CHADEMA isiiachie Kigoma

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,224
Salum Msabaha jana akiongea na wananchi wa Kigoma amesema kwamba hata kama CHADEMA watakataa kukubali kukabidhi madaraka ya Halmashauri ya Kigoma Ujiji,CCM wataingia ofisi za Halmashauri hiyo kumsimika meya wao mpya kwa shamrashamra za matarumbeta

jee CHADEMA ikubali kukabidhi madaraka kwa kuheshimu muafaka wao na CCM au wakatae. na jee kuna sheria yoyote inayoweza kutumika kuwalazimisha kukabidhi madaraka au kuwalinda wasipokabidhi madaraka hayo kwa CCM. Na msimamo wa CHADEMA katika hili ukoje? Nadhani kwa faida ya Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar,CHADEMA isiiachie Kigoma kutawaliwa na CCM!
 
Sakata la Kigoma likoje ? Hili kila mara nashindwa kulielewa kabisa .Niwekeni sawia hapa .
 
Ninavyoelewa mimi ni kuwa kulikuwa na stalmate kwenye uchaguzi wa kuiongoza Kigoma kutokana na kuwa na idadi inayoshabihiana ya madiwani. Chadema watakuwa wanafanya jambo lisilo la busara kwa kujiingiza kwenye mgogoro ambao hautakiwi uwepo kwani muafaka ulishawekwa sawa kati yao na CCM. Wasisahau kuwa CCM hawaihitaji Kigoma bali kama Chadema watafanya vurugu, itawapa CCM kiambatanishi cha kuonyesha jinsi wapinzani wasivyo na msimamo katika makubaliano.
 
Wakuu hapa nitatofautiana kidogo na wachangiaji wengi, kigoma baadaya kuonekana matokeo ya kura za meya zinalingana wakafanya makubaliano hayo. sasa ndugu zangu kwa maana hiyo sasa na Msabaha alivyosema wasimika Meya wao kwa maturunbeta hata Chadema wakigoma, what Next? Vurugu,fujo,vifo! at end of the day........ Noooooo sikubali
 
Sakata la Kigoma likoje ? Hili kila mara nashindwa kulielewa kabisa .Niwekeni sawia hapa .

Kigoma kama ilivyo Pemba kwa miaka mingi wamekuwa wanalalamika kwamba wanatengwa na serikali katika kuwapelekea maendeleo,na siyo sasa tuu hata wakati wa mfumo wa Chama kimoja.

Tatizo limeanza pale CHADEMA na CCm kufungana katika idadi ya madiwani wanaotakiwa kuchagua meya na kwa kuwa wanapiga kura kwa kufungamana na chama (Party lining voting) isingewezekana chama chochote kati ya hivyo viwili kushinda

ukapendekezwa muafaka wa kuongoza Halmashauri hiyo kwa kupokezana kwa miaka miwili na nusu kwa kila chama. Sasa zamu ya CHADEMA inakwisha mwezi julai 2008. Ndiyo CCm wana shaka kwamba huenda CHADEMA hawatakabidhi madaraka kwao!

Jambo ninaloliona hapa kwangu ni kwa nini CCM inataka uungwana katika kutekelezwa kwa muafaka wa Kigoma wakati wao hawajawahi kuonyesha hata siku moja uungwana wa kujaribu achilia mbali kutekeleza muafaka wa Zanzibar!
 
CHADEMA haiwezi kuafford ujeuri wa mtindo huo at this point. Kumbuka kuwa mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wote ni CCM iwapo CHADEMAwataleta ubishi watawaumiza wananchi kwa sababu it is clear kwamba viongozi hawa hawataitambua halmashauri itakayokataa kuheshimu makubaliao ya awali.

Kama CHADEMA wanajali maslahi ya wananchi basi waheshimu makubaliano waliyowekea sahihi.
 
Hakuna jinsi CHADEMA lazima watuonyeshe busara zao kwa kuachia madaraka kama walivyokubaliana na CCM, bila hivyo itaonyesha hata vyama vya upinzani havijali suala zima la utawala bora na suala zima la demokrasia. muafaka wa CCM na CUF ni tofauti na huu wa CHADEMA na CCM kwa sababu walikwisha maliza tofauti zao na walikuwa wanaendelea na shughuli kama kawaida.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom