nguvu baada ya kushindwa uchaguzi. Vyama kama NCCR Mageuzi na CUF havikupoteza nguvu kwa sababu ya CCM kuimarika bali kwasababu ya uongozi wa vyama hivyo kudhoofika.Vyama hivyo vilikuwa mifukoni mwa viongozi ndiyo hadi sasa ujiulize CUF bila Lipumba kinaendaje? Mpaka sasa, CHADEMA kwa asilimia zaidi ya 70 kimevuka mstari huo kwani kinazidi kujengwa katika mfumo wa kitaasisi na ndiyo maana kuna viongozi wanaosimamia chama kutoka kila kanda. Lakini pia focus ya CHADEMA siyo Ikulu tu bali pia kuongeza idadi ya wabunge na madiwani kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo nguvu ya chama haipo mikononi mwa mgombea urais kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF. Kuna watu wanadhani Mhe.Kikwete peke yake ndiye aliyeshindwa lakini si kweli kwani ni CCM.
Kwa sasa CCM ilipofika ni ngumu kaka mleta mada.
Hilo litawezekana kama ndani ya CCM hakutakuwa na mgawanyiko au UFISADI coz at this time when u talk about CCM ina maana u talk about ufisadi.
Sasa JE, ni nani wa kuzuia UFISADI ndani ya CCM wakati ufisadi ndiyo unatumika kumpata Mgombea wa Urais ndani ya CCM???
Hata kama Rais atakuwa ni wa kutoka huko CCM hakuna atakayeweza kuleta maisha bora ya Kweli ya mtanzania.
e.g: mfano rahisi na halisia: Nani wa kurudisha reli njia zote zifanye kazi, cement, mafuta ya petrol na diesel zibebwe na treni, naaaniiii!¿???? Ajitokeze.
Umeibua tuhuma nzito sana, ambazo sina uwezo wa kuzijibu. Naomba taarifa hii iwafikie Tumaini Makene, Ben Saanane, Kitila Mkumbo, @Dr Slaa, na Molemo naamini watakuwa na maelezo yanayojitosheleza kuhusiana na utendaji kazi wa ofisi ya CHADEMA makao makuu.Mkuu Lukolo, inawezekana kabisa ndani ya CHADEMA kuna watu ambao wana malengo mazuri na mtazamo hasi dhidi ya taifa hili. Binafsi kuna wakati namkubali sana Freeman Mbowe kwani ni mtu anayeshaurika na wakati fulani hujivalisha uzalendo. Ila sikubaliani kabisa na dr slaa ambaye kwake upinzani ni uadui. Mathalan, huwezi kuwa na malengo ya kwenda ikulu huku ukitukana viongozi waliopo madarakani na wa vyombo vya dola. Huko ni kufilisika kabisa kimawazo. Hata kama mtu humpendi lakini si kila kitu unampinga. Binafsi nilifarijika sana kuona mathalan mbowe na cuf walifikia muafaka mzuri kwa maslahi ya taifa baada ya kutokea mgogoro wa ushoga baina ya vyama hivi viwili. Ingekuwa dr slaa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni, ni wazi kuwa jambo lile lingeleta mtafaruku mkubwa sana nchini.
Pia CHADEMA wana tatizo kubwa la kupoteza uaminifu kwa watu ambao hawatoki mikoa ya kaskazini. Mathalan, zitto kabwe ni Naibu Katibu mkuu wa CHADEMA, lakini kwa zaidi ya miaka 3 sasa hajawahi kufanya kazi zake kama naibu hata pale dr slaa anapokuwa nje ya nchi. Badala yake John Mnyika ndiye huaminiwa na kupewa mikoba yote. Hata mbowe anaposafiri pia majukumu yakehutekelezwa na Mnyika na si Said Arfi. Kwa mtindo huu bwana Lukolo usitegemee kuwa CHADEMA watakuja kuwa chama imara na shindani kwa siku zijazo. Mie nakubaliana na wewe kuwa endapo hawatajirekebisha na hatimaye kushinda uchaguzi wa 2015, ni wazi kuwa huo ndio utakuwa mwisho wao
Mimi ninachohitaji ni maisha bora. Hata raisi akitoka CCJ au mgombea binafsi, kwangu ni sawa. Sitapiga kura kuchagua chama, nitapiga kura kuchagua mtu makini kwa nafasi ya diwani, mbunge na hata Raisi. Kuendekeza mahaba kwa vyama badala ya mtu makini ndo yamemwingiza Kikwete ikulu muhura wa Pili.
Hii ni changamoto ya kuongeza nguvu kubomoa ngome ya ccm ambayo ni vijijini. Ukweli ni kuwa sehemu kubwa ya vijijini CDM haijulikani. Watu ameisikia lakini CDM hawajafikisha elimu ya uraia huko. Hatuna wanachama wala matawi huko. Uelewa wa mjini ni tofauti na wa vijijini. Na hawa ndo wanaweza kuipa ccm ushindi miaka ijayo. Tusipoibomoa ngome hiyo, ni kweli twaweza tusishinde! Mikutano ihame mijini na kuhamia vijijini.